Alexander mkuu alivyotabiriwa na Biblia kwa usahihi

Hakuna la kheri katika kukimbia kujibu hoja.

Kuacha hoja hazijajibiwa katika mjadala uliouanzisha mwenyewe si jambo la kheri.
Ulijua nakukimbia ,twende kazi, kakuponza huyo adriz
 
Assnte
Uchambuzi mzuri kanisa. Ubarikiwe
 
Ukishaanza habari ya "Daniel imeandika unabii wa code za siri" hata Sheikh Yahya na Nostradamus nao watasema wameandika unabii wa code za siri.

Sasa kitakachomtofautisha Daniel kuwa nabii wa Mungu hapo ni nini?

Pia, unathibitishaje kuwa huu ni utabiri ulioandikwa kabla ya Alexander kuishi na si uhariri uliofanyika baada ya Alexander kuishi ikiwa wasomi wengi wanakubaliana kuwa kitabu cha Daniel kimeandikwa na kuhaririwa mpaka 2 centuries BCE, muda ambao Alexander alishaishi na kufariki tayari?

Hujajibu swali hili.
 
Ulijua nakukimbia ,twende kazi, kakuponza huyo adriz
Tatizo lako unatoka kwrnye kujadili mada kihoja, unanijadili mimi kwa viroja.

This is ad hominem attack.

Jadili mada, usinijadili mimi.

Jibu post #25, point kwa point.

Anza kwa kuthibitisha kuwa Daniel alikuwapo kweli na si muhusika wa hadithi ya kutungwa na watu tu au muhusika wa kuungaunga mambo ya watu tofauti na kuongeza chumvi ambazo hazikutokea.

Kabla ya kufika kwenye utabiri wa Daniel, huyo Daniel mwenyewe alikuwapo? Aliishi? Aliishi lini? Kuna ushahidi gani wa kihistoria kwamba aliishi?

Kama hujaweza kuthibitisha Daniel alikuwapo, aliishi, aliishi nuda huo mnaosema aliishi, kwa ushahidi wa kihistoria, unaooneshwa na vyanzo tofauti nje ya Biblia, unakuwa hujaweza hata kuthibitisha huyo Daniel aliishi, hivyo hujafika sehemu ya kusema utabiri wa Daniel ulikuwa sahihi.

Kama Daniel hakuwapo, hakuishi, ni muhusika wa hadithi ya kutungwa tu, itawezekanaje awe ametabiri utabiri uliokuja kutokea na kuwa sahihi?
 
Hakuna sehemu nimekujadili wewe,nimejikita kwenye hoja zangu, na nimekuuliza maswali

Cha ajabu unarudia pale pale ,ni wazi husomi majibu na maswali ninayokuuliza

Ungejibu maswali niliyokuuliza hili swali usingeuliza tena
 
Hakuna sehemu nimekujadili wewe,nimejikita kwenye hoja zangu, na nimekuuliza maswali

Cha ajabu unarudia pale pale ,ni wazi husomi majibu na maswali ninayokuuliza

Ungejibu maswali niliyokuuliza hili swali usingeuliza tena
Ukishaanza kunitaka niweke maneno niliyoandika mimi, nisiweke maandiko ya watu, hapo umetoka kwenye hoja na umenijadili mimi binafsi na uwezo wangu.

Hili jambo umelifanya sana hapo juu.

Inaonekana hujali hoja, unajali zaidi kumjadili mtoa hoja na kukataa maneno kwa kutumia flimsy fallacies.

This is an ad hominem fallacy.

Unamshambulia mtu badala ya kujadili hoja in the abstract bila kujali hoja imetoka kwa nani.

Unasema unapenda usomi halafu hujui kitu simple kama ad hominem fallacy?

Unaelewa ad hominem fallacy ni nini?
 
Unajua kwanini nakubana sana uwe unajibu maswali ninayokuuliza ?

Ni sababu usikimbie na kutafuta kichaka ,hili swali lako nilikujibu na kukuuliza maswali hukujibu hata moja


Niligusia 👇👇👇


hoja yako kwamba Danieli huenda iliandikwa baada ya Alexander inapingwa na ushahidi huu:

Dead Sea Scrolls, Nakala za Danieli zimepatikana huko Qumran, zikiwa zimehifadhiwa kutoka karne ya 2 K.K., na zinafanana kimsingi na maandiko tunayoyasoma leo. Hii inathibitisha kuwa Danieli alikuwa maandiko yanayojulikana muda mrefu kabla ya Baraza la Nisea (325 B.K.).

Septuaginta (LXX): Tafsiri ya Kiyunani ya Agano la Kale ilianza kutafsiriwa huko Alexandria karibu na 250 K.K., ikiwa ni pamoja na Danieli. Hii ni kabla sana ya Yesu na miaka mingi baada ya Alexander kufa, ikithibitisha kwamba maandiko hayo yalikuwepo tayari.

Mapokeo ya Kiyahudi: Wayahudi wa karne nyingi kabla ya Ukristo walihesabu Danieli kama sehemu ya maandiko matakatifu (Ketuvim), hivyo haikuwa njama ya Kikristo wala ya Warumi.


Zaidi ya hayo, hoja kwamba Wayahudi walitumia "utabiri vague" kumfurahisha Alexander haina mashiko:

Unabii wa Danieli 8 sio vague, unamtaja "mfalme wa Uyunani" akishinda "Umedi na Uajemi", pembe kubwa ikivunjika na badala yake zikainuka pembe nne. Haya ni maelezo ya moja kwa moja yanayolingana na historia ya Alexander na mgawanyo wa ufalme wake.

Ikiwa ilikuwa njama ya kumfurahisha, kwa nini Wayahudi waendelee kuamini unabii huo karne nyingi baadaye, hata pale unapomtabiri pia Mpinga Kristo na matukio mengine yasiyompendeza mtu yeyote?

Kabla hujaanza kurukaruka nijibu maswali haya ili kuonesha Kuna forgery

1. Ikiwa unabii wa Danieli uliandikwa baada ya Alexander kufa, kwa nini kuna nakala za Danieli (Qumran) zilizopo karne ya 2 K.K. ambazo ni karibu kabisa na matukio hayo, na kwa nini hakuna nakala inayonyesha "toleo la awali" bila unabii huo?


2. Kwa nini Septuaginta (iliyotafsiriwa karne ya 3 K.K.) inajumuisha Danieli ikiwa haikuwepo hadi baada ya Alexander, ilhali tafsiri hiyo ilianza miongo michache tu baada ya Alexander kufa?


3. Ikiwa ilikuwa ni njama ya Wayahudi, kwa nini unabii huo uliendelea kuwa na maelezo ambayo hayana faida ya kisiasa kwao (kama maangamizi ya baadaye ya Yerusalemu na dhuluma za Wagiriki chini ya Antioko Epifane), badala ya kumtukuza Alexander tu?



Kwa hivyo, ushahidi wa kihistoria na wa kiakiolojia unaonyesha wazi kwamba Danieli alikuwa maandiko yaliyokuwepo kabla ya Alexander na hayakuwa njama ya baadaye.
 
Sikukutaka uweke maneno yako, nilikutaka uwe na mpangilio wa hoja

Na sijakujadili wewe ,Bali nimeshangazwa na uwezo wako mdogo wa kujadili mambo tofaut na wengi wanavyokudhania, sikutegemea ushindwe vitu vidogo vidogo ,

Sikutegemea ukimbie maswali ya msingi ambayo kiukweli lazima yakubane hoja

Sio unapachika tu maelezo au kitabu chote ,Tena kwa english ili Hali hapa tunafanya majadala wa kiswahili

Ile ilikuwa mbinu yako yakukimbia mjadala , Defensive mechanism
 
Nilikuuliza 200 BCE Alexander alikuwa hai au kashafariki?

Sijaona ulipojibu swali hili.

Yani leo noje nitabiri mambo yaliyotokea mwaka 1900, nipatie vilevike.

Utanishangikia na kusema nimetabiri vizuri sana, matukio yaliyotokea miaka 125 iliyopita nimeyatabiri keo na kuyapatia vilevile?

Huo ni utabiri au historia?

Kuandika historia ni kutabiri?
 
Haya, mimi kwa kujua labda kweli sina uwezo mkubwa kwenye mada hii, nimekuwekea bandiko la maneno ya mtu mwenye uwezo mkubwa kwenye mada hii aielezee point yangu kisomi zaidi. Maana mimi si msomi wa Biblia.

Jamaa kasema yeye anaandika kwa kutumia peer reviewed sources tu, hataki longolongo.

Post #25.

Ulijibu point by point.

Umelikimbia. Hujalijibu.

Unalalamika nimeweka maneno ya watu.

Nikiweka maneno yangu unanilalamikia sina uwezo, sina usomi.

Nikiweka bandiko la msomi kusisitiza point yangu, bila mimi kutia neno unalalamika sijaandika maneno yangu.

Hivi hata wewe mwenyewe unaelewa unataka nini?
 
Shida wewe husomi ,na unakwepa kujibu, ungekuwa unajibu ninachokuuliza wala tusingefika huku

Ulianza kusema Wayahudi ndio walipanga huu unabii ,ukarukia ohoo ni Baraza la NICEA ,kote huko nilipangua hoja zako na kukuuliza maswal muhimu sana ambayo uliyakimbia ,kwa unavyojitanabaisha humu , sikutegemea ufanye michezo hii ambayo nimeizoea kwenye Mijadala na waislamu.

Nilisema Historia na akiolojia tayari zina mashahidi thabiti kwamba Danieli book kiliwepo kabla ya enzi za Maccabees na karne nyingi kabla ya Kanisa la Roma kuundwa.

1. Ushahidi wa Dead Sea Scrolls (Qumran)
Nakala za kitabu cha Danieli zimepatikana kwenye mapango ya Qumran, zikihesabiwa kati ya karne ya 2 K.K. na 1 K.K.

Kimsingi, nakala hizi zinafanana na maandiko tunayoyasoma leo. Ikiwa kulikuwa na “editing kubwa” baada ya matukio, tungeona tofauti kubwa kati ya nakala hizi na Biblia ya leo lakini hatuoni.

Je, unaweza kueleza vipi jinsi forgery ya baadaye ilivyoweza kuwa tayari imesambaa kote kabla ya Qumran bila kuacha toleo la awali popote?


2. Septuaginta (LXX)

Tafsiri ya Kiyunani ya Agano la Kale (Septuaginta) ilianza kutafsiriwa Alexandria, Misri, takribani mwaka 250 K.K., ikiwa ni pamoja na Danieli.

Hii ni miongo michache tu baada ya Alexander kufa, na kabla ya Maccabees, ikithibitisha kuwa kitabu cha Danieli tayari kilikuwepo.

Ikiwa kitabu hiki kilifanywa baadaye sana, je, kwa nini kikajumuishwe kwenye tafsiri hii ya mapema?


3. Mjadala wa Daniel kama mtu wa historia

Zaidi ya hayo, Ezekieli 14:14 na 28:3 (iliyokuwa imeandikwa karne nyingi kabla ya Maccabees) inamtaja Daniel kama mtu mashuhuri, jambo linaloonyesha kuwa jina hili na hadithi zake zilijulikana mapema.

4. Hoja kuhusu “lugha na vyombo vya muziki”

Ni kweli Danieli ina maneno ya Kiajemi na Kiyunani. Lakini hii haimaanishi kuwa iliandikwa baadaye; inadhihirisha tu muktadha wa historia ya Babeli na Uajemi, ambapo lugha hizo zilitumika katika utawala na muziki.


Hata Wababeli walitumia maneno ya Kiyunani katika muziki karne kabla ya Maccabees kwa sababu ya mawasiliano ya biashara na Ugiriki.


Ikiwa ilikuwa ni forgery iliyotungwa na Wayahudi, je, kwa nini iongeze unabii kuhusu maangamizi ya baadaye ya Yerusalemu na dhuluma za Antioko Epifane mambo ambayo hayangefaidisha kabisa kisiasa?


Je, unaweza kueleza mantiki ya kutengeneza maandiko ambayo yanawapa Wayahudi picha ya kuangamizwa na kudhulumiwa, badala ya ushindi pekee?
 
Sikulalamika ,nilikuomba tu kama msomi unayejitanabaisha humu jamvini,

Weka hoja zako hata kama za mtu kwa mpangilio wa kueleweka,hata ngumbaru aelewe ,sio kukopi kitabu na kupachika ,bila maelezo ya hoja ipi unajibu ,mjadala wa kiswahili unapachika kitabu cha English ,sura nzima ,

Ndio mlivyofundishwa huko mashuleni ?
 
Anza Alif kwa ujiti.

Jibu post#25 point by point.

Anza na point ya kwanza kabisa.

Thibitisha Daniel alikuwapo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu, au za kuungwaungwa na watu tu baadaye na kujazia tabiri kwa kutumia historia iliyokwishatokea.

Thibitisha kwa vyanzo vya kihistoria vinavyoweza kupasi mitihani ya historicity, kui validate Biblia si Biblia kama chanzo.

Anzia hapo.
 
Anza Alif kwa ujiti.

Jibu post#25 point by point.

Anza na point ya kwanza kabisa.

Thibitisha Daniel alikuwapo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu, au za kuungwaungwa na watu tu baadaye na kujazia tabiri kwa kutumia historia iliyokwishatokea.

Thibitisha kwa vyanzo vya kihistoria vinavyoweza kupasi mitihani ya historicity, kui validate Biblia si Biblia kama chanzo.

Anzia hapo.
 
Rudi usome hoja ninazojibu na kuuliza maswali ,mbona unapiga MARKTIME Mzee😂
 
Rudi usome hoja ninazojibu na kuuliza maswali ,mbona unapiga MARKTIME Mzee😂
Wapi umejibu post #25 point by point?

Niwekee post number hapa niipitie tena labda sinaiona.

Wapi umethibitisha Daniel alikuwa anaishi kweli na si muhusika wa hadithi ya kutungwa na watu tu?
 
Unarukia mbele ,ni kwamba maswali yamekushinda ?

Usipojibu maswali yangu, unafanya hoja zako zikose nguvu, unaponibu hoja zangu na maswali ndio kwanza unapata na majibu ya maswali unayouliza kila mara na ninayajibu na kukuuliza maswali

Sasa unafanya ionekane unapiga MARKTIME
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…