#COVID19 Alichonihadithia jamaa yangu anayesoma China kuhusu chanjo ya COVID-19, kimenistua

#COVID19 Alichonihadithia jamaa yangu anayesoma China kuhusu chanjo ya COVID-19, kimenistua

Mtoa mada amechemka 😀😀🤣🤣🤣 Hivi KINGA si ndio CHANJO. Chanjo ni kinga sio dawa. Omg watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Na hakuna nchi inayolazimisha ila kutafika siku bila kua na chanjo hupati huduma yoyote.
 
Kaniambia kule ukiingia huulizwi chanjo ila unapimwa kama umeambukizwa hiyo tu inatosha na sio raia toka nje tuu bali hata wao ukitoka jimbo moja kwenda kingine sharti muhimu sio chanjo ila ni kupimwa ikiwa una maambukizi
na ni sawa tu kwa kweli, huku pia hatulazimishwi kuchanja na ukiingia lazima upime
 
Umedanganywa. Uchina wanavamia nyumba moja baada ya nyingine kuwachanja watu kwa lazima kama mifugo. Hahaha. Hata ukifika airport zao unapimwa damu kuona kama una vimelea vya chanjo. Kama huna utawekwa isolation kwa muda wa wiki 2, kisha utachanjwa kwa lazima. Hata Ukikataa unapewa dawa za usingizi kisha unachanjwa ukiwa huna fahamu.

Salama yako ni kubakia huku huku bongo au ukiweza ukanunue cheti cha kuzugia.
 
Hata Bongo mbona ni hiari tu, watu wanahamasishwa tu kuchanja ila hatulazimishwi kuchanja.
Siyo kweli, mfano mdogo ni mgodi wa GGML kama huna chanjo uwe mfanyakazi au familia ayeishi nyumba za ndani ya mgodi, mzabuni au unaenda kikazi huruhusiwi kuingia

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, huko vijini sasa hivi Serikali ya Tanzania inachanja watu kwa nguvu, mama akipeleka mtoto kliniki hapati huduma hadi mama achanjwe chanjo ya Corona.
Ni kweli Mkuu, mm mkewangu aliwakatalia , akawaambia kama hamtaki kumuhudumia mtoto mpk chanjo ya COVID-19 muweke bango wananchi wote wajue. Mwisho wa siku hakuchanja na mtoto akahudumiwa vzr
 
Ninaye rafiki yangu anayesoma China ambaye yupo huko takribani miaka 3 sasa. Nilipojaribu kumuuliza kuhusu namna serikali ya China inavyofanya kuhamasisha raia wake kuchanja chanjo ya Covid, au kuhakikisha kila raia wake amechanja ili kujikinga na corona.

Yule rafiki yangu ameniambia serikali ya China imetengeneza chanjo na kuiweka kwenye vituo vya Kutolea huduma alafu raia yeyote anayetaka kuchanja aende mwenyewe kwa hiyari yake.

Wala huwezi kukuta afisa au kiongozi wa serikali akisisitizia watu kuchanja. Alichoniambia ni kwamba mkazo mkubwa wamewekeza kwenye kinga. Inavyoonekana wamepuuza kwa kiasi mambo ya chanjo.

Sasa najiuliza huku ndiko corona ilikoanzia, wao wameendelea sana kiteknolojia kuliko sisi, iweje sisi tusisitize suala la chanjo kiwango cha kutaka kulazimishana wakati wazalisha chanjo hawajafikia huko?

Ni kwa nini tunajilazimisha kuchukua chanjo zao hali ya kuwa hata wenye chanjo wenyewe hawaziamini kiwango hiki?

Ni kwa nini serikali yetu inatumia nguvu kubwa sana, ukizingatia alinidokeza nesi mmoja kwamba wamepewa kila mtu kuchanja watu hamsini kwa siku?
Duh!! hizi habari hizi....
Huna haja ya kufanya kampeni maana ugonjwa wenyewe unapungua..
 
Mimi mpaka leo naendelea kumheshimu Hayati JPM pamoja na kwamba amelala! Kwa mfano sasa hivi naona kama sijawahi kusikia Corona.
 
Ikifika chanjo ya ukimwi, je mtaipinga kama mnavyoipinga ya Covid? Nawaulizeni wazinzi je mtaipinga?
Kwahiyo una maanisha corona si hatari kama ukimwi ndio maana watu wanaweza kugomea chanjo za corona?
 
Siyo kweli, mfano mdogo ni mgodi wa GGML kama huna chanjo uwe mfanyakazi au familia ayeishi nyumba za ndani ya mgodi, mzabuni au unaenda kikazi huruhusiwi kuingia

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
Hizo ni taasisi binafsi na zina utaratibu binafsi katika utendaji wao wa kazi. Hata huko China kwenye hotels na baadhi ya taasisi binafsi kuna ulazima wa kuchanja.

Ila kwa serikali sio lazima jukumu lao ni kukuwekea mazingira ya wewe ukitaka kuchanja upate chanjo.
 
Je wawekezaji wakubwa duniani watapaje faida ikiwa shairi la EAT MORE halitaimbwa kwa sauti za juu?
 
Ipo hivi,
Serikali yetu inatumia nguvu kubwa sana, ukizingatia kuna nesi mmoja alinidokeza kwamba wamepewa kila mtu kuchanja watu hamsini kwa siku na ukweli ni kwamba, waliochanja wanawaonea wivu wasiochanja, kwamba kama kuna madhara kwny chanjo basi wanataka tuyapate wote.
 
Mkuu kwanini uhangaike? Wewe kama hujisikii kuchanja acha tu endelea na mambo mengine, waache wanaotaka kuchanja. Huna haja kuhangaisha nafsi yako

We si unamuamini rafiki yako allyeko China? Inatosha mkuu, achana na mambo ya chanjo we endelea na mengine tu
Kweli kbs ache kutupa habari za uongo china chanjo mpk watoto wanachoma, na wamechoma kuliko huku Tanzania, akili za kuambiwa changanya na zako..
 
Hii kiki ya chanjo ya uviko ni kwa minajili ya kupata ile trilioni 1.3 ya mabeberu.........hayo mengine hayana maana.
 
Kwani kwa Tanzania ni lazima kuchanja,au kuna raia aliyenyimwa huduma ya umma kwa kutopata chanjo? kwa utafiti wako ukitaka chanjwa au laah,maisha yaendelee!
 
Back
Top Bottom