Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...

Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...

nilitembelea zanji eneo la makunduchi nikaamini maisha huko bado saaana maana shamba la mihogolinalimwa kwa kutumia panga kwani eneo lote ni jiwe, hivyo unatoboa jiwe na kujaza udongo kisha unapanda muhogo, ukivuna unapanda tena hapohapo. sikuamini machoyangu, pia nikakuta wale ndiyo wanaojiita wazanzibar asilia na mpaka wana lugha yao, lakini ukienda mbali sana unakuta wale ni wandengeleko, wamakonde ,wanyamwezi nk hivyo nadhani maisha yakiwashinda bado watakimbilia tanganyika kudai huku ndiyo asili yao.
 
Zanzibar kabla mungano mitihani ya secondary ilikuwa inatoka oxford England,ilimu ya juu walikuwa wanafunzi wanapelekwa kwenye vyuo vinavyojulikana kimataifa,unajua kuwa walimu wa mwanzo wa chuo kikuu cha Daresalam wengi walikuwa wazanzibar,wamebakia wachache chuoni akina Shifji.....hamna kisichowezekana mkuu

Una uhakika na unayoyasema? Wanzanzibar wangapi walikuwa wamesoma kabla ya Muungano? Shivji ni Mzanzibar? ulitaka walimu wa vyuo vikuu waishi milele?
 
chabuso,

..kabla NECTA[baraza la mitihani] haijaanzishwa, wanafunzi wa TANGANYIKA na ZANZIBAR walikuwa wanafanya mitihani ya EAST AFRICAN EXAMINATION COUNCIL.

..miaka ya nyuma zaidi wanafunzi walikuwa wakifanya mitihani ya CAMBRIDGE LOCAL EXAMINATION SYNDICATE.

..swali la kujiuliza ni kwanini Zanzibar haikuanzisha baraza lake la mitihani baada ya kujitoa kwenye East African Examination Council??

NB:

..Prof.Issa Shivji ni mzaliwa wa Kilosa, Tanganyika.

cc: KVM
 
Last edited by a moderator:
Bora muondoke tu. Manake mna kelele sana. Na mtajuta. Manake mpaka sass tunawalipia kila kitu. Jussa ungefanya cost benefit analysis ndo ungejua watu wanachokwambia.

Nadhani weye ndio utupe hiyo detailed cost benefit analysis. Hili la wazinzibari kulipiwa kila kitu uzushi mtupu usiokuwa na mshiko wowote.
 
Bora mkae kwenu mle halua na tende kwani mmetunyonya sana.
SAFARI YA KUELEKEA MAMLAKA KAMILI IMEPIGA HATUA KUBWA:

Na Ismail Jussa

Mamlaka ambayo tayari Zanzibar itakuwa imeyarejesha kwa kuondolewa kwenye Muungano kupitia Rasimu ilotangazwa leo ni:

1. Polisi.

2. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.

3. Kodi ya Mapato.

4. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

5. Mabenki ya Kibiashara na Fedha za Kigeni.

6. Leseni ya viwanda na takwimu.

7. Elimu ya Juu.

8. Maliasili ya mafuta na gesi asilia.

9. Baraza la Taifa la Mitihani.

10. Usafiri na usafirishaji wa anga.

11. Utafiti.

12. Utabiri wa Hali ya Hewa.

13. Takwimu.

14. Mahkama ya Rufani.

15. Ushirikiano wa Kimataifa.

KAZI ILIYOBAKI KWA WAZANZIBARI ILI KUTIMIZA MAMLAKA KAMILI

Ni kutumia hatua zilizobakia kuyarejesha pia mamlaka katika mambo muhimu yafuatayo:

1. Mambo ya Nje.

2. Uraia na Uhamiaji.

3. Sarafu na Benki Kuu.

4. Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa.

5. Usajili wa Vyama vya Siasa.

TANBIHI:
Wananchi na hasa Vijana wa Zanzibar tumefikia hatua ya kurejesha mamlaka katika mambo hayo 15 kutokana na umoja wetu na kutumia njia za amani huku tukiwa na msimamo usiyoyumba. Tuendelee kuwa pamoja, tukitumia njia za amani kabisa kukamilisha mamlaka kamili tunayoyataka.

Naiona ileeeee.........
 
Nadhani weye ndio utupe hiyo detailed cost benefit analysis. Hili la wazinzibari kulipiwa kila kitu uzushi mtupu usiokuwa na mshiko wowote.

Acha kuwa mvivu wa kufikiri, kama hujui Zanzibar wanachangia mapato kiasi gani na pia wanatumia kiasi gani katika hii Serikali ya Muungano kwa sasa kaa kimya.
 
chabuso,

..kabla NECTA[baraza la mitihani] haijaanzishwa, wanafunzi wa TANGANYIKA na ZANZIBAR walikuwa wanafanya mitihani ya EAST AFRICAN EXAMINATION COUNCIL.

..miaka ya nyuma zaidi wanafunzi walikuwa wakifanya mitihani ya CAMBRIDGE LOCAL EXAMINATION SYNDICATE.

..swali la kujiuliza ni kwanini Zanzibar haikuanzisha baraza lake la mitihani baada ya kujitoa kwenye East African Examination Council??

NB:

..Prof.Issa Shivji ni mzaliwa wa Kilosa, Tanganyika.

cc: KVM

Zanzibar haikuanzisha baraza lake la mitihani baada ya kujitoa kwenye East African Examination Council kwasababu ya wanasiasa wazembe....vijana wa sasa hivi wameshtuka wamechoka kuburuzwa
 
Una uhakika na unayoyasema? Wanzanzibar wangapi walikuwa wamesoma kabla ya Muungano? Shivji ni Mzanzibar? ulitaka walimu wa vyuo vikuu waishi milele?

Siku hizi kila kitu kiko wazi ukitaka kujua wazanzibari wangapi walikuwa wamesoma kabla ya Mungano fanya utafiti.......kwaufupi Tanganyika ilikuwa nyuma sana kielimu kabla ya mungano huwezi kufanananisha na Zanzibar
 
safari ya kuelekea mamlaka kamili imepiga hatua kubwa:

Na ismail jussa

mamlaka ambayo tayari zanzibar itakuwa imeyarejesha kwa kuondolewa kwenye muungano kupitia rasimu ilotangazwa leo ni:

1. Polisi.

2. Mikopo na biashara ya nchi za nje.

3. Kodi ya mapato.

4. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

5. Mabenki ya kibiashara na fedha za kigeni.

6. Leseni ya viwanda na takwimu.

7. Elimu ya juu.

8. Maliasili ya mafuta na gesi asilia.

9. Baraza la taifa la mitihani.

10. Usafiri na usafirishaji wa anga.

11. Utafiti.

12. Utabiri wa hali ya hewa.

13. Takwimu.

14. Mahkama ya rufani.

15. Ushirikiano wa kimataifa.

Kazi iliyobaki kwa wazanzibari ili kutimiza mamlaka kamili

ni kutumia hatua zilizobakia kuyarejesha pia mamlaka katika mambo muhimu yafuatayo:

1. Mambo ya nje.

2. Uraia na uhamiaji.

3. Sarafu na benki kuu.

4. Ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa.

5. Usajili wa vyama vya siasa.

Tanbihi:
Wananchi na hasa vijana wa zanzibar tumefikia hatua ya kurejesha mamlaka katika mambo hayo 15 kutokana na umoja wetu na kutumia njia za amani huku tukiwa na msimamo usiyoyumba. Tuendelee kuwa pamoja, tukitumia njia za amani kabisa kukamilisha mamlaka kamili tunayoyataka.

Naiona ileeeee.........





watanganyika ndio wenye furaha zaidi kwani wao hawakuwa na mamlaka kamili, tanganyika ilimezwa na muungano. Na yale mambo ya kupata kazi huku bara ndiyo basi tenaaaaaa, maana mmeshakuwa nchi nyingine.
 
zanzibar mmesahau upemba na uunguja? je, mtaendelea kwa jeuri gani. serikali itaweza kuhudumia gharama hizi zilizoongezeka? kwa pato gani, pato la zanzibar not more than bilioni mia tano kwa mwaka. then compere na gharama za uendeshaji zilizo ogezekae(polisi, elimu ya juu, takwimu, n.k).Kumbuka mnategemea sector ya huduma tu hasa mahoteli na watalii wengi walio kuwa wanaingia zanzibar sio wa direct to znzr ni wale waliokuwa wanakuja mbuga za wanyama na kutazama mlima kilimanjaro ndo walikuwa wanamalizia zanzibar then wanakwea pipa. zingatia pia, kwa dizaini hii ukivunjika huu muungano ujue wakija means wanakuja kwenye nchi mbili, so gharama zitaongezeka kwao na kuathiri soko la utarii zanz ambalo ndo linachangia kwenye pato la taifa kwa kiasi kikubwa. Ila kubwa zaidi kwani nyie wazanzibari hamjui yanayo endelea huku zanji, kunakampeni za kuwafukuza wapemba unguja? na ambazo zinashamili sana kila iitwapo leo. u wil spend a lot of time kupambana nyie wenyewe kuliko kujenga nchi.......binafsi siwalaani., bt zanzibar endapo muungano ukivunjika mtatikisika sana na kurecover itawachukuwa mda na msipo angalia you 're going to die. Mnafurahia mauti yenu, sio mbaya lakini

Kaka hizi zote ni dhana zako,sikirii kama hao wanasiasa na wanaharakati hawajui hayo uliyoyaelezea hapa,huu mchakato umeanza zamani tangu enzi za Aboud Jumbe kwa matazamo wangu watu wameshajipanga,kila kitu kinawezekana
 
Hatutaki serikali ya tanzania bara bali serikali ya tanganyika.............. Tume inaficha nini? Kwa nini wazanzibar nao wasitumie serikali ya tanzania visiwani? Wanatuharibia historia
 
Jamani mimi ningependa kujua mustakabali wa hawa wazenji waliopo Tanganyika na watanganyika waliopo Zenji, rasimu imesema chochote kuhusu hilo? Vipi suala la Ardhi wataendelea kuruhusiwa kujenga huko bara hawa watu au ndiyo basi tena? Maana sijaona kama Ardhi imeorodheshwa kama jambo la muungano.
 
Mwambieni Jussa atulie. Hao waarabu wake anaodhani watamsaidia kuendesha nchi angoje watampa hela. Ila nina wasi was Zanzibar baada ya kuvunjika muungano inaweza ikawa kama Somali
 
Mwambieni Jussa atulie. Hao waarabu wake anaodhani watamsaidia kuendesha nchi angoje watampa hela. Ila nina wasi was Zanzibar baada ya kuvunjika muungano inaweza ikawa kama Somali
Hata Kamandoo Salmin Amour alijipendekeza kwa Ghadaffi na kuahidiwa kila aina ya misaada, mwisho wake kunyang'anywa mke, na kapewa upofu ili atulie kabsaaa, ili makamanda wa muammar wapokee mabaki ya mzee na kuindelea kupekuwa. ndio utamaduni wao.
 
Mimi ni mtanganyika. Nimefuatilia mjadala huu kwa makini. Nimebaini kuwa watanganyika hawakujiandaa kuwa na serikali yao. Inashangaza sana kuona kuwa hata baada ya serikali ya tanganyika kuruhusiwa, bado watanganyika wengi wanaiwaza zanzibar. Huo ni udhaifu mkubwa. Kinachotakiwa kwa sasa watanganyika tuangalie namna ya serikali yetu itakavyoundwa kwa ufanisi. Zanzibar hawana shida sana kwa kuwa wana pa kuanzia. Sisi tunaanza sifuri. Tukiendeleza malumbano itadhihilika kuwa sisi watanganyika ndio tunaohitaji zaidi muungano huu. Ushahidi wa jambo hili ni katika jina lililopendekezwa. Tume imependekeza tanzania bara, kwa nini isiitwe tanganyika? Mbona zanzibar ipo?. Tunalichukia jina la nchi yetu?. Tupo kamili kweli?. Kwa nini tunaelekeza shutuma kwa wazanzibar badala ya kujikita katika kujenga tanganyika yetu. Tujirekebishe.
Uko sawa kabisa. Watanganyika hatujajiandaa. Na tatizo letu sio jina la nchi yetu. Tatizo letu ni kuwa bado tunaona fahari kuitwa Watanzania. Wengi wengi wetu tumezaliwa ktk Utanzania na sio utanganyika. Kimsingi wengi wetu hatukuwa tunalilia sana tanganyika ILA TUMECHOSHWA NA KELELE ZA WAZANZIBARI kiasi kwamba tunaona bora waende.Kimsingi kuanzishwa kwa serikali tatu ni kujibu mahitaji ya Wazanzibari, wengi wetu tulipenda serikali moja au kuvunjwa kwa muungano kabisa kila watu wachukue nchi yao kuepusha shari zaidi.Lakini katika ulimwengu wa leo na uchumi wa kisasa, muungano ni muhimu sana, ndio maana unaona USA, EU, Au, n.k. Hii yote ni mifumo mbalimbali ya muungano wa kisiasa au kiuchumi kwa viwango tofauti tifauti. Hii ni kuonyesha mwanadamu anafanikiwa zaidi katika umoja kuliko katika utengano. Tatizo kubwa la mwanadamu ni kuushinda ubinafsi wake, kiburi (egoism) na uroho wa madaraka. Hapa ndipo muungano wetu ulipokwamia na sasa tunaanza kupiga hatua kali zaidi kurudi nyuma (kwenye utengano) kuliko kwenda mbele. Siamini kama Watanganyika WANAIHITAJI serikali yao japo najua wapo WANAOITAKA!
 
Sijui kwanini wanawang'ang'ania hawa jamaa,wapewe chao tu.
 
Back
Top Bottom