Alichokisema Rais Magufuli Tabora ni kweli; majungu watu hawafanyi kazi. Kanisa lajengwa katikati ya barabara, lapiga muziki masaa 24

Kwa kweli imani zingine ni kero wengine sijui ni ulimbukenii,naamini ibada ina mda wake,sio unafungulia mziki Kwa sauti Kwa ajili ya kuwasikilizisha wengine, bila kujali kuna wagonjwa n.k
Kuna chombo kinakula fedha za serikali kwa kutotimiza wajibu wake, huwa sielewi kwanini hakiwajibishwi "NEMC"
 
Hilo kanisa mbona lipo miaka mingi sana au nimekosea location ?
 
Hilo kanisa mbona lipo miaka mingi sana au nimekosea location ?
Hapana , hilo kanisa lilikuwa Mwanga Shop kata ya Cheyo wakafukuzwa kwa wehu wao. Ndio wakamia hapo . Mleta mada Ni mkweli kabisa happy Kuna makanisa mbali kidogo la Efata , Moravian na lingine jirani na Westland school yote haya hayana tatizo ni wastaarabu wana muziki wanafungulia taratibu bila shida isipokuwa hawa vichaa ni vichaa kabisaaa , maajabu serikali kuruhusu vichaa kuongeza mambo ya ndoa , kumuandaa mwanamke kabla ya tendo huku spika zikiwa wazi kwa sauti kubwa .
 
Yeah nafikir la EFATA ndiyo lina muda mrefu kuliko hayo mengine.
Wayback 2010 hilo la karibu na Westland ndiyo walikuwa anajenga
 
watu wamesogezewa huduma ya injili hapo
 
watu wamesogezewa huduma ya injili hapo
Hapo hakuna injili , Kuna vichaa na wajasilia dini tupu tena wehu kasoro kuvua nguo .Injili ndio unasema ufundishe jinsi ya kumuandaa mwanamke kabla ya tendo spika zikiwa wazi , watoto chini ya miaka kumi na nane 18 wakiwa wanasikia wa ndani na n'nje hilo wanaloita kanisa lao . Kupiga muziki kama wehu kwa sauti ya juu ndio injili ? Kuathiri majirani , wagonjwa , wazee, watoto ndio injili ? Injiliya wapi ? Ya nani ? Maana maandiko yako wazi soma 6:5 Mathayo Tena msalipo msiwe Kama wale wanafiki wanaotaka kuonekana na watu .
 
Nikuambie kitu?

Tatizo linaanzia kwa Mwenyekiti wa Mtaa. Wananchi mpaka wanaandika barua kwa Mkurugenzi ambapo shughuli hiyo ni ndogo sana kwa Mwenyekiti wa Mtaa ni wazi kuna tatizo kubwa kwenye ngazi hiyo
Mwenyekiti wa mtaa Ni empty set na njaa kali .
 
Majirani hapo pia wanaweza kuwasha moto juu ya moto.Mikesha ya vigodolo na miziki ya kutosha kwa mwezi mfululizo.
Huo mtaa unageuka pahala pa burudani za kidunia na Heaven.

Ukitaka kujua ubaya wa maeneo kama hayo uwe na Mtoto au mgonjwa utelewa hayo mahubiri na huo mziki jinsi unavyoumiza.

Nina ushahidi mdogo sana miaka ya 2014 Mahala flani Moro..kuna jirani alisumbua sana wenzake na Midundo mizito zaidi ya hiyo.

Basi miaka ile kila mtu aliiweka Serikali mfukoni.
Nyumba moja ilijichanga ukaletwa mzigo wenye watts za kutosha.Ukapigwa masaa 24.Ukipata joto huu unawashwa huu.
Mpaka leo mtaa ule huwezi washa mziki wa aina yoyote ile kwa sauti mana pana Historia hiyo.Kuwa wewe washa utakodishwa ambao utakaa karibu yako bila kuchoka.
Tena kuna ngoma kali sana za Kibongo..mkito mkito..Unapigwa mziki mpaka viumbe vya ardhini vinakuja juu.
Kuabudu na kusifu bila kujali mazingira yanayozunguka.Ni unafiki wa hali ya juu kabisa na ni roho mbaya mno sio Upendo huo.
 
Kuna matatizo mengi sana mengine ukifuata taratibu za kiubinadamu basi utachelewa.
Niliwahi kuumwa sana nikatoka Hospital kuugulia nyumbani , jirani yangu hakuwa anajali.Ni kelel na mziki mkali.Ikanilazimu kumdadisi jirani anatumia chombo ipi.
Huku tunachekeana nilikuja kuleta chombo mara 3 ya alicho nacho..sasa kuna amani na utulivu pia.
Mana napenda mziki..kuna mida flani unajua huu watu wamechoka unawasha sasa kutuma salamu kuwa your not alone.
Tutavunja hizi kutaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Maisha sasa yapo poa kabisa..unyonge unyonge wa kwenye Serikali za mitaa haupo tena.
Tunavyo visa vingi sana..vya namna hiyo..
 
Majirani wa hapo kwa kuwa wanajua tatizo.Wanaweza anzisha nao kanisa lao la Praise and Worship..Hapo mnatafuta Pastor wenu analipwa unapigwa mziki na kuomba mpaka Malaika mbinguni wanasema naaam.

Maana si watu wameamua fujo...ya nini kulia lia.
Vijana wapo na hzi kazi wanaziweza hapa mjini.
Unyonge upungue...
 
Usiwaite vichaa watumishi wa Mungu aliye hai. Utapigwa na Mungu. Usitafute sifa humu JF. shauri yako.
 
Kuna watu kadhaa hapo wanapaswa kuwajibishwa
1.
Mtendaji wa mtaa (yeye ni mlinzi wa amani wa mtaa)

2.
Mwenyekiti wa Mtaa (mwenyekiti wa ulinzi na usalama mtaa)

3.
Mtendaji wa Kata (mwenyekiti wa ulinzi na usalama Kata)

4.
OCS (katibu ulinzi na usalama Kata)

5.
DAS (Katibu wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya)

Wakibanwa hao utaona matokeo kabla hakujapambazuka
 
Jumapili ndio kivumbi na jasho wanaanza muziki was hatari saa moja asubuhi mpaka saa kumi na moja nonstop .
πŸ˜‚πŸ˜‚ sasa mbna unasema ni 24 hrs kumbe saa 1 mpaka 11πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Usiwaite vichaa watumishi wa Mungu aliye hai. Utapigwa na Mungu. Usitafute sifa humu JF. shauri yako.
Mkuu hao ni vichaa kabisaaa na ni watumishi wa ibilisi sio Mungu . Mungu hawezi kutuma watu waende kuwa kero kwa wengine , waende kutesa wagonjwa , wazee , watoto ambao ni majirani kwa upumbafu wao wa kupiga muziki kiendawazimu. Ukiona mambo yamefika humu ujue moto umekolea umebakiza kulipuka tu . Wehu wao huu hapa 1. Kupiga muziki kwa sauti kubwa sana ? Kutoa mahubiri ya ndoa kuandaa mwanamke mbele ya watoto na spika zikiwa wazi .3. Walipohamia kutoka cheyo walikofukuzwa , hawakuwa na choo hapo walikuwa wanavamia vyoo vya majirani bila kuomba 4. Walikuwa wanavamia visima vya majirani kuteka maji . 5. Walipojenga choo wakawa wanachukua ndoo zao za chooni wanadumbukiza kwenye visima vya majirani kuteka maji . Hawa wehu ndio wamuombe Mungu anidhulu ? Masihara .
 
Mkuu na sisi tunataka tununue vyombo vyenye uwezo mara kumi yake ili wakianza tu muziki wao na sisi tunafungulia mpaka mwisho ndio serikali itaelewa ?
 
Hao wote taarifa wanazo ila hawataki kuchukua hatua .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…