Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 14,677
- 18,561
Tatizo lako hupendi mawazo kinzani.Che...
Ikiwa huoni kama unanitukana hakuna shida.
Mimi nina miaka 73.
Unadhani naweza kuwa na mjukuu kwa umri wako?
Nakusihi tuishie hapa.
Hupendi kalamu yangu ukiona post yangu DELETE.
Huna sababu ya kuja hapa umeghadhibika.
Tatizo lako hupendi mawazo kinzani.Che...
Ikiwa huoni kama unanitukana hakuna shida.
Mimi nina miaka 73.
Unadhani naweza kuwa na mjukuu kwa umri wako?
Nakusihi tuishie hapa.
Hupendi kalamu yangu ukiona post yangu DELETE.
Huna sababu ya kuja hapa umeghadhibika.
Pole sana mwanangu Askofu Mohamed Said. Lala ukue. Hawa watakuzeesha bure mwanangu.Tatizo lako hupendi mawazo kinzani.
Mimi sijawahi kukutukana popote ingawa nimeona wengine wanakuambia kuwa ni Mdini.
Mimi sijaghadhibika ila nakupa iliyo kweli:
Historia yako inalenga kutubagua kidini:
Historia ya ujumla tumekubaliana kuwa Watanzania wote tulishirikiana kuleta Uhuru na Umoja ili kudumisha mshikamano kwa vizazi vijavyo:
Historia yako inasema ni Waislamu pekee ndio waliopigania Uhuru wa Tanzania:
Kwa historia yako hii unaitengenezaje Tanzania ijayo kama msomi ?
Hivi vita ya Majini maji ya kumtaa mkoloni ilipiganwa na Waislamu pekee ?
Au Mtemi Mkwawa wa Iringa alipigana na Mjerumani kwakuwa tu alikuwa Mwislamu ?
Kama sivyo hao watawala hawakuwa chachu ya kupigania uhuru wa Mtanzania?
Watu wa Pwani walipambana kumwondoa mkoloni kama watu wa Bara:
Bila ya kuangalia kabila au dini zao:
Wote walishikamana kumwondoa mkoloni:
Habari za Waislamu pekee ndio waliofanya jizihada za kumwondoa mkoloni Mzungu hazina manufaa kwa Watanzania:
Ikiwa wewe unaamini kuwa Watanganyika wote walipiganiaTatizo lako hupendi mawazo kinzani.
Mimi sijawahi kukutukana popote ingawa nimeona wengine wanakuambia kuwa ni Mdini.
Mimi sijaghadhibika ila nakupa iliyo kweli:
Historia yako inalenga kutubagua kidini:
Historia ya ujumla tumekubaliana kuwa Watanzania wote tulishirikiana kuleta Uhuru na Umoja ili kudumisha mshikamano kwa vizazi vijavyo:
Historia yako inasema ni Waislamu pekee ndio waliopigania Uhuru wa Tanzania:
Kwa historia yako hii unaitengenezaje Tanzania ijayo kama msomi ?
Hivi vita ya Majini maji ya kumtaa mkoloni ilipiganwa na Waislamu pekee ?
Au Mtemi Mkwawa wa Iringa alipigana na Mjerumani kwakuwa tu alikuwa Mwislamu ?
Kama sivyo hao watawala hawakuwa chachu ya kupigania uhuru wa Mtanzania?
Watu wa Pwani walipambana kumwondoa mkoloni kama watu wa Bara:
Bila ya kuangalia kabila au dini zao:
Wote walishikamana kumwondoa mkoloni:
Habari za Waislamu pekee ndio waliofanya jitihada za kumwondoa mkoloni Mzungu hazina manufaa kwa Watanzania wasasa na wajao:
Kila eneo la Tanganyika lilipambana kumwondo mkoloni katika eneo lao na sio watu wa Dini fulani:
Father...Pole sana mwanangu Askofu Mohamed Said. Lala ukue. Hawa watakuzeesha bure mwanangu.
I love that mwanangu. Lazima kuongeza madini kichwani mwanangu. Basi kitabu chema mwanangu.Father...
Ndiyo kwanza nangia Maktaba muda wa kulala bado.
Mimi sizeeki kwa kusoma au kuandika.
Nazeeshwa na miaka inaposonga mbele.
Mzee unanifurahisha sana:Ikiwa wewe unaamini kuwa Watanganyika wote walipigania
uhuru wa Tanganyika sawa sina haja ya kukupinga kwani
nimetafiti na kuandika historia ambayo inaghitilafiana
na historia yako.
Mimi najua kuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir
alikuwa mwanachama wa TANU na akiuza kadi za TANU misikitini.
Ikiwa wewe una jina la Askofu aliyekuwa anauza kadi za TANU kanisani
tutajie jina lake tumsome tufahamu historia yake.
View attachment 3313649
Mtaa huu umepewa jina la Sheikh Mohamed Yusuf Badi aliyepigania
uhuru wa Tanganyika Lindi, Southern Province.
hongera kwa miaka 73 mzee saidi. ni mingi kweli kweli, ulitakiwa uwe umeshajifunza mengi na kujua namna ya kuishi na watu na kuvumilia. kweli age is just numbers.Che...
Ikiwa huoni kama unanitukana hakuna shida.
Mimi nina miaka 73.
Unadhani naweza kuwa na mjukuu kwa umri wako?
Nakusihi tuishie hapa.
Hupendi kalamu yangu ukiona post yangu DELETE.
Huna sababu ya kuja hapa umeghadhibika.
I love that mwanangu. Lazima kuongeza madini kichwani mwanangu. Basi kitabu chema mwanangu.
Si adabu kumwita mtu, "We..."We
Mzee unanifurahisha sana:
Hivi unajua ni Mapadre wangapi tena Wazungu waliandaa vita ya Maji Maji ya kuupinga Ukoloni wa Mzungu mwenzao ?
Mzee unatakiwa kurudi shule kujifunza Historia halisi ya Tanganyika:
Yaani mchango wa Wamissionari wa Kukusomesha hadi ukawa na ufahamu wa kudai uhuru wa nchi yako bado huutambui ?
Au unafikiri kudai Uhuru kunataka vita za Bunduki tu ?
Hivi mzungu angetaka kututawala milele wewe na Waislamu wenzako mngeweza kumzuia ?
Kwa kusoma Dua ?
Au hujui kuwa hiari ya Wazungu wenyewe ndio iliyotupa Uhuru Watanganyika ?
Sasa mzee wangu (kama ulivyo pendekeza) huko chuoni kwako ilikuwa unasoma nini ?
Hukusoma kuwa Tanganyika tulipata Uhuru toka kwa Wazungu kwa kukumbushana mikataba yao wenyewe tu:.
Na sio kwa vita na Waislamu...!
..ni moja ya wadau walioeneza na kuimarisha uislamuUislamu haukuletwa na waarabu someni historia
Umependekeza suluhisho la kijinga sana.Ndugu Muhamed said, wewe pendekeza tu:
Labda kama unataka sisi wa dini nyingine tuhamie Kongo mmbaki wapigania uhuru Waislamu hapa Tanzania wewe pendekeza tu:
Au kama unapendelea Tanzania ifuate Islamic Laws muwe mnachinja Mashoga na Wazinzi kila Ijumaa baada ya swala wewe sema tu.
Tatizo lako ndugu Muhamed Saidi, kila andiko lako ni la kulalamika tu:
Sisi tunao kufuatilia tunataka sasa utoe hitimisho (Conlusion)
Na kuna hitimisho Mbili tu:
Mosi, tuwa achie Wapigania uhuru Waislamu hii nchi, kwakuwa ndio walio uleta Uhuru:
Pili, tugawane mikoa,
Waislamu mpate mikoa yenu ili muishi kwa kutekeleza Sharia zenu kwa kushirikiana na waasisi wa dini yenu Waarabu:
Sisi Wakristo tupewe mikoa yetu na ni marufuku kwa Mkristo au Mwislamu kuishi katika mkoa usio wake:
Kati ya hitimisho hizi mbili Mzee Msomi Muhamedi Saidi unachagua ipi ?
Tumechoka na maandiko yako yaleyale ya kila siku:
Sema unataka nini?
Utafiti bila hitimisho ni kama Pumba tu:
Kwa hiyo AA ilikuwa Association ya waislamu?Castr,
Historia ya African Association vipi iliasisiwa mwaka wa 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 iliandikwa na Kleist Sykes baba yake Abdul Sykes kabla hajafariki mwaka wa 1949.
Historia hii ipo Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam, East Africana kama Seminar Paper ya Idara ya Historia (1968).
Seminar Paper hii imeandikwa na mjukuu wa Kleist, bint wa Abdul Sykes jina lake Aisha Daisy Sykes akiwa mwanafunzi University of East Africa 1968 akisoma History and Education.
Zipo pia Nyaraka za Sykes ambazo ndizo nilizotumia kuandika historia ya TANU kupitia maisha ya Abdul Sykes.
Nyaraka hizi zinarudi nyuma miaka 100.
Ni haki zipi za waislamu na ukweli usioheshimiwa?Umependekeza suluhisho la kijinga sana.
Suluhisho hakuna mbili ni moja tu.Waislamu na wakristo hawawezi kutenganishiwa mikoa.Muhimu haki za waislamu na ukweli viheshimiwe.
Ukweli usioheshimiwa ni kutotajwa wahusika halisi wa uhuru wa Tanganyika na badala yake historia yote kuanza na kumalizia na Nyerere.Tena hayo yamo kwenye vitabu vinavyofundishwa mashuleni.Ni haki zipi za waislamu na ukweli usioheshimiwa?
Amandla...
Na wahusika halisi wote walikuwa waislamu?Ukweli usioheshimiwa ni kutotajwa wahusika halisi wa uhuru wa Tanganyika na badala yake historia yote kuanza na kumalizia na Nyerere.Tena hayo yamo kwenye vitabu vinavyofundishwa mashuleni.
Haki muhimu ni kunyimwa ajira na haki za kielimu kwa waislamu.Mwanzoni ilisemwa hawakusoma na baadae hata waliosoma huwa wanawekwa pembeni.
Umeongea pointi sana:Umependekeza suluhisho la kijinga sana.
Suluhisho hakuna mbili ni moja tu.Waislamu na wakristo hawawezi kutenganishiwa mikoa.Muhimu haki za waislamu na ukweli viheshimiwe.
Kwani kuna baya lolote Askofu Pissa amelisema? Hili zee nalo wakati mwingine linakuwa kama andazi!Ni facebook huku akinakili video ya tamko la Askofu Wolfang Pissa Ambaye Pia Ni Rais Wa Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania.
--------------------------
ASKOFU ANAIJUA HISTORIA YA KANISA KATOLIKI LINDI TANU ILIPOINGIA SOUTHERN PROVINCE 1955?
N miaka mingi sasa toka nilipofika kuliona Kanisa Katoliki Lindi wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.
Kanisa hili lina historia nzuri sana baina ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Waislam wengine wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.
Nakuwekea hapo chini kipande nilichoandika kuhusu kanisa hili mwaka wa 1955 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:
Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi.
Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.
Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.
Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.
Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.
Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.
Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.
Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.
Misa hii ‘’maalum,’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.
Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam.
DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara.
Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi la TANU uliohudhuriwa na Nyerere na Ali Mwinyi Tambwe.
Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC.
Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara.
Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja.
Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia.
Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano.
Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao.
Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe.
TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.