Mbona nishakujibu.
1."Utabiri" kuandikwa na mtu aliyeishi miaka mingi baadaye cha ajabu ni kipi?
Mfano leo nikiandika habari kama mtu aliyeishi mwaka 1800 anatabiri maisha yote ya Nyerere, hapo ugumu uko wapi kupatia maisha yote ya Nyerere?
2. Kitabu cha Daniel kinekosea mambo mengi ya kihistoria. Yametajw akwenye post #25. Hujqyajibu point by point. Kwa hivyo swali lako kwanza halijajengwa katika nsingi wa ukweli.
Lakini hata matukio yaliyopatiwa, kama yamekuwa editwd baada ya natukio kutokea cha ajabu ni kioi hapo?
Dead Sea Scrolls zinathibitishaje uwepi wa Daniel? Kwa mfano kama Dead Sea scrolls zimekopi tu firgery ikiyot9kea awali ya kuweka hadithi za Daniel kuwapo, wakati hakuwahi kuwapo, hapo zinathibitusha vipi Daniel alikuwapo?
3. Historia inapinga uwepo wa Daniel. Kwanza hakuna ushahidi wowote nje ya Biblia unaoonwsha Daniel alikuwapo.Post #25 imeandika hoja hii in detail.
Tatizo unajibu bila kusoma.
Rudi kwenye post # 25 halafu ijibu point by point.
Nasoma vizuri sana ,na najitahidi kupitia kwenye hoja zako, maswali hujibu sababu unapalaza tu kiwepes ,
Nitarudia Tena uone kuwa upo shallow ,na kwa majibu haya inakubidi ukasome Tena
Swali lako la kwanza unasema
“
Kama Daniel hakuwapo, na mtu aliandika baadaye akijifanya yeye, cha ajabu ni nini kama akipatia matukio yaliyokuwa tayari yametokea?”
kwanza unatakiwa ujue kitabu cha Danieli hakisimamii tu historia ya Babeli, Medo-Persia na Ugiriki.,kama unavyodhani , Kinaendelea kuonyesha mambo yaliyotokea baada ya karne ya kwanza K.K., kama vile kuanguka kwa Yerusalemu mwaka 70 B.K., pamoja na mambo ya mwisho kama ufufuo, hukumu na Ufalme wa Mungu (Danieli 12:1–3).
Hii ni tofauti kubwa na maandiko ya uongo ya Kiyahudi (pseudepigrapha), ambayo mara nyingi yalijikita tu katika historia ya nyuma.
Mfano wako wa mtu kuandika mwaka 1800 akitabiri maisha ya Nyerere unaweza kueleza mambo yaliyopita, lakini hauwezi kueleza kwa usahihi matukio ya karne nyingi baadaye hadi sasa na yajayo., Hivo hoja yako ni mfu ,ndio maana nakushangaa unakwama wapi ...
Kuhusu makosa ya Kihistoria unayosema moja ni “Dario Mmedi” ambaye hajulikani vizuri katika vyanzo vya nje, au mfuatano wa wafalme wa Babeli na Medo-Persia.
Cha ajabu na kilichokuja kuwaumbua hao unawaotegenea , archaeology baadaye.,imekuja kuthibitisha Kwa 100%,
Kwa mfano, kwa karne nyingi Belshaza hakujulikana kabisa katika historia, lakini maandiko ya cuneiform yaliyogunduliwa karne ya 19 yalibainisha kuwa kweli alikuwa regent, mwana wa Nabonidus jambo linalolingana kabisa na Danieli 5.
KWAHIYO HOJA YAKO IMEKUFA KIFO CHA MENDE,
Pili, kuhusu “Dario Mmedi,” tafsiri bado inajadiliwa, na tafsiri moja ni kwamba jina hilo linamrejelea Gubaru, mtawala aliyeteuliwa na Koreshi baada ya kuanguka kwa Babeli.
Dead Sea Scrolls pia ni muhimu kwa sababu zinaonyesha kuwa ifikapo karne ya pili K.K., kitabu cha Danieli tayari kiliheshimiwa kama kitabu cha kinabii na kilishasambazwa.
Hii ina maana kwamba hakiwezi kuwa kilitungwa baada ya wakati huo, wala kusiwepo na nafasi ya “kuhariri” unabii wa kuanguka kwa Yerusalemu mwaka 70 A.D., kwani maandiko yalikuwa tayari yameshaandikwa ,hii nayo inakufa kibudu.
Kuhusu hoja ya kutokuwepo kwa ushahidi wa kihistoria wa mtu binafsi aitwaye Danieli, ni hoja Nyepesi sana ,baada ya kushindwa kujibu hoja hapo juu
Vyanzo vilivyopona kutoka Babeli ni vichache sana na havikutaja kila mtu aliyehudumu ikulu.
Kuna watu wengi waliokuwa na nafasi kubwa lakini hawajulikani leo.
Hivyo kutokupatikana kwa jina la Danieli hakuthibitishi moja kwa moja kwamba hakuwapo.
Ikiwa Danieli hakuwapo na kitabu kiliandikwa baadaye, unabii wa kuanguka kwa Yerusalemu mwaka 70 B.K. uliandikwa vipi kabla ya tukio hilo?
Kwa nini kitabu cha Danieli kilipewa hadhi ya kinabii na Wayahudi wa Qumran ikiwa kilikuwa “hadithi iliyotungwa tu”?
Unawezaje kueleza ukweli kwamba Belshaza, aliyesemekana kuwa “kosa la kihistoria,” alithibitishwa na archaeology karne nyingi baadaye, sawa kabisa na simulizi la Danieli?
Je, kutokuwepo kwa kumbukumbu za moja kwa moja za Danieli ni ushahidi thabiti wa kutoishi kwake, ilhali rekodi za kale ni chache na hazikuhifadhi majina ya maelfu ya watumishi wa kifalme?