Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Field marshal Ni jina tu la kujikweza baada ya ushindi dhidi ya udhalimu alilojipa John O. Pengine.
Ha ha ha Askari mlinda benki. Mzee wangu kuwa mtaalam wa historia si kujua vyote on Sasa umeanza kejeli.
Kwa namna yoyote ile matokeo ya tafiti huwa hayaachi kumtikisa mtafiti, Kwa Aina ya uandishi na uanazuoni wako hata kitokee Nini usingekuwa tayari kuandika ukweli kuhusu John.
Sela...
Si lazima ukubali ñiandikayo.

Katika tafiti nilizofanya wote waliopata kunipinga hakuna aliyefanya hivyo kwa ushahidi wa utafiti mwingine ila kwa hisia zake tu.

Tafiti zimeninyanyua juu hazikunitingisha.

Nimealikwa vyuo vingi kuzungumza niyajuayo katika historia ya Tanganyika.

Kazi yangu ni kueleza yale niyajuayo.

Ukipenda amini usipopenda kuamini na ukaamini hisia zako kwangu ni sawa.

Si kejeli huyo askari yuko katika video clip nje ya benki.

Nilitumiwa nimtambue kama ni katika makomredi au Mmakonde kutoka Kipumbwi.

Walioniletea wanauthamini ujuzi wangu.

Nieleza kuwa makomredi muonekano wao ni mwingine kabisa na hawana haiba hiyo.
 
Walioteseka walipinduliwa na kukimbizwa Zanzibar. Sasa wamebaki wazalendo wanakula maisha. Wengine waliobaki ni Vibaraka wa waliokimbizwa baada ya Mapinduzi.
Komeo...
Unazungumza kwa hisia zako si kwa utafiti.

Wakati wa utafiti wa kitabu, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," nilipata fursa ya kukutana na wengi walioshiriki katika mapinduzi katika nyumba zao walizokuwa wakiishi.

Nimeshuhudia kwa macho yangu ugumu wa maisha yao.

Nimekutana na wagonjwa ambao hawawezi kujitibia.

Nimewaona watu wazima waliochoka wamepanga chumba kimoja banda la uani.

Nimewaona waliokuja kutuona kwa mahojiano wamevaa kandambili zilizochoka.

Nimekutana na waliopinduliwa Dubai, Muscat, London, Berlin na Humburg na wengine nimekutananao wakija Zanzibar likizo.

Hawa ni watu ninaojuananao vyema kabisa.

Nayajua haya mambo vizuri sana.
 
Nlimjibu mhusika kutokana na namna ambavyo aliandika. Maisha yao hayawezi kuwa 100 mazuri. Nenda hata SA. Waliopigania uhuru wengine wapo taabani, nenda afghastan, nenda Egypt, nenda Zimbabwe. Kote Duniani pako hivyo. Why? Je baada ya uhuru walifanya nini hata Bara tu. Wapo wapigania Uhuru ambao wanatamani arudi Mkoloni.
 
Umesema kweli lakini wewe ulileta hoja ya Zanzibar nami nikakujibu kwa hoja ya Zanzibar.
 
Si kweli kuwa wote watakuwa na maisha mazuri. Na kuwa waliopinduliwa wana maisha mabaya. Si kweli. La msingi baada ya mapinduzi. Serikali ilijipanga vipi. Baada ya Uhuru nchi zilijipanga vipi. Kuna watu wanakumbuka na kuona nyuma kulikuwa bora kuliko sasa.
 
Mzee wako barua ya Cheguevara aliipokea kwa posta au DHL?

Ule uzi mwingine anasema Karume alikuwa anapiga simu kuulizia updates? Miaka 1960’s Simu zilikuwepo kutoka Dar kupiga Zanzibar?
 
Tatizo lako wewe unajifanya mjuaji sana angalia hapo unapojisifu eti unajua vingi kuliko mimi...ulisema waliokifanya kazi kwenye mashamba ya mkonge ni wamakonde nikakuuliza mbona mimi nawajua wazee wengi wa kimwera na kiyao waliokaenda kufanya kazi kwenye mashamba ya mkonge? Kwanini uwataje wamakonde tu?
Kipumbwi umefika?
 
Si kweli kuwa wote watakuwa na maisha mazuri. Na kuwa waliopinduliwa wana maisha mabaya. Si kweli. La msingi baada ya mapinduzi. Serikali ilijipanga vipi. Baada ya Uhuru nchi zilijipanga vipi. Kuna watu wanakumbuka na kuona nyuma kulikuwa bora kuliko sasa.
Komeo...
Sina haja ya kukueleza yaliyotokea baada ya mapinduzi.

Hii ni historia ya pekee na inafahamika.

Nakushauri isome historia hadi kufikia kuuliwa kwa Karume.
 
Kwa mujibu wa sheikh rogo anadai Nyerere ndie kamuua Karume
 
Yaani haiingii akilini eti wengine wafanye mapinduzi ila kwenye kutangaza kuwa wameshinda wanaogopa mpaka wakaenda mitaani kumtafuta Okello aje awatangazie. Huyu mzee side boi anatuona sisi kama watoto wadogo sana kwamba hatuwezi kuhoji wala kufikiri.

Sasa swali linakuja kwanini hao anaosema wapigania mapinduzi waliogopa kukaa front?mpaka wakakimbilia tanganyika.
Hapo asingekuwa John bali ali angekubali
 
Mna...
Ilikuwa kiasi cha kama saa tatu hivi mimi, Dr. Harith Ghassany na Mzee Mkwawa tulipofika Kipumbwi.

Kwa asili ni kijiji cha wavuvi.

Asubuhi ile radio zote FM Stations nimeshangaa zimekamata Zanzibar zinapigwa nyimbo za taarab.

Sababu ni kuwa Kipumbwi ni karibu mno na Zanzibar usiku unaziona taa za Zanzibar.

Mzee Mkwawa akatuonyesha myumba ambayo wakati ule ilikuwa hoteli wakila chakula cha usiku kabla hawajaingia katika majahazi kuvuka kwenda Zanzibar.

Akatupeleka kwenye uwanja ambao walikuwa wanawapa Wamakonde mazoezi ya vita.

Baada ya hapo akatutumbukiza chini ya ardhi.

Kwa nje ukitazama ni mchanga mweupe wa pwani ukiteremka unaingia chini kwenye pango kubwa juu ardhini limefichwa na majani tabu kujua chini yake kuna nini.

Hapa chini ndiyo yalipokuwa yakiegeshwa majahazi ya kuwavusha Wamakonde kwenda Zanzibar wakiwa na mapanga makali ya kukata mikonge.

Hawa Wamakonde pamoja na Mzee Mkwawa wamevaa marapurapu kama wavuvi wa Kidigo na kichwani wamevaa kofia za majani ya mnazi.

Tukafika Sakura Estate kwenye nyumba walizokuwa wakiishi Wamakonde si mbali na Kipumbwi.

Sikupata kumuona Dr. Ghassany kafurahi kama siku ile.

Kuna picha nimeshika video camera napiga picha huku naeleza kama hivi unavyosoma hapa.

Sijapata kumuona Dr. Ghassany amefurahi kama siku ile.

Tuko pwani maji kupwa tumesimama kwenye ardhi ambayo watu walioingia Zanzibar walikotokea.

Siri ambayo ilifichika kwa miaka mingi bila kufichuka kiasi haikuwa sehemu ya historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Kipumbwi ilikuwa sehemu kubwa sana ya msaada wa Tanganyika kwa ASP na Karume kupindua serikali ya ZNP/ZPPP iliyokuwa ikiongozwa na Mohamed Shamte.

Mpaka leo hakuna kiongozi yeyote wa Zanzibar ambae mimi nimepata kumhoji kuhusu Wamakonde aliye tayari kukubali kuwa kuliingia mamluki wa Kimakonde kutoka Tanganyika waliokuja kusaidia mapinduzi na hawa ndiyo walioua Waarabu wengi sehemu za shamba.

Baada ya Kipumbwi ilibaki kufanya mahojiano na Victor Mkello Kiongozi Mkuu wa wakata mkonge.

Kisa cha Victor Mkello ni historia nyingine.

Tulimkuta mgonjwa anahesabu siku zake kalalia kitanda cha mauti.
 
Mna...
Ilikuwa kiasi cha kama saa tatu hivi mimi, Dr. Harith Ghassany na Mzee Mkwawa tulipofika Kipumbwi.

Kwa asili ni kijiji cha wavuvi.
Asubuhi ile radio zote FM Stations nimeshangaa zimekamata Zanzibar zinapigwq nyimbo za taarab.

Sababu ni kuwa Kipumbwi ni karibu mno na Zanzibar usiku unaziona taa za Zanzibar.

Mzee Mkwawa akatuonyesha myumba ambayo wakati ule ilikuwa hoteli wakila chakula cha usiku kabla hawajaingia katika majahazi kuvuka kwenda Zanzibar.

Akatupeleka kwenye uwanja ambao walikuwa wanawapa Wamakonde mazoezi ya vita.

Baada ya hapo akatutumbukiza chini ya ardhi.

Kwa nje ukitazama ni mchanga mweupe wa pwani ukiteremka unaingia chini kwenye pango kubwa juu ardhini limefichwa na majani tabu kujua chini yake kuna nini.

Hapa chini ndiyo yalipokuwa yakiegeshwa majahazi ya kuwavusha Wamakonde kwenda Zanzibar wakiwa na mapanga makali ya kukata mikonge.

Hawa Wamakonde pamoja na Mzee Mkwawa wamevaa marapurapu kama wavuvi wa Kidigo na kichwani wamevaa kofia za majani ya mnazi.

Tukafika Sakura Estate kwenye nyumba walizokuwa wakiishi Wamakonde si mbali na Kipumbwi.

Sikupata kumuona Dr. Ghassany kafurahi kama siku ile.

Kuna picha nimeshika video camera napiga picha huku naeleza kama hivi unavyosoma hapa.

Sijapata kumuona Dr. Ghassany amefurahi kama siku ile.

Tuko pwani maji kupwa tumesimama kwenye ardhi ambayo watu walioingia Zanzibar walikotokea.

Siri ambayo ilifichika kwa miaka mingi bila kufichuka kiasi haikuwa sehemu ya historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Kipumbwi ilikuwa sehemu kubwa sana ya msaada wa Tanganyika kwa ASP na Karume kupindua serikali ya ZNP/ZPPP iliyokuwa ikiongozwa na Mohamed Shamte.

Mpaka leo hakuna kiongozi yeyote wa Zanzibar ambae mimi nimepata kumhoji kuhusu Wamakonde aliye tayari kukubali kuwa kuliingia mamluki wa Kimakonde kutoka Tanganyika waliokuja kusaidia mapinduzi na hawa ndiyo walioua Waarabu wengi sehemu za shamba.

Baada ya Kipumbwi ilibaki kufanya mahojiano na Victor Mkello Kiongozi Mkuu wa wakata mkonge.

Kisa cha Victor Mkello ni historia nyingine.

Tulimkuta mgonjwa anahesabu siku zake kalalia kitanda cha mauti.
Mpaka hapo nimeelewa kuwa unavyowaelezea wamakonde ni kama kwa kejeli hivi,
 
Hapo asingekuwa John bali ali angekubali
Edwayne,
Ukiondoa kejeli na ubishi utachota elimu nyingi na utajifunza mengi ambayo hukuwa unayajua.

Mimi binafsi kabla nilikuwa na picha yangu ya Wazanzibari.

Picha hii ni ya Wazanzibari rafiki wa baba yangu wakija nyumbani na wake zao.

Watu wapole wake zao wanawake wazuri wamependeza kwa mavazi wananukia udi.

Haikunipitikia kuwa Wazanzibari hawa hawa waliokuwa wakija kwetu wananiuliza kama nimekwisha khitimu Qur'an wanaweza kufanyiana yale niliyoyakuta katika mapinduzi.

ASP haikuogopa kutoa tangazo la kuanguka kwa serikali.

ASP walimpa radio Okello kuongeza "drama," katika yale yaliyokuwa yametokea usiku.

ASP ilitaka Wazanzibari waisikie sauti na lafidh ambayo hata siku moja haijasikika masikioni mwao.

Sauti hii na lafidh yake ilizua taharuki kubwa.
 
Mpaka hapo nimeelewa kuwa unavyowaelezea wamakonde ni kama kwa kejeli hivi,
Mnachihangu,
Sina haja ya kufanya kejeli.

Hapa nipo darasani nasomesha.

"Wamakonde" wa Kipumbwi na John Okello ni sehemu muhimu katika mauaji yaliyofanyika katika mapinduzi.
 
Kwahiyo wale wamwera na wayao waliokifanya kazi kwenye mashamba ya mkonge waliishia wapi?
 
Kwahiyo waliishia kwenye mashamba ya mkonge tu?
Mnachihangu,
Kwa nini unahangaishwa na kitu ambacho si sehemu ya historia ya mapinduzi?

Wabondei walikuwapo Kipumbwi lakini hawakuvushwa kwenda Zanzibar lau kama Victor Mkello ni Mbondei.
 
Back
Top Bottom