Ali Mufuruki on ITV: Kilimo kwanza kiliishia wapi? Viwanda vya Saruji kupata hasara si ishara nzuri

Ali Mufuruki on ITV: Kilimo kwanza kiliishia wapi? Viwanda vya Saruji kupata hasara si ishara nzuri

Very funny!

Yaani mtu ambae yupo kwenye private sector for almost 30 years bado ni lazima asome Google kufahamu mazingira ya biashara ya Tanzania na nini kinahitajika?!

Ameshawahi kuwa mwenyekiti au bado Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania!

Hapo kabla au hadi sasa amepata kuwa board member wa Mwananchi Communication, Nation Group (KE) pamoja na Stanbic Tanzania pamoja na ATC!

Nadhani hadi sasa bado ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wananchi Group inayomiliki ZUKU tv & ZUKU Fibre!

Yaani kwa akili yako mtu kama huyo atashindwa kufahamu nini kinahitajika Tanzania when it comes to business?!
Weeee! Unadhani wote tuko kiwango cha Mufuruki wako? Yuko private ipi? Walipoalikwa ikulu uliona walichokuwa wanaeleza? Wengi waliishia kutetea biashara zao badala ya mazingira ya biashara ndani ya nchi. Hawa ni wale wale! Wakitafuta PPP maana yao ni kutafuta kupendwa na wanasiasa au kuzoeana nao wapate nafasi ya wizi.

Hebu aeleze infosys yake ilivyoingia na Lugumi. Aeleze ubora wa kazi yake ktk CRDB. Jizi huyu!
 
Tafuteni tweets zake za early 2016. Huyu ni miongoni wasomi na wafanyabiashara wakubwa walio amini sera za mkulu ni muarobaini wa matatizo yakiwemo ya uuchumi wa nchi yetu. Bila shaka naye pia atakuwa ameanza kuisoma namba
 
Weeee! Unadhani wote tuko kiwango cha Mufuruki wako? Yuko private ipi? Walipoalikwa ikulu uliona walichokuwa wanaeleza? Wengi waliishia kutetea biashara zao badala ya mazingira ya biashara ndani ya nchi. Hawa ni wale wale! Wakitafuta PPP maana yao ni kutafuta kupendwa na wanasiasa au kuzoeana nao wapate nafasi ya wizi.

Hebu aeleze infosys yake ilivyoingia na Lugumi. Aeleze ubora wa kazi yake ktk CRDB. Jizi huyu!
Nonsense! Nilitarajia u-challenge kwa hoja hayo niliyotaja badala ya kuja na viroja!!

Sasa habari za eti "...Mufuruki wako zinatoka wapi?" Btw, wa wapi wewe usiyefahamu hata umuhimu wa PPP kwa watu wa private na hata wa public sector?!
 
Mfuruki ni mjanja mjanja tu wa hapa mjini. Fobes wanasema Jamaa yupo top 10 kwa matajiri Tanzania, wakati jamaa hatujui kabisa bussness zake zaidi ya maduka ya Wolwoth sidhani kama ana kiwanda or tangible investment

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu google "ali mufuruki"........bila quotation marks
 
Ameulizwa swala la Kenya kuwa ndio exporter namba 1 wa parachichi wakati sisi tuna ardhi kubwa kuliko kenya.

Akajibu changamoto iliyoko tanzania ni kutokuwepo kwa commercial farming na kutokuwepo kwa agri proccesing industry..
Ametoa mfano bukoba ( kimondo bay sina hakika na usahihi wa hili jina) kilimo cha parachichi kinafanyika lakini

1. hakuna kiwanda cha kuongeza thamani ya parachichi

2. Gharama za usafirishaji kuzipeleka mwanza ni kubwa sana hali inayopelekea bei ya mwisho kwa mlaji kutokuwa nzuri sana.

Yuko sahii. Ukweli ni kuwa mkoa wote wa Kagera unafaa kulima parachichi na atakaye pata njia ya kuyafikisha Entebbe kwa ajiri ya export atakuwa ameukata.
 
Ni mmoja kati ya wachache walioifilisi CRDB orijino Kabla haijachukuliwa na akila Kimei. Baadaye aliunda kikampuni kikiitwa infosys ambacho kilitajwa kwenye mambo ya Lugumi na Polisi wao. Kikampuni kikawa uchochoro wa kupitishia pesa nzito za mirahi krk awamu za upigaji. Mtu huyu hafai hata kusikilizwa.

Tatizo pia ni hao waandishi wa habari, Wanatafuta mtu wa kuzungumzia mambo muhimu ya kitaifa bila hata kuangalia historia yake na bila kumuuliza mambo yake ya nyuma. Anapoachiwa kubwabwaja, baadaye anawekwa kwenye kundi la wenye influence. Baadhi yetu wenye ufahamu wa mtaani tunamuona bonge la mtaalamu! Anatakiwa asipewe muda wa 'kuelimisha' umma, badala yake aitwe kuulizwa mambo yake ya hovyo hovyo.
Very interesting. Wewe unamuona hafai lakini kampuni kama Vodacom wanampa uenyekiti. Kati yako na Vodacom tumuamini nani?
 
Yuko sahii. Ukweli ni kuwa mkoa wote wa Kagera unafaa kulima parachichi na atakaye pata njia ya kuyafikisha Entebbe kwa ajiri ya export atakuwa ameukata.
Entebe yanatakiwa yafike yakiwa kwenye firm gan mkuu?
 
Jifunzeni kuchangia kwa hoja na siyo kuchangia kimajungumajungu. Sijui kwa nini Watanzania wengi hawana uwezo wa kujenga hoja. Uwezo wao unaishia kujenga majungu

Unayaita majungu kwasababu yanamuumbua mtu wako lakini tungekuwa tunamsifia kuwa ana umahili ungeziita hoja!! Tatizo la wadanganyika ni njaa, na ndio maana ni rahisi kuwadanganya na wao kuwa wasahaulifu upesi sana!!
 
Infosys na infotech ni vitu viwili tofauti.

Halafu swala la lugumi lifuatilie vizuri sababu unachanganya madesa mkuu
Yawezekana Boss lakini ukweli uko pale pale! Ni mmoja waliohusika kuiibia CRDB original
 
Very interesting. Wewe unamuona hafai lakini kampuni kama Vodacom wanampa uenyekiti. Kati yako na Vodacom tumuamini nani?
Interesting? Learn operating or success route ya mashirika. Unafahamau sababu ya kumuweka hapo? Hao wanasiasa waliokuwa na position Voda, kwani sababu ilikuwa ni business competence? Mashirika huweka hata wezi ili wasaidie shirika lao, bora tu wao wasiwe waathirika.
 
Nimemsikiliza, ana mambo mazuri sana na uelewa mkubwa wa masuala ya uwekezaji na mitaji.

Alitolea mfano Singapore, wanapotafuta mwekezaji, wanakuwa wamefanya utafiti wa kutosha juu ya uwezo was Hugo mwekezaji wanayemtaka, na wao kama nchi wanakuwa pia wamekwisha Fanya utafiti wao na kuweka mazingira rafiki, pamoja na kumhakikishia faida atakayopata.

Pia wanamhakikishia Sera zisizobadilika badilika kwenye uwekezaji. Nimemfurahia sana, na watendaji wetu has a TIC na Waziri wa viwanda na biashara, wana kitu cha kujifunza.

Amedai, huwezi kusema tunataka kuwa nchi ya viwanda bila kuainisha aina ya viwanda, mkakati wa kupata wataalamu, mkakati wa kupata malighafi na masoko pia. Akatoa mfano, Tz kwa mwaka wahitimu mainjinia ni 1,200 nchi yenye watu milioni 50 wakati Singapore watu mil 30 inawahitimu zaidi ya laki moja kwa mwaka.
Hilo linawezekana. Basi tupe biashara au investment zake kubwa hapa bongo

Sent using Jamii Forums mobile app

Ali Mfuruki ndiye wakala mkuu wa kampuni ya Woolworths hapa nchini na mwenyekiti wa Tanzania Round Table miongoni mwa shughuli zake nyingi hapa Tanganyika
 
Ha ha ha, mkuu hata wewe ukiamua kusoma taarifa husika kwa ajili ya presentation inawezekana, na tunaweza kudhani unajua sana kwenye hiyo sekta.

Applicability ndo changamoto, ni sawa na Mwl Kashasha anavyochambua mpira, mpe ukocha uone.
Humjui mwl Kashasha weye wacha ubwabwa! Mtafute Enock Bwigane au Jesse John wa TBC wakwambie mwl Kashasha ni nani na kama una mtandao wa haja muulize Kassim Majaliwa atakwambia Mwl Kashasha ni nani!
Usilolijua litakusumbua weye! Ali Mfuruki ni kichwa hasa sio wa kukaririshwa kama vichaa vichaa wengine, the guy knows his stuff, do your home work properly kabla ya kukimbilia kwenye keyboard! Bs
 
Soma msg hizi ili baadaye ujue uliyemsikiliza siyo mtaalamu, ni Bonge la Tapeli.
Kama utapeli unampa mtu mafanikio kiasi hicho, na wala hatujasikia akiitwa police au mahakamani, kwa nini na wewe au Mimi tusiwe matapeli mkuu?
 
Humjui mwl Kashasha weye wacha ubwabwa! Mtafute Enock Bwigane au Jesse John wa TBC wakwambie mwl Kashasha ni nani na kama una mtandao wa haja muulize Kassim Majaliwa atakwambia Mwl Kashasha ni nani!
Usilolijua litakusumbua weye! Ali Mfuruki ni kichwa hasa sio wa kukaririshwa kama vichaa vichaa wengine, the guy knows his stuff, do your home work properly kabla ya kukimbilia kwenye keyboard! Bs

Kuna mahali nimetamka kwamba Ali siyo kichwa?

My point is, anyone can present a thing he/she read about, doesn't tell how genius that person is.

And, talking isn't doing.
 
Back
Top Bottom