Wewe nawe yawezekana kuna mahali hakujakaa sawa.
Huyu Ntobi ametoa maneno ya hovyo, tena akijifanya kuwakilisha kauli ya chama wakati yeye si msemaji wa chama wala hana mamlaka ya kukisemea chama.
Yeye anasema eti chama kilimteua Lisu mwaka 2020 kugombea Urais kwa sababu Lisu ni mropokaji!! Jiulize:
1) Lisu alichaguliwa na vikao halali vya chama kuwa mgombea kupitia CHADEMA. Hakuteuliwa na Ntobi. Je, wewe unaamini kwamba CHAMA kiliweka sifa ya anayetakiwa kuteuliwa kuwa mgombea, anatakiwa awe mropokaji? Na kwa kuzingatia sifa hiyo, ndiyo Lisu alishinda? Je, yeye Ntobi ndiye ameteuliwa kukisemea chama?
Ntobi ana uhuru wa kumchagua, au kumpamba mgombea yeyote ambaye yeye anamtaka, lakini hana haki wala mamlaka ya kuyafanya hayo kwa kujipa mamlaka ya chama. Kwa hiyo hana haki kuyaongelea maamuzi ya chama, iwe ya sasa au yaliyowahi kufanywa.
Kamati ya nidhamu, imchukulie hatua huyu mropokaji Ntobi kwa kukidhalilisha chama kuwa eti kiliwapelekea wananchi mgombea ambaye angeweza kuwa Rais, kuwa sifa kubwa iliyozingatiwa ni mropokaji.