Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani


Msikilize hapo akiongea akiwa na Karume.

Kijana mdogo sana miaka 29 akapindua nchi. Bila Okello Zanzibar ingekua bado chini ya Sultani.

Okello tutakukumbuka Daima, haijalishi umekufa ila kumbukumbu yako haitafutika.
Hii video Kuna wazenj /Islam watapita kama hawaioni!hawapendi kukili Mkristo John Okelo,ndio aliongoza mapinduzi,
 
Tuache upotoshaji...unasema Karume akaitwa ili alejee kukalia kiti chake. Unataka kusema Karume alikua amefukuzwa na kunyanganywa madaraka yake na waarabu?

Pili tunaweza kukubaliana kua Karume alikua mafichoni wakati wa mapinduzi na kwa maana hiyo Karume akushiriki mapinduzi moja kwa moja. Mwisho tuelewe kua mtangaza mapainduzi na mafanikio ya kupindua ndiye kiongozi wa mapinduzi. HONGERA SANA JOHN OKELLO kwa kuongoza harakati za Uhuru dhidi ya Sultan Jamshid
 
Bish...
Huwezi kuanza kuyaeleza mapinduzi pale John Okello alipozungumza kwenye radio.

Historia ya mapinduzi inaanza nyuma sana kwenye kuweka mipango ya kupindua serikali ya ZNP/ZPPP.

Kuna nafasi ya Hanga na Kambona.

Kuna viongozi wa Kambi ya Kipumbwi.

Kuna vyombo vya usalama vya Tanganyika.

Kuna mchango wa Israel na Algeria na Waingereza pia.

Ukipita huku kote utaielewa historia ya mapinduzi.

Nakushauri umsome Dr. Harith Ghassany.
 
Huyu Ali Mwinyi Tambwe si ndiye yule aliyekuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
James...
Ndiye yeye na ndiye aliyekwenda Nansio kwa Hamza Mwapachu na Abdul Sykes kutaka ushauri wa kumwingiza Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA 1953 kisha waunde TANU 1954.
 
Nikadhani upo kwenye hoja ya nani aliongoza mapinduzi kumbe upo kwenye ukristo
 
Kama hampendi, na ikiwafurahisha, mkapande pipa Muelekee Omani.

Msituharibie nchi na Ukimbari wenu huo
 
Umekover mjadala wote

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Sela...
Nakuwekea picha hiyo hapo chini itazame na linganisha:


Hii picha hawa Makomredi wamesimama wapigwe picha na picha hii imepigwa mapinduzi yameshatokea siku chache zilizopita.


Picha hii imepigwa Okello anawekewa silaha na yeye mwenyewe ameshika silaha apigwe picha.

Katika hiyo picha ya Makomredi wawili nimepata kuzungumza nao Amour Dughesh na Hashil Seif.

Dughesh alinionyesha picha nyingine ya yeye na comrade mwingine ambae ni rafiki yangu wakiwa kwenye combat wameshika bunduki wako lindoni.

Picha hii ni tofauti na picha hiyo ya kwanza hapo juu.

Nakuwekea na picha nyingine hapo chini lakini huyu kwa mjuonekano wake ni ''askari'' tofauti sana na waliomzunguka Okello.

''Eti utafiti.''

''No research no right to speak.''
Chairman Mao.

Utafiti ndiyo msingi wa elimu.
Si kitu cha kubeza au kukejeli.

Nimemjua vipi Comrade Hashili Seif:

 
Sasa anawekewa ya nini na tayari ameshika silaha? But why wafanye hivyo kwa mtu ambaye hahusiki na mapinduzi? Sometimes sijui mnatufikiriaje. Mara sauti yake ilihitajika kuwatisha wazanzibar maana wao ni waoga. Baadaye tena picha zake zinatakiwa kuwatisha akina nani? Wazanzibar hao hao? Please....mumkumbuke John Okello ana mchango Mkubwa sana katika kuikomboa Zanzibar. Dini yake ya kiasili au yoyote isiwe sababu ya kuficha tendo lake la kishujaaa....
 

Moja ya wazee wa hovyo,mamruki wa waarabu huyo.
 
Chizi...
Sijasema Okello hakuhusika na mapinduzi.
Waliohusika na mapinduzi ni wengi sana.

Nakuwekea picha ya mwana ASP ambae hujapata kumsikia lakini ana mchango mkubwa.

Bahati mbaya inaelekea wengi hampendi kusoma lakini mnapenda mjadala unaoufanya bila ya kuwa na elimu ya kutosha ya somo unalojadili.

Kushoto: Mohamed Omari Mkwawa jina alilopewa na Mzee Karume ni Tindo kila penye ugumu Karume alimpeleka yeye, huyu ndiye mvushaji wa Wamakonde kutoka Kipingu hadi Kizimkazi; Maulid Sheni kiongozi wa vyama vya wafanyakazi Zanzibar mwana ASP shupavu na mkusanyaji wa Wamakonde Kipumbwi. Picha hii ni kutoka kitabu, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.'' Haya yalikuwa mazungumzo ya mwisho katika utafiti baada haya kitabu kikachapwa Marekani 2010.
 
Kwanini ukielezwa kitu huwa unaanza kuwa haujaja kushindana? Nimekuuliza swali unasema wamakonde ndio waliokifanya kazi kwenye mkonge ila nikakueleza kuwa mbona wapo wamwera kibao walikuwa wanafanya hiyo kazi
 
Kwanini ukielezwa kitu huwa unaanza kuwa haujaja kushindana? Nimekuuliza swali unasema wamakonde ndio waliokifanya kazi kwenye mkonge ila nikakueleza kuwa mbona wapo wamwera kibao walikuwa wanafanya hiyo kazi
Mnachi...
Sababu ni kuwa mimi nimetafiti na nimefika hadi Kipumbwi na nimezungumza na Victor Mkello na msaidizi wake Maulid Sheni.

Nimefika hadi Sakura walipokuwa wanaishi Wamakonde kwa ufupi nayafahamu haya mambo kupita wewe.

Ndiyo unapokataa kusikiliza utafiti naamua iwe basi amini upendacho hapana haja ya ubishi.

Mimi niko hapa kuisomesha historia ambayo kabla haikuwa inajulikana.
 

Wewe kila kitu umetafiti, vingi tu unasimuliwa na kuunda historia yako.

Okello ndiye jemedari wa mapinduzi hao wengine walishindwa kazi wakaishia kujigicha mafichoni wakisubiri mwanaume apige kazi.

Ugumu unakujia wapi ku appreciate kazi aliyoifanya okello na iko wazi kabisa.
 
Sela...
Nakuwekea picha hiyo hapo chini itazame na linganisha:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…