Tad...
Ikiwa huwezi kusoma basi si tatizo.
Mimi katika maisha yangu nimekuwa sichagui katika kutafuta elimu nasoma kila kitu isipokuwa matusi.
Ndiyo sababu nimekuwa hivi.
Ikiwa utakuwa unasoma vile unavyopenda ndiyo hivyo leo unaamini hadithi ya Okello.
Ungemsoma na Ghassany ungemsoma Abeid Mmasai na wengine hawajatajwa katika historia ya mapinduzi.
Mwisho ungejiuliza mbona Kassim Hanga hatajwi katika historia ya mapinduzi ilhali yeye ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa mapinduzi?
Kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika ungejiuliza mbona Ally Sykes TANU Card No. 2 na kaka yake Abdul Sykes TANU Card No. 3 hawatajwi kwenye historia ya TANU?
Ikutoshe baba yao Kleist Sykes ndiyo aliyeasisi African Association 1929 na ndiye aliyejenga ofisi ya TAA ilipozaliwa TANU 1954.
Vipi historia nzima inamtaja Nyerere peke yake?