Masaningala
JF-Expert Member
- Nov 19, 2010
- 543
- 199
Zanzibar tutasimama kwenye hoja hadi tufike pale tutakapo . Mungu ibariki Zanzibar
nchi kadogo tunalisumbua bonge la nchi .
Tembo lazima atamtapika chura alie mmeza
Wazanzibari mna haki ya kudai mnachodai. Muungano sio msahafu toka mbinguni. Hata Mungu mahali pengine na wakati mwingine amesema usifungamane na wao usionia nao pamoja. Miaka hamsini tumevumiliana na inaonekana umoja wetu unazidi kuwa karaha zaidi. Katika Biblia takatifu, Ndugu wawili, Ibrahimu na Lutu walikuwa wakikaa pamoja na kuchunga mifugo yao pamoja, lakini wakati ukafika watumishi wao wakaanza kugombana. Abrahamu akamwambia Lutu, sii vyema sisi tugombane, tazama ardhi ni kubwa wewe nenda upande huu na mimi nitaenda upande ule na hii itakuwa suluhisho la ugomvi kati ya watumishi wangu na wa kwako. Wakati umefika kwa dhati kabisa, turuhusu Zanzibar iwe nchi kamili na Tanganyika vivyo hivyo. Ila tubaki na shirikisho la masuala tutakayokubaliana kwa uwazi wa pande zote.