Nikiwa Tabora ambapo nilikwenda kwenye msiba wa rafiki yangu aliyefiwa na mama yake mwezi huu. Nilikutana na kituko cha mwaka ambapo tukiwa hapo msibani ulisikika muziki mkubwa sana kiasi ambacho huwezi kuongea na mtu jirani yako, huwezi kupokea simu au kusikiliza simu. Nilipouliza nikaambiwa hilo ni kanisa la walokole Bethel, ambao walifukuzwa kutoka kata ya cheyo ndio wamehamia Kariakoo Tabora kata ya Kitete, ambapo toka wahamie Muziki ni masaa 24 kwa sauti ya juu sana.
Wakazi wa eneo hilo licha ya kulalamika kwa mkuu wa wilaya kwa maandishi DC Komanya, mkurugenzi, mtendaji kata, mwenyekiti wa mtaa, polisi mkuu wa kituo Mmassy, OCD, bado kanisa hilo linaendelea na fujo, vurugu huku mchungaji wa kanisa hilo Mch Jackson akiwambia wakazi hao kuwa serikali yote ya mkoa ameiweka mfukoni.
Mbaya zaidi huyo kaamua kujenga katikati ya barabara na kuziba barabara mtaa hivyo hapapitiki kwa gari, huwezi kupitisha mgonjwa, maiti hata kwa matumizi ya kawaida.
Jirani na kariakoo Ni eneo la Tukutuku ambapo nyumba zaidi ya Mia zilivunjwa kwa kujengwa maeneo yasiyoruhusiwa na bila kibali cha manispaa. Kanisa hilo linajengwa katikati ya barabara bila kibali? Au ndio afisa mipango miji katoa kibali Cha kujenga katikati ya barabara be? Haya yanafanyika huku Mkuu wa Mkoa yupo, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkurugenzi yupo, Afisa Mipango Miji yupo na taarifa za malalamiko wanazo au ndiyo ukweli wa maneno ya rais Magufuri kuwa Tabora wamekalia majungu hawafanyi kazi?
NB: Kanisa na nyumba ya mchungaji vimejengwa kuziba barabara. Muziki mkubwa kanisani waliomo ndani sasa hata kumi hawafikiriki.
View attachment 1701280