The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Ninaye rafiki yangu anayesoma China ambaye yupo huko takribani miaka 3 sasa. Nilipojaribu kumuuliza kuhusu namna serikali ya China inavyofanya kuhamasisha raia wake kuchanja chanjo ya Covid, au kuhakikisha kila raia wake amechanja ili kujikinga na corona.
Yule rafiki yangu ameniambia serikali ya China imetengeneza chanjo na kuiweka kwenye vituo vya Kutolea huduma alafu raia yeyote anayetaka kuchanja aende mwenyewe kwa hiyari yake.
Wala huwezi kukuta afisa au kiongozi wa serikali akisisitizia watu kuchanja. Alichoniambia ni kwamba mkazo mkubwa wamewekeza kwenye kinga. Inavyoonekana wamepuuza kwa kiasi mambo ya chanjo.
Sasa najiuliza huku ndiko corona ilikoanzia, wao wameendelea sana kiteknolojia kuliko sisi, iweje sisi tusisitize suala la chanjo kiwango cha kutaka kulazimishana wakati wazalisha chanjo hawajafikia huko?
Ni kwa nini tunajilazimisha kuchukua chanjo zao hali ya kuwa hata wenye chanjo wenyewe hawaziamini kiwango hiki?
Ni kwa nini serikali yetu inatumia nguvu kubwa sana, ukizingatia alinidokeza nesi mmoja kwamba wamepewa kila mtu kuchanja watu hamsini kwa siku?