Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Upo Sahihi kabisa. Mfano mzuri tu humu ni 'Wamakonde' ....kimaumbile, hulka za kivita, na rangi!
Syll...
Wamakonde walikuwapo Kipumbwi wameajiriwa na Sakura Sisal Estate.

Si kama hili ni jambo la kuzua.
 
Mnachihangu,
Kwa nini unahangaishwa na kitu ambacho si sehemu ya historia ya mapinduzi?

Wabondei walikuwapo Kipumbwi lakini hawakuvushwa kwenda Zanzibar lau kama Victor Mkello ni Mbondei.
Kwanini walivushwa wamakonde tu na sio wengine?
 
Sela...
Nakuwekea picha hiyo hapo chini itazame na linganisha:

View attachment 2479862
Hii picha hawa Makomredi wamesimama wapigwe picha na picha hii imepigwa mapinduzi yameshatokea siku chache zilizopita.

africa-independence-zanzibar-tanzania.jpg

Picha hii imepigwa Okello anawekewa silaha na yeye mwenyewe ameshika silaha apigwe picha.

Katika hiyo picha ya Makomredi wawili nimepata kuzungumza nao Amour Dughesh na Hashil Seif.

Dughesh alinionyesha picha nyingine ya yeye na comrade mwingine ambae ni rafiki yangu wakiwa kwenye combat wameshika bunduki wako lindoni.

Picha hii ni tofauti na picha hiyo ya kwanza hapo juu.

Nakuwekea na picha nyingine hapo chini lakini huyu kwa mjuonekano wake ni ''askari'' tofauti sana na waliomzunguka Okello.

''Eti utafiti.''

''No research no right to speak.''
Chairman Mao.

Utafiti ndiyo msingi wa elimu.
Si kitu cha kubeza au kukejeli.

Nimemjua vipi Comrade Hashili Seif:

View attachment 2479876
Wew jamaa unatuona watoto sana[emoji1787][emoji1787]...

Ati anawekewa silaha...
 
Syll...
Wamakonde walikuwapo Kipumbwi wameajiriwa na Sakura Sisal Estate.

Si kama hili ni jambo la kuzua.
Mzee wangu, siwezi kukataa au kukubali unayodai kama mimi sijui lolote kuhusu hayo mapambano, kuhusu Mapinduzi.
Kwa kihivyo, siwezi kukuzulia kitu ambacho sikijui.

Mzee nilikuwa nafuata mtiririko wa bandiko zako, dingi na jiwe angavu, na nime comment kutokana na hayo hususani utumiaji wako wa lugha, jinsi unavyoiwasilisha, binafsi niliona imejenga Ukimbari wa Rangi....Wamakonde weusi Wamakonde wanatisha na Wanatoka bara - Okello ni mweusi Okello ni wabara na Lufudhi ya Okello inatisha...=.Watu weusi wanatisha?
Utanisahihisha

Na moja yapo ya utumiaji wa lugha za kimbari, ni kumuunganisha Mwafrika na haya ...mtu mweusi ni katili(savages) mjinga(unintelligent)mtu mweusi sauti yake inatisha, mtu mweusi huwa anapandisha Sauti kwa Lafudhi(ni mfokaji) mtu mweusi ni mtumwa(anakata katani) on and on and on...unaelewa natoka wapi, nimefikia wapi

au nakosea?
 
Wew jamaa unatuona watoto sana[emoji1787][emoji1787]...

Ati anawekewa silaha...

Huyu mzee anatuchukulia humu ni watoto wadogo yani kila anachokisema tukipokee na kukikubali,eti kisa tafiti wakati inajulikana fika tafiti zake zimeelemea upande wa dini ya waarabu.
 
Huyu mzee anatuchukulia humu ni watoto wadogo yani kila anachokisema tukipokee na kukikubali,eti kisa tafiti wakati inajulikana fika tafiti zake zimeelemea upande wa dini ya waarabu.
Jiwe...
Siku zote husema silazimishi mtu kuniamini.

Hapa mimi hueleza kile nikijuacho.

Ikiwa sikijui nasema sijui.

Najua hapa niko na watu wazima.
 
Jiwe...
Siku zote husema silazimishi mtu kuniamini.

Hapa mimi hueleza kile nikijuacho.

Ikiwa sikijui nasema sijui.

Najua hapa niko na watu wazima.
baadhi ya vijana humu ni wa ajabu sana:
- hawasomi vitabu wanategemea maneno ya vijiweni
-ukiandika wao ndiyo wa kwanza kukuita muongo, mdini....
-hawafanyi utafiti wowote lakini wanalazimisha wewe uliyefanya utafiti uingize matokeo ambayo hukuyapata.
 
baadhi ya vijana humu ni wa ajabu sana:
- hawasomi vitabu wanategemea maneno ya vijiweni
-ukiandika wao ndiyo wa kwanza kukuita muongo, mdini....
-hawafanyi utafiti wowote lakini wanalazimisha wewe uliyefanya utafiti uingize matokeo ambayo hukuyapata.
Biti...
Hili ni tatizo kubwa kwa upande wao.

Historia niliyokujanayo kwa wengi ni mpya na iko tofauti sana na historia inayofahamika na kufundishwa shule na vyuoni.

Mtu anapoisikia kwa mara ya kwanza anashtuka na kughadhibika.

Anatamani kama historia hiyo ingekuwa siyo.

Matokeo yake ndiyo huku kukimbilia kutaja udini nk.
 
Mnachihangu,
Ujuba si tusi.

Ujuba maana yake "ukaidi."

Unaweza kuniambia mimi, "Mzee Mohamed unatochosha na ujuba wako."

Hujanitukana.
 
Back
Top Bottom