Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...

nilitembelea zanji eneo la makunduchi nikaamini maisha huko bado saaana maana shamba la mihogolinalimwa kwa kutumia panga kwani eneo lote ni jiwe, hivyo unatoboa jiwe na kujaza udongo kisha unapanda muhogo, ukivuna unapanda tena hapohapo. sikuamini machoyangu, pia nikakuta wale ndiyo wanaojiita wazanzibar asilia na mpaka wana lugha yao, lakini ukienda mbali sana unakuta wale ni wandengeleko, wamakonde ,wanyamwezi nk hivyo nadhani maisha yakiwashinda bado watakimbilia tanganyika kudai huku ndiyo asili yao.
 

Una uhakika na unayoyasema? Wanzanzibar wangapi walikuwa wamesoma kabla ya Muungano? Shivji ni Mzanzibar? ulitaka walimu wa vyuo vikuu waishi milele?
 
chabuso,

..kabla NECTA[baraza la mitihani] haijaanzishwa, wanafunzi wa TANGANYIKA na ZANZIBAR walikuwa wanafanya mitihani ya EAST AFRICAN EXAMINATION COUNCIL.

..miaka ya nyuma zaidi wanafunzi walikuwa wakifanya mitihani ya CAMBRIDGE LOCAL EXAMINATION SYNDICATE.

..swali la kujiuliza ni kwanini Zanzibar haikuanzisha baraza lake la mitihani baada ya kujitoa kwenye East African Examination Council??

NB:

..Prof.Issa Shivji ni mzaliwa wa Kilosa, Tanganyika.

cc: KVM
 
Last edited by a moderator:
Bora muondoke tu. Manake mna kelele sana. Na mtajuta. Manake mpaka sass tunawalipia kila kitu. Jussa ungefanya cost benefit analysis ndo ungejua watu wanachokwambia.

Nadhani weye ndio utupe hiyo detailed cost benefit analysis. Hili la wazinzibari kulipiwa kila kitu uzushi mtupu usiokuwa na mshiko wowote.
 
Bora mkae kwenu mle halua na tende kwani mmetunyonya sana.
 
Nadhani weye ndio utupe hiyo detailed cost benefit analysis. Hili la wazinzibari kulipiwa kila kitu uzushi mtupu usiokuwa na mshiko wowote.

Acha kuwa mvivu wa kufikiri, kama hujui Zanzibar wanachangia mapato kiasi gani na pia wanatumia kiasi gani katika hii Serikali ya Muungano kwa sasa kaa kimya.
 

Zanzibar haikuanzisha baraza lake la mitihani baada ya kujitoa kwenye East African Examination Council kwasababu ya wanasiasa wazembe....vijana wa sasa hivi wameshtuka wamechoka kuburuzwa
 
Una uhakika na unayoyasema? Wanzanzibar wangapi walikuwa wamesoma kabla ya Muungano? Shivji ni Mzanzibar? ulitaka walimu wa vyuo vikuu waishi milele?

Siku hizi kila kitu kiko wazi ukitaka kujua wazanzibari wangapi walikuwa wamesoma kabla ya Mungano fanya utafiti.......kwaufupi Tanganyika ilikuwa nyuma sana kielimu kabla ya mungano huwezi kufanananisha na Zanzibar
 





watanganyika ndio wenye furaha zaidi kwani wao hawakuwa na mamlaka kamili, tanganyika ilimezwa na muungano. Na yale mambo ya kupata kazi huku bara ndiyo basi tenaaaaaa, maana mmeshakuwa nchi nyingine.
 

Kaka hizi zote ni dhana zako,sikirii kama hao wanasiasa na wanaharakati hawajui hayo uliyoyaelezea hapa,huu mchakato umeanza zamani tangu enzi za Aboud Jumbe kwa matazamo wangu watu wameshajipanga,kila kitu kinawezekana
 
Hatutaki serikali ya tanzania bara bali serikali ya tanganyika.............. Tume inaficha nini? Kwa nini wazanzibar nao wasitumie serikali ya tanzania visiwani? Wanatuharibia historia
 
Jamani mimi ningependa kujua mustakabali wa hawa wazenji waliopo Tanganyika na watanganyika waliopo Zenji, rasimu imesema chochote kuhusu hilo? Vipi suala la Ardhi wataendelea kuruhusiwa kujenga huko bara hawa watu au ndiyo basi tena? Maana sijaona kama Ardhi imeorodheshwa kama jambo la muungano.
 
Mwambieni Jussa atulie. Hao waarabu wake anaodhani watamsaidia kuendesha nchi angoje watampa hela. Ila nina wasi was Zanzibar baada ya kuvunjika muungano inaweza ikawa kama Somali
 
Mwambieni Jussa atulie. Hao waarabu wake anaodhani watamsaidia kuendesha nchi angoje watampa hela. Ila nina wasi was Zanzibar baada ya kuvunjika muungano inaweza ikawa kama Somali
Hata Kamandoo Salmin Amour alijipendekeza kwa Ghadaffi na kuahidiwa kila aina ya misaada, mwisho wake kunyang'anywa mke, na kapewa upofu ili atulie kabsaaa, ili makamanda wa muammar wapokee mabaki ya mzee na kuindelea kupekuwa. ndio utamaduni wao.
 
Uko sawa kabisa. Watanganyika hatujajiandaa. Na tatizo letu sio jina la nchi yetu. Tatizo letu ni kuwa bado tunaona fahari kuitwa Watanzania. Wengi wengi wetu tumezaliwa ktk Utanzania na sio utanganyika. Kimsingi wengi wetu hatukuwa tunalilia sana tanganyika ILA TUMECHOSHWA NA KELELE ZA WAZANZIBARI kiasi kwamba tunaona bora waende.Kimsingi kuanzishwa kwa serikali tatu ni kujibu mahitaji ya Wazanzibari, wengi wetu tulipenda serikali moja au kuvunjwa kwa muungano kabisa kila watu wachukue nchi yao kuepusha shari zaidi.Lakini katika ulimwengu wa leo na uchumi wa kisasa, muungano ni muhimu sana, ndio maana unaona USA, EU, Au, n.k. Hii yote ni mifumo mbalimbali ya muungano wa kisiasa au kiuchumi kwa viwango tofauti tifauti. Hii ni kuonyesha mwanadamu anafanikiwa zaidi katika umoja kuliko katika utengano. Tatizo kubwa la mwanadamu ni kuushinda ubinafsi wake, kiburi (egoism) na uroho wa madaraka. Hapa ndipo muungano wetu ulipokwamia na sasa tunaanza kupiga hatua kali zaidi kurudi nyuma (kwenye utengano) kuliko kwenda mbele. Siamini kama Watanganyika WANAIHITAJI serikali yao japo najua wapo WANAOITAKA!
 
Sijui kwanini wanawang'ang'ania hawa jamaa,wapewe chao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…