Alichoandika Mnyika: Maneno ya Ntobi si msimamo wa Kamati kuu Wala CHADEMA na mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti huyo yako chini ya Kanda

Alichoandika Mnyika: Maneno ya Ntobi si msimamo wa Kamati kuu Wala CHADEMA na mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti huyo yako chini ya Kanda

Watanzania wanatamani mabadiliko tatizo mpaka sasa hakuna chama mbadala,vilivyopo ni taasisi za watu fulani fulani za kujipatia kipato binafsi na wapambe wao.
 
Hata wale kina Nyerere, boni, kilewo, ni washamba. kuna steji za kiuongozi ukifika hutakiwi kuwa emotional kiasi kile. Sio busara kuonesha hisia za uchawa kwenye hali kama ya sasa cdm. Kiongozi lazima uoneshe ukomavu flani wa kuweza kutulia kwanza ukisubiri lolote lijalo.

kwa mfano: Mbowe akisema hatogombea, wao watafanyaje. Bila shaka watateseka sana. In some situations, neutrality is a better choice!

YESU NI BWANA&MWOKOZI
Sentensi ya mwosho imeingizw kwa sababu ya stress zako au msongo wa mawazo
 
IMG-20241220-WA0020.jpg
 
Watanzania wanatamani mabadiliko tatizo mpaka sasa hakuna chama mbadala,vilivyopo ni taasisi za watu fulani fulani za kujipatia kipato binafsi na wapambe wao.
wakimwangusha Lisu kwenye hili, Ibara ya tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, isomeke: "Tanzania ni nchi ya mfumo wa chama kimoja"

tuache unafiki
 
Wapambe/Chawa wasipokuwa makini wanaenda kukiua chama,wanatakiwa watambue chama sio mali ya mtu binafsi au watu fulani tu kiasi ambacho mtu mwingine akionesha nia ya kugombea uongozi basi iwe nongwa.
Wakumbuke Mbowe ni binadamu leo yupo kesho hayupo, Je ikitokea hivyo wataweka sanamu lake ndiyo liongoze chama? Kila mwanachama ana fursa sawa ya kugombea uongozi ndani ya chama na mwisho wa siku wajumbe wataamua nani awe kiongozi.
 
Hivi watu wanajua matusi au ni mahaba tu..mtu kusema jamaa hawezi kuwa kiongozi hata wa mtaa ni tusi??? Mbona Mama Samia watu wanasema zaidi ya hayo, mkiulizwa mnasema ndo demokrasia hiyo, lkn kwa Lissu mtu anasemwa anatukanwa.
Kuwa kiongozi mkubwa sio lele mama..lazima mawe yalushwe tu
Kiongozi wa CCM wa mkoa hawezi kutoa kauli hiyo dhidi ya kiongozi wake wa Taifa wa chama.
Kiongozi wa chama pinzani akisema hivyo ni sawa kabisa lakini sio kiongozi wa chama ngazi ya mkoa atoe maoni hayo kwa kiongozi wa chama chake Taifa na mgombea urais.
Hapo hamtukani na kumdhalilisha huyo kiongozi bali chama kilichompa uongozi.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Bw Emmanuel Ntobi licha ya kutojibiwa chochote na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Tundu Lissu kwa muda mrefu Sasa bado ameendelea na kumdhihaki, kumdhalilisha na kumtweza utu wake kinyume kabisa na Katiba, kanuni na miongozo ndani ya CHADEMA .

Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw.John John Mnyika alipoulizwa na Wanachama wa CHADEMA mitandaoni kama anachokifanya Mwenyekiti wa Shinyanga kama ni msimamo wa Kamati kuu au CHADEMA,

Kwa haraka Katibu Mkuu huyo alimjibu Mwanachama huyo kuwa huo si msimamo wa Kamati kuu Wala CHADEMA na mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti huyo yako chini ya Kanda na anamshangaa kwanini Emmanuel Ntobi anaendelea kutamba kwa kutweza wengine utu wao hadharani tena mitandaoni Waziwazi bila kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu.

Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 kosa alilolifanya BW. Emmanuel Ntobi adhabu yake ni kufutwa Uongozi au Kufukuzwa Uanachama au vyote kwa pamoja,

Hata hivyo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Bw Godbless Lemma amesisitiza pia hatua zinapashwa kuchukuliwa ili kuepa visasi na majibizano ya kukidhalilisha chama na wanachma

View attachment 3180661
View attachment 3180647
View attachment 3180816
Kiujumla kama chama Cha siasa nidhamu ni muhimu kwa viongozi wa chama, Yaani makamu mwenyekiti anadharauliwa na kukebehiwa namna hii na mwenyekiti wa mkoa anaangaliwa tu
 
Kiongozi wa CCM wa mkoa hawezi kutoa kauli hiyo dhidi ya kiongozi wake wa Taifa wa chama.
Kiongozi wa chama pinzani akisema hivyo ni sawa kabisa lakini sio kiongozi wa chama ngazi ya mkoa atoe maoni hayo kwa kiongozi wa chama chake Taifa na mgombea urais.
Hapo hamtukani na kumdhalilisha huyo kiongozi bali chama kilichompa uongozi.
Fact, sijajua katiba ya chadema inasemaje juu ya hili
 
Rumble in the Jungle
...and this time, the ruthless heavy handed George Foreman (Mbowe), gonna be KOed by the much younger, savy and flamboyant Mohammed Ali (Lissu). It is time to float like a butterfly and sting like a bee. Lissu let's go!

Lissu bumaye!
 
Back
Top Bottom