Niaje wadau.
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu Alikiba kupokonywa ushindi huko MTV EMA.Naomba hapa nitumie nafasi hii kufafanua kilichotokea ili kuweza kuondoa huu utata.
Kwa mujibu wa Mtv Ema Alikiba ameshinda kwa kura nyingi sana alizopigiwa na mashabiki na wamemtangaza kuwa katika kipengele cha kura nyingi Ali ndio mshindi.
Naomba tufahamu kwamba Tuzo kubwa kama MTV EMA na BET kuna vipengele ambavyo maamuzi yake hayategemei kura za mashabiki bali huamuliwa na wadhamini, majaji pamoja na waandaaji wa Tuzo. Kipengele hiki huangaliwa ni kiasi gani msanii anafanya vizuri katika category aliyowekwa cz inawezekana msanii akakosa kura nyingi lakini anastaili kupata tuzo kutokana na mchango wake katika mziki.
Kipengele hicho ndicho kilichomfanya Wizzy ashinde Tuzo hiyo ya MTV EMA.
Kiukweli MTV EMA hawajakosea katika hilo cz watanzania wengi walimpigia kura Kiba bila kujali team zao lakini kwa viwango vya kimataifa kiba hawezi kumfikia hata Robo Wizkid.
Alikiba alitakiwa kuwaambia ukweli mashabiki zake na sio kulalamika kwenye media kuwa haelewi kilichotokea wakati anafahamu ukweli wote. Kulalamika kwa Ali kutamsababishia picha mbaya na sidhani kama MTV EMA watakuja tena kumchagua kuwania Tuzo hizo katika Category yoyote ile.
Natumaini nimeeleweka japo kwa uchache.
Jana Asubuhi
Ukiingia ktk website ya MTVEMA ukiclick winners, Alikiba ndiye aliyeonekana Mshindi, Mwenye ICON ya kushinda.
Ishu ikaja mbona alikiba anaonekana kashinda, au yupo ktk list ya winners kwa nini hajapewa??? Wakati wenzie wote walipewa?? Hilo ndilo lililoleta usumbufu kwa Mashabiki, na hata sasa ukiingia website yao MTVEMA ni Kipengele cha BEST AFRICAN ACT tu ndiyo kinaonekana hakina Mshindi, Vyote vilivyobaki vina Mshindi.
Kwa Kumbukumbu nzuri, Alikiba alishinda wale MTVEMA wakashangaa imekuwaje kashinda wakati hata MTVMAMA hakupata hata mmoja??? wakawauliza MTVBASE/MTVMAMA kuhusu ushindi huo, hapo ikabidi MTVMAMA waseme anayestahili kuwa BEST WORLD WIDE ACT NI WIZKID, Lakini tatizo likaja Wiz hawezi kupata hiyo mpaka awe ameshinda BEST AFRICA ACT, Ndiyo hapo unakuja kukutana na WAAFRIKA KUITWA NYANI, MTVBASE wakajifanya kimbelembele kumtangaza wiz kid ili kujua RESPONSE YA WATU IKO VIPI, Wakasahau Mtandao wa MTVEMA upo AUTOMATIC unaonesha nani kashinda, wakampa jamaa TUZO, wakati watu wakitazama aliyeshinda na KIBA, Uswahili ukaanzia hapo!!!
Mpaka sasa MTVEMA hawajaeleweka, na MILLARD AYO wakati anaposti ktk Mtandao wake alijua kabisa, ktk ile list ikabidi asiripoti kipengele cha Best African Act kwa sababu kilikuwa kinamwonesha ALIKIBA Mshindi wakati MTVBASE walishamtangaza wizkid. Hii ni Scandal kwa MTVEMA iliyosababishwa na MTVBASE.
Nimechukia sana namna watu wanavyomzarau Alikiba,
Me nataka niwaambieni kitu washkaji, kama umesoma probability, utaelewa Both artist have equal chance of winning, The issue was VOTING.
Kusoma UDOM, Mzumbe, UDSM, SAUT, HARVAD, MAKERERE au popote, Tunapokutana ktk Interview ina maana UDOM akifanya Vizuri kuliko harvad ndiyo tumwache??? Au Mzumbe kafanya Vizuri kuliko UDSM tumwache?? Tumchukue HARVAD kwa vile ni wa kimataifa??? This is non-sense.
SIKU WAAFRIKA MKIACHA KUJIDHARAU WAZUNGU HAWANA CHA KUWARINGISHIA.
I HATE THAT HATE.