Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mnachihangu,Tatizo lako wewe unajifanya mjuaji sana angalia hapo unapojisifu eti unajua vingi kuliko mimi...ulisema waliokifanya kazi kwenye mashamba ya mkonge ni wamakonde nikakuuliza mbona mimi nawajua wazee wengi wa kimwera na kiyao waliokaenda kufanya kazi kwenye mashamba ya mkonge? Kwanini uwataje wamakonde tu?
Nimekujibu suala la Wamakonde kwa kukueleza kuwa Wamakonde walitawala kazi ya kukata mkonge kuliko makabila mengine yote ya Tanganyika.
Huu ndiyo ukweli wa historia.
Wala sijifanyi najua.
Kuwa najua ni kweli najua.
Ukitaka ushahidi zaidi kuhusu Wamakonde wa Kipumbwi soma kitabu cha Dr. Ghassany, "Kwaheri Ukoloni..." utaona na picha zao na utasoma waliyosema.
Mimi kusema najua si majisifu ni kweli historia hii naifahamu vizuri.
Unahitaji utulivu na kusoma ninayoandika utajifunza mengi.
Ikiwa hutaki kukubali sikulazimishi.