joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Ninaomba kuwasalimia wana jamii kwa jina la utukufu wa juu, pili ningependa kuwaomba tujadili kuhusu mgawanyo wa bajeti ya Kenya katika sekta za kilimo na Elimu.
Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa la Kenya, zaidi ya 75% ya Wakenya huishi vijijini kwa kutegemea Kilimo, kilimo ndicho kinachotoa ajira nyingi zaidi kuliko sector yoyote ile, ni namba mbili kwa kuipatia Kenya fedha za kigeni, kilimo ndicho kinachotegemewa kwa kuzalisha malighafi za viwandani.
Kenya ni nchi yenye kukumbwa na njaa kila mwaka na watu wengi hufariki kutokana na njaa, Kenya ni nchi pekee hapa Afrika ambayo inategemea Chakula cha msaada kulisha watu wake isiyokuwa na vita vya ndani.
Kenya ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo kama ingetumia ardhi yake vizuri kwa kuwekeza katika miradi mikubwa mikubwa ya umwagiliaji kama ule wa Galana kulalu, ingeweza kuzalisha Chakula cha ziada hata kusafirisha nje ya nchi.
Hivi katika mazingira hayo ambapo uchumi wa nchi umeshikiliwa na Kilimo, kuwekeza $500M katika wizara ya Kilimo na kuwekeza $5B katika Elimu?. Ikumbukwe kwamba Elimu kimsingi ni miongoni mwa "recurrent expenditure", kwamba pesa nyingi hutumika kulipa mishahara ya walimu, wakati kwenye KILIMO asilimia kubwa huingia katika uwekezaji hivyo kuzalisha pesa nyingi zaidi ili kuendesha uchumi WA nchi na kupunguza gharama za maisha.
Naomba kuwasilisha.