Kwa hiyo unasema Biblia haijabadilishwa kabisa?Hakuna sehemu nimesema au nimekwambia Biblia imebadilishwa ,hayo ni ya kwako
Ndio maana nimejikita kwanza kukupa ushahidi wa manuscript zilizopo kabla hata ya Yesu kuzaliwa ,zikiwa zinafanana 99.99% na biblia ya Leo
Nimejibu vizuri ,ni wewe tu unataka kutoka nje ya mada
Twende na jicheleweshe ,ukidhani hayo maswali nitayasahau
Kwanza kama Daniel hakuwepo unavyotaka kukimbilia hicho kichaka
kwa nini maandiko yake yapatikane kwenye tafsiri ya Kigiriki (Septuaginta) inayokamilika sehemu kubwa karne ya 3 K.K.?
Ikiwa Daniel ni hadithi kama unavyodai , je, inafutaje ukweli kwamba mpangilio wa falme ndani ya kitabu unalingana na historia ya dunia bila makosa ? Kasome kitabu cha Daniel uone mpangilio wa falme za Dunia hata nyingine hakuziona kama Roma empire na Roma ya kidini
ikiwa maandiko yalitungwa tu kumfurahisha Alexander, kwa nini yatabiri kuanguka kwa Uyunani na kutokea kwa himaya nyingine (Roma), jambo ambalo lingeweza kumkasirisha?Yaani watunge kumfurahisha ,Tena wamtabirie kuanguka ππ
Nimekuruhusu njoo na staili hiyo, maana itabidi niende kama unavyotaka ,inabidi ubatizwe tuWewe hata husomi, unahamanika.
Hakuna nilipopachika likitabu la Kugel.
Kugel nimeweka jina la kitabu na link yake tu na kusema Biblia inekuwa editwd sana, link hii hapa.
Hiyo twxt ndefu hata si ya Kugel. Inaonesha husomi.
Unanionesha kuwa unajibu kihisia na kwa kuhemuka hufuatilii mada.
Zaidi, hata ningepachika likitabu la Kugel, inawezekana likitabu la Kugel ndilo lina ushahidi.
Sasa kusema sijaweka ushahidi nimeweka likitabu la Kugel, kwani likitabu la Kugel haliwezi kuwa na ushahidi?
Huoni kuwa nii ni non sequitur fallacy?
Huoni kuwa hii ni false dichotomy fallacy?
Kwa mtu unayejinadi kutaka usomi unafanya fallacies nyingi sana.
Umejaa ad hominem fallalcies, umejaa non sequitur fallacies, umejaa false dichotomy fallacies.
Unajicontradict kila pahali.
Unatuletea habari za likitabu la Biblia.
Halafu na sisi tukikujibu kwa likitabu lingine, unakataa, unasema msilete likitabu.
Hivi unaelewa hata wewe mwenyewe unataka nini?
Kitabu cha Daniel kimekosea mpaka historia, mpaka mpangilio wa wafalme, kwa namna ambayo mtu aliyeishi muda huo mnaodai Daniel aliishi, na kukaa kuwaangalia kwa karibu wafalme, na kuandika kitabu, asingeweza kukosea hivyo.Nimekuruhusu njoo na staili hiyo, maana itabidi niende kama unavyotaka ,inabidi ubatizwe tu
Ulichoweka ni jina la kitabu cha James Kugel na link yake nimesoma vizuri sana hoja zako, japo ulipachika tu, bila ustaarabu ili hata ngumbaru aelewe hoja zako ni zipi na nini,
Unasema Biblia imehaririwa mara nyingi.,kupitia huyo Kugel .
Kugel ni msomi, ndiyo, lakini hiyo kauli haijibu swali maalum la muda wa uandishi wa Daniel.,na ndio hoja kuu
Hoja yangu haikiwa biblia kuhaririwa ,bali ilikuwa kwamba hujaleta dondoo za moja kwa moja kutoka humo zinazothibitisha madai yako kuhusu Daniel kama forgery ya baadaye.,nataka ushahidi wa kueleweka
Hoja zangu nilikupa kwa ushahidi,na nilijua tu huwezi kutoboa pale,ndio maana ukakopi maelezo marefu ukapachika ukakimbia ,ila tutaenda hivo hivo unavyotaka ,Mimi nataka mwisho ubatizwe
NARUDIA nakupa ushahidi huuππ
1. Ushahidi wa maandiko β Dead Sea Scrolls zinaonyesha Daniel akiwa na maandiko yaliyokamilika kabla ya karne ya 2 K.K. na bila marekebisho makubwa.,na biblia tuliyo nayo Leo.
2. Ushahidi wa tafsiri β Sehemu za Daniel zipo kwenye Septuaginta (tafsiri ya Kiyunani ya Agano la Kale) karne ya 3 K.K., ikimaanisha maandiko yalikuwepo kabla ya βkarne ya 2 K.K.β unayotaja.
3. Ushahidi wa kihistoria β Josephus (karne ya 1 BK) anamnukuu Daniel na kumhusisha na unabii wa Alexander, akidai hilo lilisomwa kwa Alexander mwenyewe.
NARUDIA Tena maswali haya uyajibuππ
Ikiwa unabii wa Daniel ni baada ya karne ya 2 K.K. kama ulivyodai , unaelezaje uwepo wake katika maandiko ya Septuaginta karne ya 3 K.K.?
Ikiwa maandiko yalihaririwa ili kuonekana kama unabii wa Alexander, kwa nini yahusishe unabii wa kuanguka kwa Uyunani na kupanda kwa himaya nyingine (Roma), jambo ambalo lingeudhi Wagiriki?
Una ushahidi wa moja kwa moja (manuscript au rekodi ya kale) unaothibitisha kwamba maandiko ya Daniel yalibadilishwa baada ya karne ya 2 K.K.?
Falme nyingine nimegusia ,usikimbilie huko kutaka kujifichia hicho kichaka ,Umetaja falme.
Tuongelee falme na wafalme.
Mpangilio wa wafalme katika kitabu cha Daniel umekosewa, post #25 imetaja hilo in great detail. Ukiangalia historia halisi na kitabu cha Daniel, unakuta kitabu cha Daniel kina makosa. Kimewaweka mpaka wafalme wa kujitungia ambao hawakuwapo.
Muandishi anatufungua macho na kutuambia habari hizi zingeweza kuandikwa hivi na mtu ambaye aliandika baadaye, ambaye hakujua falme hizo kama mtu wa wakati huo. Kwamba aliyeandika alikuwa anaandika kama aliishi katika wakati huo, wakati aliandika baadaye sana na kwa kweli hakuujua wakati huo, angeujua, asingwkosea mambo kama hayo.
Yani ni kama mwanahistoria anayesema kaishi miaka yetu halafu ashindwe kujua juwa Rais Nyerere alifuatiwa na Mwibyi, halafu Mwinyi akafuatiwa na Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia.
Mtu anayesema aliishi miaka yetu yote hii halafu akashindwa kutaja orodha ya marais hivi, tutamuwekea shaka kwamba huyu kaishi muda huu kweli au alikuja kuandika baadaye sana mpaka list hii kashindwa kuiweka sawa?
Ila hili umeliruka.
Ama hujalisoma, ama umelisoma na kukataa kuli address kwa sababu linatuonesha kitabu cha Daniel kimeungwaungwa tu na watu baadaye, watu ambao hata hawakujua chronology ya wafalme.
Yote majanga.
JIbu maswali yangu huko nyuma ,tuendelee na mada yetuKitabu cha Daniel kimekosea mpaka historia, mpaka mpangilio wa wafalme, kwa namna ambayo mtu aliyeishi muda huo mnaodai Daniel aliishi, na kukaa kuwaangalia kwa karibu wafalme, na kuandika kitabu, asingeweza kukosea hivyo.
Hili linatuonesha kuwa kitabu hiki kimeandikwa baadaye na mtu ambaye hakuzijua zama hizo vizuri mpaka akakosea mlolongo wa majina ya wafalme ulivyotokea kihalisia kwa kuangalia historia.
Post #25 imeelezea hili in detail kisomi kuliko ninavyoweza kuelezea mimi.
Hujajibu hoja hii.
ukiwa muongo usiwe msahaulifu, wewe mwenyewe kwa hizo copy and paste zako umekuwa kila siku ukikana hakuna maandishi ya kuwa Allah ni Mungu na una associate hilo jina na viumbe vingine. Leo unakiri kuwa maana yake ni mungu na ushawahi kuulizwa bible za kiarabu zinamtajaje Mungu, ukasema hatajwi kwa jina hilo.Umeandika maelezo mengi yasiyo na msingi
Kwanza nikuambie tu neno Mungu kwa kiarabu ni Allah ,hata wakristo wa arabuni ,biblia zao neno Mungu ni Allah ,
Swali ni Mungu yupi?
Ni YWHW
Kwa akili yako unadhani biblia za kiarabu ,neno Allah ni huyu wa hapo mecca anayeabudiwa na wapagani wakikureshi?π
Jitahidi basi utumie akili na elimu, mnafeli wapi aisee
Halafu Mimi sijasoma Quran tu, baba yangu alinipeleka pia kusoma lugha ya kiarabu
Wewe inaonesha ukinikuta nimevaa kanzu yangu na bagalashia ,utasema Mimi ni sheikh ,
Badili mtazamo
Hujajibu hoja yangu kwamba kitabu cha Daniel kina makosa katika kutaja mlolongo wa wafalme, kwa namna ambayo mtu aliyeishi muda huo mnaosema Daniel aliishi, akawafuatilia Wafalme kwa karibu, akaandika vitabu, hawezi kufanya.Falme nyingine nimegusia ,usikimbilie huko kutaka kujifichia hicho kichaka ,
Tulia kwenye mada moja ,jibu maswali unayoulizwa ,
Mbona unapotea hivo,?
mada ya mpangilio wa falme katika Daniel unayotaka kuizua itakushinda ,kama hiyo unayotaka kunikimbia ,Mimi ni mwanaaikolojia mzuri tu, π
Nakushauri jikite kwenye mada husika na ujibu maswali ninayokuuliza ,maana nilipokwambia ukae kwenye Hoja ukasema nakuogopa,
Hoja yako unayotaka kujifichia humo ni kwamba kuna makosa ya kihistoria na kwamba haya yanaonyesha uandishi wa baadaye.
Kwanza, mpangilio wa falme katika Daniel mara nyingi huchanganya vitu hiviππ
Majina ya kifamilia/kikabila (dynastic titles)
Majina ya heshima (regnal names)
Na wakati mwingine majina ya CODE ZA SIRI kwa mtazamo wa unabii.
Mfano, Wafalme wa Misri wote wa nasaba fulani waliitwa Farao, bila kujali jina halisi.
Vivyo hivyo, katika ulimwengu wa Wababeli na Wamedi, majina kama Dario na Koreshi yalitumika kama vyeo, si lazima jina la kuzaliwa.
Pili, hoja ya kwamba Dario Mmedi hakuwahi kuwepo ni hoja ya karne ya 19 ambayo ilikosa ushahidi wa akiolojia uliokuja baadaye.ππ,Unajua hili ???
Ugunduzi wa maandiko ya kale (Cyrus Cylinder na Nabonidus Chronicles) unaonyesha uwepo wa gavana/mtawala wa Kimea aliyeitwa Gobryas (Ugbaru) aliyechukua Babeli kwa niaba ya Koreshi.
Watafsiri wengi wa Biblia na wanahistoria wanakubaliana kwamba huyu ndiye Dario Mmedi jina la heshima, si jina la kuzaliwa.
Tatu, madai kwamba mwandishi alijipangia falme kwa ujuzi mdogo yanapuuza ukweli kwamba Daniel anaonyesha maarifa ya undani ya
Mila za kifalme za Babeli
Mfumo wa washauri (magoi)
Sheria isiyobadilika ya Wamedi na Waajemi (Danieli 6:8), jambo lililothibitishwa kihistoria
Lugha na vyombo vya kifalme vya Kaldia na Umedi
Kwa maneno mengine, mwandishi alikuwa na maarifa halisi ya enzi hizo jambo lisilowezekana kwa mtu wa karne ya 2 K.K. bila vyanzo vya moja kwa moja vya kale.
Wewe tatizo ni elimu Dunia tu ,huna tatizo kubwaukiwa muongo usiwe msahaulifu, wewe mwenyewe kwa hizo copy and paste zako umekuwa kila siku ukikana hakuna maandishi ya kuwa Allah ni Mungu na una associate hilo jina na viumbe vingine. Leo unakiri kuwa maana yake ni mungu na ushawahi kuulizwa bible za kiarabu zinamtajaje Mungu, ukasema hatajwi kwa jina hilo.
Kiarabu ni lugha nami naifahamu si kwa kuisoma bali kwa kuiishi, nimejifunzia mitaani huko ilipotokea na ni moja ya lugha tano za kimataifa nayozungumza kwa ufasaha kabisa. Kuna watu wa aina yako wana chuki mpaka wanashindwa kuelewa kuwa maeneo ya Palestina, Syria,Lebanon, Jordan na Egypt kuna non muslim na wanasali kanisani kwa kiarabu
BTW wewe jibu hoja unazoulizwa huko kwanini wewe unaona sawa kukopi vitabu na maandiko ya wengine ila wakileta wengine unaona ni kosa as if kuna cha kwako ulichoandika na kwanini unapenda kufanya ad hominem, kushambulia mtu badala ya hoja au kugeuza na kupotosha hoja ya mtu ili ishambuliwe kama siyo hiyo narcissistic personality disorder (NPD)? ambazo dalili zote unazionesha.
Badili mtazamo
Nimekujibu ,halafu ni kama umetafuta tawiππHujajibu hoja yangu kwamba kitabu cha Daniel kina makosa katika kutaja mlolongo wa wafalme, kwa namna ambayo mtu aliyeishi muda huo mnaosema Daniel aliishi, akawafuatilia Wafalme kwa karibu, akaandika vitabu, hawezi kufanya.
Yani kitabu cha Mungu kinabumbabumba vipi majina tu kiasi cha kuacha utata hivi? Mungu alishindwaje kunyoosha hata majina tu tuangalie tusione utata tujue Daniel ni nabii wa Mungu kweli?
Yani ni kama atokee muandishi baadaye aseme aliishi zama zetu hizi za leo na kusema Nyerere alianza kuwa rais, akafuatiwa na Kikwete, halafu akaja Samia, halafu akaja Mkapa, na Mkapa akafuatiwa na mtoto wa Mkapa, kisha akaja Msubi, halafu akaja Magufuli.
Tukiona muandishi kaandika hivyo tutawekea maswali mengi maandiko yake yote na kujua kuwa muandishi huyu kaungaunga habari tu hakuishi zama hizi na kajitungia tu habari kuhusu zama ambazo hakuzijua.
Unarudi mule mule ,halafu maswali hujibu ,hoja mpya uliyoibua huwezi kujitetea Tena ,maana nikisema ukae kwenye mstari ,wanasema nakuogopa ,sasa nimeamua kwenda na wewe hivo hivo unavyotakaWasomi wa Bibkia wanasema Daniel kikiandikwa 2nd Century BCE. Baada ya Alexander kufariki. Si 6th Century BCE kama inavyodaiwa.
Sasa, kitabu kilichoandikwa au kuhaririwa baada ya matokeo kinachosema kimeyatabiri kutokea, kitakuwaje kimeyatabiri matokeo hayo?
Mfano leo mimi niandike kitabu cha kutabiri matokeo ya miaka ya 1900.
Nitabiri vita vikuu vya kwanza vya dunia, nitabiri mapinduzi ya Urusi, nitabiri anguko la masoko ya dunia, nitabiri vita vya pili vya dunia, nitabiri anguko la ukoloni, nitabiri internet, nitabiri muungano wa Tanganyika na Zanzibar, nitabiri marais wa Tanzania, nitabiri yoote yaliyotokea miaka ya 1900.
Utanisifia kwamba mimi ni mtabiri mzuri sana, mambo yote niliyotabiri yametokea kama nilivyotabiri?
Tatizo hujasoma post #25 na kuijibu point by point.Nimekujibu ,halafu ni kama umetafuta tawiππ
Huko nyuma umejibu maswali niliyokuuliza ?
Au unataka niyarudie Tena ?kama umeyashindwa sema
Naona umejitengenezea ka mada kako ka pembeni ,ukiona ni karahisi ,sasa nikwambie hiki kichaka nacho nakipiga moto ,nione utakimbilia wapi, Wakati unadhani nitasahau ,hata huku pia nachoma hichi kichaka ,
hoja yako kwamba kitabu cha Daniel kina makosa ya mlolongo wa falme kisa unafananisha na mtindo wa leo wa marais, jambo ambalo ni kinyume na uhalisia wa kihistoria,kwanza unatoa aibu kwa watu wanaokujua humu, Majina kama Dario ,Herode,farao ,hivo vilikuwa vyeo ,wewe unafananisha na magufuli, mkapa πππππππ..
Katika ulimwengu wa kale, majina kama Dario au Koreshi hayakumaanisha mtu mmoja tu bali yalikuwa majina ya heshima (regnal titles) yaliyotumika na watawala wengi, mfano halisi ukiwa Misri ambapo kila mfalme aliitwa Farao bila kujali jina lake binafsi, au Roma ambapo kila mfalme aliitwa Caesar hata baada ya Julius Caesar kufa.
Sikutegemea kumbe wewe ni Mweupe kiasi hiki ππ
Hivyo Daniel anapomtaja Dario Mmedi si jina bali ni gavana halisi aliyeteuliwa na Mfalme Koreshi baada ya kuiteka Babeli, anayejulikana katika rekodi za akiolojia kama Gobryas (Ugbaru), na kwa tamaduni za Kiyahudi alihesabiwa kama mfalme.
Ukitaka naweka ushahidi wa AKIOLOJIA,Sina wasiwasi
Kitu unachokikwepa ni kwamba maandiko ya kale kama Cyrus Cylinder na Nabonidus Chronicle yaliyopo makumbusho ya Uingereza na Paris yanaunga mkono mfumo wa utawala na mabadiliko ya falme kama ulivyoandikwa katika Daniel, na haya yalikuwepo mamia ya miaka kabla ya karne ya 2 K.K.
Unapodai eti maandiko haya yaliandikwa baadaye, unatakiwa utoe maelezo ni kwa nini waandishi hao wa karne ya 2 K.K. wangeacha makosa ya kihistoria yaliyoweza kurekebishwa kwa urahisi ili kuonekana wakamilifu, badala ya kuyaacha kama yalivyo na kujitengenezea hatari ya kufichuliwa.,Jitahidi kutumia ubongo ,mbona hoja Nyepesi sana hizi π
Kwa lugha rahisi, hoja yako inalazimisha tukubaliane kwamba walighushi lakini wakaghushi vibaya kwa makusudi jambo lisilo na mantiki.
Zaidi ya hapo, unadai Daniel ni hadithi, lakini unabii wake unagusa mambo madogo kabisa ya kiutawala kama βsheria isiyobadilika ya Wamedi na Waajemiβ kasome (Daniel 6:8), jambo ambalo limehakikishwa na historia na halikujulikana kwa vizazi vya baadaye vilivyodaiwa kuandika upya.
Unawezaje kueleza usahihi wa mambo kama haya ya ndani ya mfumo wa kisheria wa karne ya 6 K.K. kama si matokeo ya mtu aliyeishi na kuyaona?
Pia, kama unakataa ushahidi huu, uko tayari kuonyesha maandiko ya kale yanayopingana na Daniel na kutupa tarehe yake ya uhakika kabla ya kujificha nyuma ya kauli za jumla kuhusu βeditingβ za baadaye?ππ
Kwa sasa, hoja yako imejikita kwenye kulinganisha historia ya kifalme ya kale na siasa za kisasa za marais, jambo ambalo kiuhalisia ni kulazimisha mlinganisho usio na msingi.
Nakupa elimu Kihistoria, mfumo wa utawala wa nyakati za Daniel na namna majina yalivyotumika unaufanya mpangilio wake wa falme uwe sahihi kulingana na enzi hizo, na ushahidi wa akiolojia unaunga mkono maelezo yake badala ya kuyabatilisha.
NDIO NACHOMA MOTO HIVO HIKI KICHAKA
Nimesoma na hoja zako nimezijibu ,na nimekuuliza maswali kama kweli ni forgery ,hujajibu hata swali mojaTatizo hujasoma post #25 na kuijibu point by point.
Daniel imekosea mpaka namba ya mikoa ya falme kwa namna ambayo mtu aliyeishi muda huo hawezi kukosea hivyo.
Yani kama leo mtu aseme ameishi leo Tanzania halafu akosee namba ya mikoa nchi ina mikoa 30 aseme ina mikoa 120.
Hatusemi Daniel ni forgery kwa sababu moja, kuna sababu nyingi sana kika ukisoma unaona huu ni uongo umeungwaungwa tu.
Tatizo hutaki kuijibu post #25 point by point.
Kwa sababu huwezi.
Nimesoma na hoja zako nimezijibu ,na nimekuuliza maswali kama kweli ni forgery ,hujajibu hata swali mojaTatizo hujasoma post #25 na kuijibu point by point.
Daniel imekosea mpaka namba ya mikoa ya falme kwa namna ambayo mtu aliyeishi muda huo hawezi kukosea hivyo.
Yani kama leo mtu aseme ameishi leo Tanzania halafu akosee namba ya mikoa nchi ina mikoa 30 aseme ina mikoa 120.
Hatusemi Daniel ni forgery kwa sababu moja, kuna sababu nyingi sana kika ukisoma unaona huu ni uongo umeungwaungwa tu.
Tatizo hutaki kuijibu post #25 point by point.
Kwa sababu huwezi.