Kuna maajabu sana hapa ulimwenguni. Fikiria, mtu anajilazimisha kuponda kitu kizuri sana, kilichofanyika kitaalam ili tu kuburudisha nafsi yake. Haya ni mambo ya kushangaza sana, na yamenifanya nijiulize ni watu wa namna gani ambao tunajadili nao kuhusu music.
Mnaijua show aliyochapa Alikiba kwenye Koroga Festival? Mnajua akina nani walialikwa kuhudhuria ile show? Mjue kabisa kama Alex Okosi alikuwepo na alikubali uwezo wa Alikiba, msidhani kama MTV Base walikurupuka tu kujipendekeza kwa Alikiba, walipata comments za Okosi.
Ni hivi tu Alikiba alivyo hapendi masifa yasiyo na maana, anatulia tu ili wakati ukifika watu waone wenyewe. Muziki mzuri unajisema wenyewe, hauna haja ya mbwembwe nyingi, kazi inaonekana.
Wajuzi wa muziki wote wamehamaki kwa Lupela hadi wanaachia nyimbo zao ovyo ovyo ili kujaribu kuipoteza lakini ngoma bado iko palepale imesimama. Wanahangaika kusaka visingizio vingi ili kuishusha hadhi lakini hawapati sababu ya maana ya kueleweka.
Na nakuambia huu mwaka tutaheshimiana tu, maana kuna video nyingine mbili zimepigwa Hollywood zimewekwa kabatini zikisubiri muda ufike ziachiwe.
Ova