Uislamu hauna makosa hata kidogo.
Ila sisi binadamu ndo tuna makosa.
Linapotokea tatizo kuhusu Waislamu basi walaumu Waislamu na usiulaumu Uislamu.
Nani katika hii dunia hajawahi kukosea?
Kwani ukristo unaruhusu kuimba?
Na mbona wakristo wanaimba mpaka makanisani?
{ Wakristo tumeruhusiwa kuimba na toka zama za Manabii Nyimbo ziliimbwa.}
Hesabu 21:17
Ndipo Israeli wakaimba wimbo huu; Bubujika Ee kisima; kiimbieni;
1 Mambo ya Nyakati 15:16 Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha.
(Maana ya Zaburi ni Nyimbo.)
Zaburi 98:5
Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
Mathayo 26:30 Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.
Marko 14:26 Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni.
1 Wakorintho 14:15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.
Ufunuo wa Yohana 5:9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Ufunuo wa Yohana 14:3 na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi.
Ufunuo wa Yohana 15:3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
[ Kwa Mwislamu anayedhubutu kuimba anamkufuru Mungu wake. kwakuwa hakuna mahali waliporuhusiwa kuimba.]