Alichokifanya huyu jamaa, kweli tutafute pesa sana na usimwache Mungu

Kwanza kwa Tanzania sahau kabisa,ukijaribu kufanya hivi utaambiwa wewe unafanya kampeni ili umuondoe mbunge/diwani wa hapa utaletewa mizengwe kibao.mmesahau lile sakata za mzee Bakhresa na pale kigamboni fery.

Huku mtaani kwetu umeme ulichelewa kutoka main road ambako umeme umepita mpaka hapa ilikuwa kama 1km,kuna mdau alikuwa kajenga jumba lake zuri kafatilia umeme hadi kaenda dodoma kukutana na katibu wa wizara kuwa yuko tayari apigiwe cost zote atalipa including mafundi ,nguzo hadi transformer ,ila serikali ikamchomolea wanasiasa baadhi walijua angeteka nyota yao.

Lakini tukashukuru tulimdaka Kalemani kipindi hicho akiwa waziri tukamsogezza akashangaa kaya zaidi ya 5000 hazina umeme akampiga mkwara meneja mkoa ndio ikawa heri yetu.

Sometimes huu umaskini wa kwetu unachagizwa na wanasiasa what if kama kila mtz akiwa anajiwea nani utamdanganya akupe kura kwa hongo ya kanga na kofia
 
kwanza kwa Tanzania sahau kabisa,ukijaribu kufanya hivi utaambiwa wewe unafanya kampeni ili umuondoe mbunge/diwani wa hapa utaletewa mizengwe kibao.mmesahau lile sakata za mzee Bakhresa na pale kigamboni fery...
Duuh! ni wapi huko mkuu?

Yani wanasiasa wako radhi kwa chochote ili mradi watetee vyeo vyao! Wako radhi watu kuumia hata kufa yani!

Ona sasa,wamewatesa wananchi kwa sababu za kujinga kabisa
 
ishu inakuja kwa serikali ya huo mji, je wataweza kuzisimamia hizo assets?hapo ndo utata
 
Kenya pia kuna jamaa kama huyo mdiaspora kajenga mji wake ndani ya kijiji chao...

 
a) Kwa nini mkuu?.
b) Na je wewe you're not materialistic?
Binafsi naona hakuna mbadala wa UTU.

Pili, Mali nyingi, status na pesa ni siyo vitu asili. Ni vitu vya kutengeneza tu ambavyo ndani ya muda mfupi unaweza kuamka havina thamani yoyote.
 
Dah..!! Hivi ingekuwaje kama angekuwa amefanya mabaya unayoyasema, LAKINI AWE HAJAJENGA KWAO?
Duniani watu hawataki kusikia habari nzuri.

Ingekuwa habari inaonesha jamaa anaponda mali huko visiwa vya Ibiza na watoto wazuri.

Wengi tungempongeza, " huyu ndio mwanaume, anajua kutumia pesa zake"
 
Angeenda kuwaondoa wale wa makoko Community wanaoishi juu ya maji ingeleta maana sn
 
Ana akili nzuri.
 
Bora hata huyo ako na njia nzuri za kutumia pesa zake za majini.
 
Nafkiri kulea asilimia kubwa ni wafugaji angeweka kiwanda Cha kusindika mazao yatokanayo na wanyama mfano kusindika maziwa nyama ngozi n.k
 
ishu inakuja kwa serikali ya huo mji, je wataweza kuzisimamia hizo assets?hapo ndo utata
Wameweza mkuu nimefuatilia, mfano hospitali iliyokabidhiwa kanisa catholic imekifanya kijiji kuwa updated plus movement za watu hadi kutoka mjini wanakuja.

Kuna kitivo cha uchunguzi wa magonjwa hadi wazungu wanakuja hapo kutoa mafunzo na kujifunza so sidhani kama patadoda kama chato!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…