Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...

Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...

chabuso,

..kabla NECTA[baraza la mitihani] haijaanzishwa, wanafunzi wa TANGANYIKA na ZANZIBAR walikuwa wanafanya mitihani ya EAST AFRICAN EXAMINATION COUNCIL.

..miaka ya nyuma zaidi wanafunzi walikuwa wakifanya mitihani ya CAMBRIDGE LOCAL EXAMINATION SYNDICATE.

..swali la kujiuliza ni kwanini Zanzibar haikuanzisha baraza lake la mitihani baada ya kujitoa kwenye East African Examination Council??

NB:

..Prof.Issa Shivji ni mzaliwa wa Kilosa, Tanganyika.

cc: KVM

Hiki kitu kinachoitwa EAST AFRICAN EXAMINATION COUNCIL hakikutumika Tanzania. Mitihani ya CAMBRIDGE LOCAL EXAMINATION SYNDICATE ilifanyika Tanzania kwa mara ya mwisho mwaka 1970. Mwaka 1971 ndipo mitihani ya Baraza la Mitihani Tanzania ndipo ilipoanza.
 
Siku hizi kila kitu kiko wazi ukitaka kujua wazanzibari wangapi walikuwa wamesoma kabla ya Mungano fanya utafiti.......kwaufupi Tanganyika ilikuwa nyuma sana kielimu kabla ya mungano huwezi kufanananisha na Zanzibar

Hayo unayoyasema siyo kweli. Kama unazo data leta ukumbini.
 
Hayo unayoyasema siyo kweli. Kama unazo data leta ukumbini.

Je unafahamu kuwa nchi ndogo kama Znz yenye wati wasiozidi milioni moja na nusa wana University 6. Je tanganyika yenye watu zaidi ya Milioni 40 kuna university ngapi?

Angalia vile vile namba ya graduates kwa mwaka kwa nchi hizo mbili kisha utajua hilo.

Pole sana
 
chabuso,

..kabla NECTA[baraza la mitihani] haijaanzishwa, wanafunzi wa TANGANYIKA na ZANZIBAR walikuwa wanafanya mitihani ya EAST AFRICAN EXAMINATION COUNCIL.

..miaka ya nyuma zaidi wanafunzi walikuwa wakifanya mitihani ya CAMBRIDGE LOCAL EXAMINATION SYNDICATE.

..swali la kujiuliza ni kwanini Zanzibar haikuanzisha baraza lake la mitihani baada ya kujitoa kwenye East African Examination Council??

NB:

..Prof.Issa Shivji ni mzaliwa wa Kilosa, Tanganyika.

cc: KVM

Joka kuu,

Naona haupo sahihi kabisa.

Kumbuka kuwa Tanganyika na Znz na nchi zote za East Afrika zilizokuwa chini ya Ukoloni wa Muingereza walikuwa wanafanya Mitihani ya CAMBRIDGE LOCAL EXAMINATION SYNDICATE nayo kwa upande wa Tanzania ilikoma mwaka 1970. na mwaka 1971 ndipo mitihani ya Baraza la Mitihani Tanzania ndipo ilipoanzishwa.

Naona umeteleza au imekupuruchuka mkuu.

Pole sana
 
Je unafahamu kuwa nchi ndogo kama Znz yenye wati wasiozidi milioni moja na nusa wana University 6. Je tanganyika yenye watu zaidi ya Milioni 40 kuna university ngapi?

Angalia vile vile namba ya graduates kwa mwaka kwa nchi hizo mbili kisha utajua hilo.

Pole sana

Hiki kinachokileta ni mada tofauti. Tulikuwa tunazungumzia mada kuwa Zanzibar kabla ya Muungano ilikuwa na wasomi wengi kuliko Tanganyika.

Vilevile imeleta swala la idadi ya wasomi ukilinganisha na idadi ya wananchi(per capita). Tunaweza kunyambua zaidi ya hapo tukatazama upande wa ubora wa elimu yenyewe, n.k.
 
Je unafahamu kuwa nchi ndogo kama Znz yenye wati wasiozidi milioni moja na nusa wana University 6. Je tanganyika yenye watu zaidi ya Milioni 40 kuna university ngapi?

Angalia vile vile namba ya graduates kwa mwaka kwa nchi hizo mbili kisha utajua hilo.

Pole sana

Hivi hizo ni university au madrasat?

NOTE:
Zanzibar kuna ILIMU na sio ELIMU.
 
Barubaru, KVM,

..asanteni kwa marekebisho kwamba wanafunzi wa Tanzania hawakupata kufanya mitihani ya East African Examination Council. nakiri kwamba niliteleza.

..pamoja na ningependa kufanya marekebisho kidogo kwamba NECTA ilianzishwa kisheria mwaka 1973. zaidi, kama mlivyoeleza mitihani ya Cambridge ilisita mwaka 1970. sasa labda tujaribu kuangalia btn 1970 na 1973 mitihani ilitungwa na chombo gani.

cc: Kichuguu, Augustine Moshi, NasDaz, Kitila Mkumbo
 
Takriban mambo yote yanayohusu shughuli zenye gharama kubwa za kila siku za nchi yametolewa katika muungano na kila serikali ya nchi mshirika (Tanganyika na Zanzibar) itaendesha mambo hayo yenyewe. Mambo ambayo bila shaka yanahitaji pesa nyingi katika kugharamia uendeshaji wake. Tanganyika ina uchumi mkubwa na hivyo ikitumia vyema uchumi wake pamoja na mapato yatokanayo na muungano inaweza kuendesha serikali yake ya Tanganyika na kumudu vyema ghrama za uendeshaji. Zanzibar kwa upande wake ina uchumi mdogo na vyanzo vichache vya uchumi ambvyo pia vina misingi tofauti na vile vya Tanganyika. Vyanzo hivi vinahitaji kuwekewa sera tofauti na zile za Tanganyika na pia political will isiyotegemea hisani au ridhaa ya Tanganyika.
Zanzibar inahitaji mamlaka kamili ili iweze kupanga sera zake na uchumi wake na hivyo kuweza kumudu gharama za mambo lukuki ambayo sasa hayatakuwa chini ya mwamvuli wa muungano.
Wajumbe wa Mabaraza ya katiba na wajumbe wa Bunge la katiba wajipange vyema tokea sasa kuhakikisha mambo yafuatayo yanatoka katika orodha ya mambo ya muungano ili kuipa nchi yetu ya Zanzibar mamlaka kamili ya kisiasa na kiuchumi na hivyo kumudu gharama za kuendesha shughuli zote za nchi. Mambo hayo ni:
1. Uraia na Uhamiaji
2. Sarafu na benki kuu
3. Mambo ya nje
4. Vyama vya siasa

Mchezo wowote mchafu wa kuchakachua sauti kubwa ya wazanzibari ya kudai mambo hayo 4 katika hatua mbili zijazo za mabaraza ya katiba na Bunge la katiba kama ilivyofanyika katika kuandaa rasimu ya katiba itatupa sababu muafaka wazanzibari ya kuipigia katiba mpya kura ya HAPANA kwa kuwa haitokani na matashi yetu na hivyo kuufelisha mchakato mzima.
https://www.facebook.com/photo.php?...00001430714596&type=1&relevant_count=1&ref=nf
 
Hayo unayoyasema siyo kweli. Kama unazo data leta ukumbini.
ingia kwenye google utapata data zote,search for Zanzibar before Union wakati zanzibar ina kiti UN,Tanganyika haijulikani
 
GHIBUU,

..majadiliano kuhusu mambo gani yawepo ktk muungano yalipaswa kuwa kati ya TGK na ZNZ.

..sijui kama unakumbuka hii ndiyo ilikuwa rai kuu ya mh.TUNDU LISSU.

..sijui kama unakumbuka matusi na dhihaka alizotupiwa mheshimiwa Lissu kwa kudai kwamba wa-TGK na sisi tupewe serikali yetu, kama ndugu zetu wa Znz mlivyo na serikali yenu.

cc: Nonda, Mdondoaji, Barubaru, Kibunango
 
Last edited by a moderator:
HUYU Jussa ni Mliberali kabisa
263307_638921402803820_1706461455_n.jpg
 
Wazanzibari washakwambieni wao wanataka MAMLAKA KAMIL, maana yake wao wanataka nchi yao, na nyinyi mchukuwe nchi yenu, ili tugawane mbao.
 
Tatizo la hawa WANGUNYA ni kutotaka kusema UKWELI.

Semeni kwa SAUTI MMOJA kwamba HAMUTAKI MUUNGANO full stop. Hii ya kuzunguka mbuyu haitawasaidia.

Sasa mkitoa hayo mambo 4 yakabaki mambo 3 tu ya MUUNGANO utakuwa tena huo ni MUUNGANO?!
 
Sasa ukiyatoa hayo kuna muungano tena? semeni hamtaki muungano mtaeleweka!
Mungano ni makubaliano ya nchi mbili Huru,nchi za scandinavia zimeungana lakini kila nchi ina mamlaka kamili,makubaliano makubwa ambayo yanatakiwa yawepo ni ulinzi,biashara,maingiliano ya raia(mouvement of People)
 
Mbona jeshi la wananchi haorodheshi?

Bado hawajapata majambia ya kutosha kujilinda.Unajua hawa jamaa ni kama changudoa wakati wote anapiga kelele kutetea maslahi yake kwa jicho moja bila kujua kuna gharama upande mwingine ata kama ulimnunulia pombe na chakula kabla ya kuanza kuchachuana.Waache waende makwao watuondolee na mkata viuno wa taarabu HADIJA MAKOPA
 
ingia kwenye google utapata data zote,search for Zanzibar before Union wakati zanzibar ina kiti UN,Tanganyika haijulikani
chabuso,

..TANGANYIKA tulipata uhuru December 9, 1961.

..ZANZIBAR ilipata uhuru wa bandia December 10, 1963.

..TANGANYIKA ilipata uanachama wa UN December 14, 1961.

..ZANZIBAR ilipata uanachama wa UN December 16, 1963.

..TANZANIA ilipata uanachama wa UN November 1, 1964.

..hayo yote niliyoandika nimeyapata hukohuko kwenye google.

cc: Nguruvi3, Nonda, Barubaru, KVM, Kibunango, GHIBUU
 
hahaha hizo data zako source Yake wapi,mpaka hii Leo nchi inayoitwa Tanzania inatumia kiti kilichokuwa cha Zanzibar UN,uhuru bandia hizo ni stori za kipropaganda mbona aliekuwa waziri mkuu wa mwanzo zanzibar alikuwa mpemba Kama sikosei,Sultan alikimbilia Tanganyika halafu uingereza na anaishi mpaka Leo Portmouth,hakukimbilia Oman kwasababu alikuwa raia wa zanzibar sio wa Oman,ndio maana UK walimpa hifadhi ya kisisasa
 
Back
Top Bottom