Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani


Msikilize hapo akiongea akiwa na Karume.

Kijana mdogo sana miaka 29 akapindua nchi. Bila Okello Zanzibar ingekua bado chini ya Sultani.

Okello tutakukumbuka Daima, haijalishi umekufa ila kumbukumbu yako haitafutika.
Kama Okello hakuhusika hapo kwenye mahojiano muhimu anafanya nini? Wala urojo wakubali tu Okello ndo alifanya mambo, Karume alilaza
 
Mohamed Said hawezi kukuletea story za John Okello kuwa Ni shujaa kwasababu sio mwislamu
Last...
Hapana historia ya Okello naifahamu vyema.

Na sijui kwa nini wengi wenu hapa mnashikilia kuwa alikuwa mtu muhimu sana kiasi mnasema ni baba wa taifa la Zanzibar.

Nimejitahidi kueleza historia ya mapinduzi na mipango yake na pia kukuelezeni wahusika wakuu lakini inaelekea hamtaki kusikia.

Mnataka kuifanya historia ya Okello kuwa historia ya Mkristo aliyekuja kuwaokoa Waislam Waafrika waliokuwa wanakandamizwa na Waarabu.

Hii siyo historia ya mapinduzi.
 
Nadhani Okello angekuwa mwislamu mpaka leo mchango wake ungekuwa unaimbwa Zanzibar. Hata kama ni kidogo
 
Mleta mada ficha ujinga wako, Okello kamuondoa mkoloni gani?

Mohamed Said hawezi kukuletea story za John Okello kuwa Ni shujaa kwasababu sio mwislamu
Nadhani Shida kubwa ipo Hapa. Na wanajaribu sana kumzika kwenye hili Tukio. But watu hatudanganyiki. John Okello baba wa Taifa la Zanzibar.
 
See... Nlisema mimi shida ni DINI YA OKELLO. UKRISTO WAKE NDO UMEMPONZA WATU WA ZANZIBAR HAWATAKI IONEKANE ALIKUWA MWAFRIKA ALIYEKUJA OKOA WAAFRIKA WENZIE. WANAFIKIRIA KWANZA JINA LAKE. MAANA UNAWEZA KUTA HATA HAKUWA MKRISTO ILA ANA JINA LA KIKRISTO.
 
Mouse...
Lafidhi yake radioni ilotumika kuwatisha watu.
Kwani lafudhi ya sauti ni issue si unaigiza tu.
Kwahiyo, unataka kusema kuwa wazanzibari ni watu wa kuogopa sauti?( Nashangaa kidogo).
Mimi najua kuwa wanaoogopa sauti ni watoto wadogo, lakini mtu mzima humwangalia yule anayetoa sauti na hufanyia maamuzi mwonekano siyo sauti.
KIFUPI: JOHN OKELLO ndie aliyeongoza mapinduzi Zanzibar, na ndio maana wote waliokuwepo hapo kwenye video wanakubaliana kuwa John Okello ndiye aliyefanikisha zoezi hilo.
Katika uandishi wa historia, "eye witness" ndio mtu wa kwanza wa kupata"trusted information", na siyo tunatumia taarifa za mtu aliyekuwa Tabata( DSM) wakati wa mapinduzi. Tukitumia taarifa za mtu aliyekuwa DSM wakati wa mapinduzi tunapata "fabricated information". Vinginevyo mtu huyo awe na "connection" na mwanamapinduzi huyo au kikundi chake, tutachanganya na REASONING.
 
Museme kwa nyerere pia mpikaji na mpotoshaji wa histori! Nyerere alikuwa wa mchongo na aliipika historia ya Tanzania shem on her
Una miaka mingapi?, Maana wewe pengine hukuwepo wakati wa NYERERE na umesimuliwa tu.
NB
Kuna mitazamo miwili ya uandishi wa historia.
"Bourgeoisie perceptions" na " Marxist perceptions".
Inategemea unatumia mtazamo gani kuandika historia yako.
By the way, sijaona kitabu cha historia alichoandika NYERERE.
Nimesoma vitabu vya historia ya Tanzania vilivyoandikwa na I .KIMAMBO, John Illife, Ogot,nk. Sijamwona NYERERE ( tutajie kitabu cha historia alichoandika Nyerere, na kama siyo chuki binafsi dhidi ya Nyerere).
Tuache kuwasingizia watu vitu ambavyo hawakutenda kwa maslahi yetu.
 
Una uhakika gani hiyo picha ya mwanzo ndio ya 1964 na siyo hiyo ya chini ya Okelo Kwamba Ni ya siku za mbele baada ya Uhuru huo?
NB kwa wazoefu wa harakati za kivita, asiye kamanda kabisa Hana Uhuru wa kuwasogelea makamanda Kama vile, huwa hajiamini na kwa namna flani hujitofautisha hats kwa muonekano wa uso wake uliojaa uoga mkuu.
Mzee lazima ukubaliane hata moyoni John O Ni moja ya makamanda waliojitolea maisha yao bila malipo kuhakikisha wanaondoka wadhalimu. Na kwa moyo wangu naamini John hata baada ya kuondoka visiwani alikosekana tu mtu wa kushirikiana nae kuikomboa Afrika iliyokuwa ikipigana kuwaondoa wadhalim wa ulaya huko Angola, Kongo, Mozambique.
Na pengine leo John angekuwa shujaa wa kuimbwa Kama Che,Mandela nk.
 
Nyerere kwangu ni wa mchongo! Nasisitiza hilo
 
See... Nlisema mimi shida ni DINI YA OKELLO. UKRISTO WAKE NDO UMEMPONZA WATU WA ZANZIBAR HAWATAKI IONEKANE ALIKUWA MWAFRIKA ALIYEKUJA OKOA WAAFRIKA WENZIE. WANAFIKIRIA KWANZA JINA LAKE. MAANA UNAWEZA KUTA HATA HAKUWA MKRISTO ILA ANA JINA LA KIKRISTO.
Alikuwa na jina la kizungu ila hakuwa Mkristo.

Kuna mahojiano anasema Mungu wake wa kiafrika, Sasa huo Ukristo umetokea wapi?

Ila kiukweli Wazanzibari ni watu waongo kupita maelezo kutomtambua baba wa Taifa lao.

Ni sawa na kusema wamakonde kupelekwa kule kitu ambacho sio kweli nadhani ni Vijana kutokea kusini mwa nchi ikijumlisha wayao, Wamakua,Wamwera,Wamakonde mpaka Wamatumbi walikuwepo ila jina lao maarufu lilikuwa Chinga
 
Sela...
Ukweli ni kuwa binafsi huu mjadala unanifundisha mambo ambayo hayakunipitia kabla.

Kubwa ni utambuzi kuwa wengi wetu hatusomi vitabu hata vya hayo tunayoyapenda na hapa sisi tuko katika ukumbi wa historia.

Chukua mfano huu wa Okello kufananishwa na Che Guevara na Nelson Mandela.

Okello mwenyewe alijipa cheo cha Field Marshall.

Okello kajiona yeye ni sawasawa na Field Marshall Tito wa Yugoslavia aliyepigana na Wajerumani Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945).

Inahitaji kwanza uijue historia ya Tito na jeshi lake la Partisan katika uwanja wa mapambano ndiyo uweze kuona kioja cha John Okello na uweze kujicheka wewe mwenyewe.

Okello kufananishwa na Mandela ni kioja kingine.

Unahitaji uisome historia ya Mandela ndiyo uone kuwa hakuna njia yeyote ambayo unaweza kumfananisha Okello na Mandela.

Okello kumfananisha na Che Guevara ni kioja kingine.

Che na Castro hawa wako mbali sana na hata wanamapinduzi wenye sifa za kufahamika.

Mtafuteni Marshall Tito katika kitabu hiki: "The Rise and Fall of the Third Reich," Mtafute Mandela katika kitabu alichoandika mwenyewe kwa mkono wake, "Long Walk to Freedom."

Angalieni movie hii ya Tito: "The Fifth Offensive."

Jifunzeni kwanza kusoma muelimike.

Elimu ndiyo itakupa maarifa ya kujadili na uwezo wa kuchambua mambo mengi.

 
Mzee hujui kuwa sio kila utafiti ni sahihi? Ni mara ngapi tulisikia dawa fulani iligundulika baada ya utafiti kuwa haifai tena kwa matumizi baada ya kubainika mapungufu yake?
Mzee hujui kuwa kuna watu huwa wanaingiza interest zao kuhalalisha jambo fulani in the name of research?
Mzee umesahau kuwa hata Lamack na Darwin wamepingana kwenye mchakato mzima wa Evolution huku kila mmoja akitetea hoja zake kupitia utafiti?

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo lako wewe unajifanya mjuaji sana angalia hapo unapojisifu eti unajua vingi kuliko mimi...ulisema waliokifanya kazi kwenye mashamba ya mkonge ni wamakonde nikakuuliza mbona mimi nawajua wazee wengi wa kimwera na kiyao waliokaenda kufanya kazi kwenye mashamba ya mkonge? Kwanini uwataje wamakonde tu?
 

Hata wanyamwezi na wasukuma wengi tu walikuwa manamba kwenye mashamba ya mikonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…