Ali Kiba Fans' Special Thread...

Ali Kiba Fans' Special Thread...

hapana sio mwanamitindo ni mwanamuziki ila pia ana kipaji cha mpira wa miguu.mbeya city wanatafuta mshambuliaji km vp angepima upepo hko maana mziki inaonekana km umemkataa ila kuna watu wanamjaza ujinga anaendelea kusugua.ana watoto watatu wote wanaishi kwa bibi yeye yupo dusco inavyoonekana miaka ya badae vile vifaranga vitakuja kurithi blackberry

i see!! Wivu sina ila roho inauma.
 

Attachments

  • 1417434052076.jpg
    1417434052076.jpg
    8.3 KB · Views: 99
Dah! Jamaa utakuwa unanikubali sana, yaani kwa kuandika hivyo tu umeona nimetumia akili nyingi sana. Asante kwa kunikubali, lakini ukweli wala sikutumia akili nyingi, kwani wakati naandika hiyo ndo nilikuwa nimetoka kulala.
Kwa huku niliko niliiandika saa 8 usiku, after kupokea Simu ya familia na kuzungumza nayo. Huwa natumia akili nyingi kwa kazi zilizonileta huku, kwangu muziki ni burudani tu kama ilivyo soka.
Ukweli upi uliopindishwa? Kwamba maelezo yangu yamesema Nassib hakupata tuzo? Si kweli kwamba studio kuu ya Channel O iko SA? Si kweli kwamba studio kuu ya MTV Base iko Nigeria? Si kweli kwamba CHOAMVA ni Tuzo za kituo cha TV?
Kwa taarifa yako Tuzo zina sarakasi nyingi sana, unajua kama Kanye West aliwahi kupanda ghafla jukwaani na kuponda Beyonce kunyimwa Tuzo aliyokuwa akiwania na Taylor Swift? Yote hiyo ni kwa sababu ya sarakasi za Tuzo. Matola kakueleza kwamba Westside Connection walikuwa wakali watupu na walitoa nyimbo kali tupu na hawakuwahi kupata tuzo?
Ova

Naomba unitajie tuzo yoyote duniani isiyolalamikiwa? Yoyote......


Unapindisha mantiki kwa kutumia mifano mfu
Ni sawa na useme Davido hastahili matuzo aliyopata kuanzia mwka jana hadi huu kwa kutumia mifano ya westside conn
 
Last edited by a moderator:
Mi mwenyewe nimeshangaa eti!
Ila Diva Beyonce alishashtukiaga akawaambia wawe wanakuja na IDs zao za siku zote! Duh kweli Kiba nomaa!

Umeona eeh?tokea huu uzi uanze nimeona ID's mpya ambazo sikuwahi kuziona kabla....ni hatari
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh?tokea huu uzi uanze nimeona ID's mpya ambazo sikuwahi kuziona kabla....ni hatari

Hatari kwakweli maana watu wanapoteza energy yao bure!
Jamani mwenye picha za Kiba atupiemo basi watu tuendelee kusuuzika!
 
Kiba u r the best...marekebisho muhimu kama tulivokushauri maana kurudia rudia sio issue....much respect!Jaman picha za King plz...
 

Attachments

  • 1417440371189.jpg
    1417440371189.jpg
    7.5 KB · Views: 113
  • 1417440407367.jpg
    1417440407367.jpg
    6.6 KB · Views: 109
Last edited by a moderator:
Naomba unitajie tuzo yoyote duniani isiyolalamikiwa? Yoyote......


Unapindisha mantiki kwa kutumia mifano mfu
Ni sawa na useme Davido hastahili matuzo aliyopata kuanzia mwka jana hadi huu kwa kutumia mifano ya westside conn

Afadhali umekubaliana na karibu kila tuzo hulalamikiwa. Sasa sababu ya kulalamikiwa ndizo hizo sarakasi zilizomo kwenye hizo tuzo. Na ndicho nilichokisema, kwa maana ya kwamba Adele aliweka rekodi ya tuzo nyingi, lakini Nicki Minaj akauza sana album. Kama Davido kupata tuzo nyingi, lakini 2 Face Idibia akauza nakala nyingi za album.
Nijuavyo, maana ya mifano mfu ni ile ambayo haipo, lakini mimi nimekuwa mifano ya historia ya maisha ya muziki, kwani kiazi chetu tunajifunza kufuatana na historia kwa maana ya kumbukumbu, ndio maana leo tuna vitabu vitakatifu ambavyo vina miongozo ya matukio na maisha ya zamani.
Sasa kama mfano wa historia ya yaliyopita kwenye maisha ya muziki unaita mfu, unahitaji nini zaidi? Sijui kama unajua kama vitabu vinavyouzwa sana ukiondoa vya novel, ni vile vya kumbukumbu za watawala na watu mashuhuri waliopita kwa ajili ya watu kutaka kujifunza kupitia kwao.
Mifano niliyotoa ina maana kwamba unaweza ukawa mkali lakini bado usipate tuzo. Sikuwahi kutoa mfano wa asiyestahili kupata tuzo, kila anayefanya sanaa anaweza kupata tuzo au akakosa, lakini tuzo ni tofauti na matokeo ya darasani kwa maana ya uwezo halisi.
Katika tuzo ni tofauti, watu mtapiga kura nyingi muwezavyo lakini zinapewa asilimia 10 tu katika ushindi, kisha kuna kundi la watu watajifungia ndani na kuamua kwa muono wao kuwa huyu na huyu ndio washindi, kama unavyojua kila binadamu ana utashi wake.
Ndio maana tunaona Casper Nyovest kapata tuzo nyingi kwa wimbo wake wa Doc Shebeleza, lakini katika kufuata hisia za wapenzi wa muziki, huo wimbo wa Doc Shebeleza umeweza kuupoteza Y Tjukutja wa Uhuru alioimba na akina Professor, Oskido na Dj Bucks? Umeupoteza Khona wa Mafikizolo?
Ova
 
Ali kiba anajua sana kuimba kuliko wanamuziki wengi sana tz akiwemo diamond
Lakini ali kiba hajui "kufanya" muziki

Ukiwa umesoma au kupitia comments za humu, hili jambo limezungumzwa sana na fans wa Kiba nikiwemo mimi, na hii ndio tofauti na uzi wetu na uzi wa watu wengine, ambao huona wanaowashabikia wakoperfect hata kama wanakosea au kuikosea jamii kwa vitendo vichafu.
Hilo ulilosema liko wazi ni mpuuzi tu au shabiki maandazi ndiye anayeweza kukubishia, ila kwa sasa tulio humu tunafahamu na tunakubaliana na wewe moja kwa moja kuhusu uzembe huu. Kiba ana tungo nzuri sana, ambapo kwa Bongo waweza mshindanisha na Mwana FA, na ana sauti tamu hana mfano, na anatamka Swahili sanifu hana mfano.
Ova
 
Ukiwa umesoma au kupitia comments za humu, hili jambo limezungumzwa sana na fans wa Kiba nikiwemo mimi, na hii ndio tofauti na uzi wetu na uzi wa watu wengine, ambao huona wanaowashabikia wakoperfect hata kama wanakosea au kuikosea jamii kwa vitendo vichafu.
Hilo ulilosema liko wazi ni mpuuzi tu au shabiki maandazi ndiye anayeweza kukubishia, ila kwa sasa tulio humu tunafahamu na tunakubaliana na wewe moja kwa moja kuhusu uzembe huu. Kiba ana tungo nzuri sana, ambapo kwa Bongo waweza mshindanisha na Mwana FA, na ana sauti tamu hana mfano, na anatamka Swahili sanifu hana mfano.
Ova

Nimeipenda hii,hasa hapo kwenye tungo na sauti...awweee
 
Sisi Mashabiki wa Kiba pamoja na mahaba yooote hatusiti kumpa Kiba ukweli wake ili ajirekebishe....umpendae unamweka bayana....sio kusifia kila kitu utadhani umekua ndondocha bwana aaarghhh...!
 
Back
Top Bottom