Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Sela...Field marshal Ni jina tu la kujikweza baada ya ushindi dhidi ya udhalimu alilojipa John O. Pengine.
Ha ha ha Askari mlinda benki. Mzee wangu kuwa mtaalam wa historia si kujua vyote on Sasa umeanza kejeli.
Kwa namna yoyote ile matokeo ya tafiti huwa hayaachi kumtikisa mtafiti, Kwa Aina ya uandishi na uanazuoni wako hata kitokee Nini usingekuwa tayari kuandika ukweli kuhusu John.
Si lazima ukubali ñiandikayo.
Katika tafiti nilizofanya wote waliopata kunipinga hakuna aliyefanya hivyo kwa ushahidi wa utafiti mwingine ila kwa hisia zake tu.
Tafiti zimeninyanyua juu hazikunitingisha.
Nimealikwa vyuo vingi kuzungumza niyajuayo katika historia ya Tanganyika.
Kazi yangu ni kueleza yale niyajuayo.
Ukipenda amini usipopenda kuamini na ukaamini hisia zako kwangu ni sawa.
Si kejeli huyo askari yuko katika video clip nje ya benki.
Nilitumiwa nimtambue kama ni katika makomredi au Mmakonde kutoka Kipumbwi.
Walioniletea wanauthamini ujuzi wangu.
Nieleza kuwa makomredi muonekano wao ni mwingine kabisa na hawana haiba hiyo.