kulagha nenga
JF-Expert Member
- Jan 1, 2026
- 690
- 1,375
Kadi unampa liniMnaopenda gutter politics lazma mtaumiza mioyo yenu tu bure. Mh.Mbowe anajua maana halisi ya uongozi,upinzani na siasa kuliko wengi asa upande wa upinzani. Kinacho kosekana kwa sasa ndani ya CHADEMA hamna mtu mwenye hulka ya hivyo. Pamoja na yote Mh.Mbowe akuwai kuwataka wananchi na wafuasi wa CHADEMA waichome nchi...UKWELI NI KUA LISSU atoshi kwenye siasa zenye ustaarabu na utaifa..Kinachowagharim ndiyo hicho
Kadi ya nini wakati yeye ndiye katufanya tuijue CHADEMA na kua wanachama watiifu kuliko huyu mvurugajiKadi unampa lini
Hivi kamanda tulishiriki uchaguzi? Vipi walio shiriki wanasema je? KARIBU KAMANDAAmani si kuwa mjinga, kama ni wapinzani kuuwawa wameuwawa sana, acha ukatili waliofanyiwa ili ccm ibakie madarakani kwa shuruti. Ni amani ipi unaongelea labda? Ni wapi unaweza kusema zimetokea kura 31m wakati hakukuwa na idadi hiyo ya wapiga kura? Mnadhani kila mtu atakalia kimya uovu wenu kwa kulinda amani fake ya kuburuzwa na ccm?
Mzee Mimi sio mtu WA siasa ila unakosea sana ila. Huwzi jua kuwa unachokosea, pili huzijui siasa, Yaani umesahai mbowe alikuwa na kesi ya ugaidiNdugu ,you have nailed it... Mbowe ni mwanasiasa halisi sio mwanaharakati kwa aslimia ata 20% .Waliochukua chama kwasasa wao ni harakati,payuka,tukana,beza nk.. CHADEMA kwasasa aiwezi kufanya operation yenye maana kama enzi za Mbowe-OPERATION SANGARA
Sijui kama unasoma na kuelewa kilicho andikwa,pia hongera kwa kuzijua siasa. GOODMzee Mimi sio mtu WA siasa ila unakosea sana ila. Huwzi jua kuwa unachokosea, pili huzijui siasa, Yaani umesahai mbowe alikuwa na kesi ya ugaidi
Kamanda,hivi kufunguliwa kesi maana yake tayari umekutwa na hatia? Ata kamanda Lissu anaweza kutoka asipokutwa guilty..kuna shida gani hapo?Aliwahi kusimama na kusema ccm mpore chaguzi za nchi hii na kufanya mauaji. Kama haijawahi kusimama na kusema mchome nchi hii, kesi ya ugaidi mlibambikia ya nini?
Wanataka kumpa kadi na uteuzi WA ubungeMnavyompamba Mbowe, kipi cha maana alifanya kwenye Upinzani? Tutoleeni udalali hapa.
Lengo zima sini kuvuruga uchaguzi na kuhamasisha uasi au? Hivi kwani tume huru imeandikwa kua italetwa kwa kuvuruga uchaguzi na kufanya uasi? Lissu sio malaika ni mwanadamu kama mimi na wewe kwahiyo anaweza nae kukosea au kuteleza.Na yeye ameshasema ili mwelewe kauli zake na sio kuchukua kipande cha vídeo kisichozidi dakika moja. Elewa lengo zima ndio utafahamu,
Ni takataka, zaman sana walishasema yuko kwenye payroll ya chama, ni mtu mbaya sana, anajifanya yuko na sisi kimbe anatunafkia, nina wasiwasi hata inshu ya mwenyekiti kuchapwa shaba anajua…Huyu mzee ukute hata alikua analala ikuluuu
HaswaaaUNAFIKIRI KUMVUA UANACHAMA MH.MBOWE ITAMCOST KWELI?
Mbowe bado ana wafuasi wengi ndani ya Chadema. Akirudi tu kwenye siasa wataungana nae. Chadema ya Mbowe ilipambana kuliko ya hivi sasa. Na wengi wanakumbuka hilo...mazingira ya Mbowe kurudi kwenye siasa yanazidi kuwa magumu kama moderates hawana nafasi ktk political space.
Mbowe hapendwi na CCM. Wanamkumbatia ili kumharibia machoni mwa Chadema. Wanajua..siasa zinazoendelea sasa hivi hazina " afya " kwa Mbowe, wala Lissu. Na asitokee mmoja wao akajiona yeye ana afadhali machoni mwa Ccm.
Mbowe bado ana wafuasi wengi ndani ya Chadema. Akirudi tu kwenye siasa wataungana nae. Chadema ya Mbowe ilipambana kuliko ya hivi sasa. Na wengi wanakumbuka hilo.
Mbowe hapendwi na CCM. Wanamkumbatia ili kumharibia machoni mwa Chadema. Wanajua
ana uwezo wa kukijenga chama chake na kuibua watu wenye uwezo mkubwa. Chadema ya Lissu ni one trick pony. Sasa hivi wameelekeza nguvu zao karibu ya zote kwenye kesi ya Lissu. Wakati wa kesi ya Mbowe, Chadema iliendeleza mpambano nje ya Mahakama. Ingawa wanaharakati na wanamtandao walimpigania sana lakini hawakuwa peke yao.
Bawacha, Bavita, Bazecha waliendelea kumpigania na kukipigania chama bila uoga. Waliwekwa ndani lakini kesho yake walikuwa mtaani.
Amandla...
Mbowe kaondoka lini Chadema? Hayuko active ( tunavyoona) lakini bado ni mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya Chadema. Hiyo nafasi hawezi kunyang'anywa na mtu yeyote...Mbowe akirudi Chadema na yeye ataundiwa kesi mbaya ili awe jela asikijenge chama.
..tunafanya makosa kufikiri kwamba tatizo ni Mbowe, Lissu, au Chadema. Tatizo ni siasa zetu ni Ccm ambao wanatumia vyombo vya dola, na mahakama, kukandamiza wapinzani.
Mbowe kaondoka lini Chadema? Hayuko active ( tunavyoona) lakini bado ni mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya Chadema. Hiyo nafasi hawezi kunyang'anywa na mtu yeyote.
Nadhani CCM ina mchango mkubwa katika matatizo yetu lakini naamini wapinzani nao wanachangia. Wangeweza kushirikiana wangeipa shida sana CCM. Kwa mtazamo wangu Chadema inabidi ibebe lawama kubwa kwa kutaka vyama vyote vya upinzani vikisujudie.
Chadema wanapambana kwa guvu zaidi na ACT-WAZALENDO na Chaumma kuliko wanavyofanya na CCM. Hauwezi kutegemea ushirikiano kwa kuwaita wengine CCM B na kujinadi kuwa wewe peke yako ndio mpinzani wa kweli.
Amandla...
Ndio maana sikusema Chadema ya Lissu. Mbowe amehusika katika kudhoofisha ushirikiano uliokuwepo baina ya vyama wakati wa Ukawa. Hakwepi lawama kwenye hili...mikwaruzano ya Chadema na ACT ilikuwepo wakati Mbowe ni Mwenyekiti.
Wakati wa Mbowe Chaumma kilionekana inconsequantial na hivyo beneath the attention ya Chadema. Chadema kimeelekeza chuki yake kwa Chaumma baada ya baadhi ya wanachama muhimu kuhamia huko baada ya kutofautiano mtizamo na wakina Lissu. Unachoita mikwaruzano ni mostly Chadema ikikiandama Chaumma. Mwanachama pekee wa Chaumma mwenye vendetta na Chadema ni Yericko Nyerere...mikwaruzano ya Chadema na Chaumma imeibuka wakati huu wa Tundu Lissu mwenyekiti.
Inawezekana kuwa nimetia chumvi lakini katika kampeni za uchaguzi wa 2025 Chadema ilikuwa mbele kuvuruga kampeni za wagombea wa Chaumma kama Catherine Ruge. Makamu Mwenyekiti ametumia lugha isiyopendeza kuwashambulia wakina Suzan na Sigrada. Kwa upande wa ACT ndio usiseme. Viongozi wa Chadema wanapo pambana na CCM hawatumii lugha binafsi kama wanavyotumia dhidi ya Chaumma na ACT...sikubaliani na wewe unaposema Chadema wanapambana zaidi na ACT, au Chaumma, kuliko Ccm.
Hizo ni policy issues na mara nyingi Chadema inazitumia kuaminisha kuwa Chaumma na ACT ni vibaraka kwa vile tu katika hizo hawakubaliani tu na NRNE...Kwa mfano, hoja kuu za Chadema ni NRNE,Tume Huru, na Katiba Mpya. Hoja hizo zinashambulia zaidi watawala kuliko ACT,au Chaumma.
Nakubaliana na wewe. Lakini hilo linakuwa ngumu kama chama kikuu kinajiona kuwa peke yake ndie mpinzani na vingine ni vibaraka. Chama kikuu cha upinzani kinatakiwa kuwa na vyama vingine katika hili na sio kutumika katika kuvikatisha tamaa. Najua kuwa katika upinzani kuna vyama ambavyo vinakubali kutumiwa lakini sio vyote. Vinakuwepo vyama vingi vya upinzani vitakipa chama tawala ugumu inapotaka kuvishughulikia...kwa upande mwingine vyama vya upinzani viwe macho na mitego ya Ccm kuvichonganisha. Nadhani kwa yaliyotokea ktk chaguzi za 2019 mpaka 2025 vyama vya upinzani vitakuwa vimejiridhisha pasina shaka kwamba Ccm ndio adui yao namba moja.
.
Ndio maana sikusema Chadema ya Lissu. Mbowe amehusika katika kudhoofisha ushirikiano uliokuwepo baina ya vyama wakati wa Ukawa. Hakwepi lawama kwenye hili.
Wakati wa Mbowe Chaumma kilionekana inconsequantial na hivyo beneath the attention ya Chadema. Chadema kimeelekeza chuki yake kwa Chaumma baada ya baadhi ya wanachama muhimu kuhamia huko baada ya kutofautiano mtizamo na wakina Lissu. Unachoita mikwaruzano ni mostly Chadema ikikiandama Chaumma. Mwanachama pekee wa Chaumma mwenye vendetta na Chadema ni Yericko Nyerere.
Inawezekana kuwa nimetia chumvi lakini katika kampeni za uchaguzi wa 2025 Chadema ilikuwa mbele kuvuruga kampeni za wagombea wa Chaumma kama Catherine Ruge. Makamu Mwenyekiti ametumia lugha isiyopendeza kuwashambulia wakina Suzan na Sigrada. Kwa upande wa ACT ndio usiseme. Viongozi wa Chadema wanapo pambana na CCM hawatumii lugha binafsi kama wanavyotumia dhidi ya Chaumma na ACT.
Hizo ni policy issues na mara nyingi Chadema inazitumia kuaminisha kuwa Chaumma na ACT ni vibaraka kwa vile tu katika hizo hawakubaliani tu na NRNE.
Nakubaliana na wewe. Lakini hilo linakuwa ngumu kama chama kikuu kinajiona kuwa peke yake ndie mpinzani na vingine ni vibaraka. Chama kikuu cha upinzani kinatakiwa kuwa na vyama vingine katika hili na sio kutumika katika kuvikatisha tamaa. Najua kuwa katika upinzani kuna vyama ambavyo vinakubali kutumiwa lakini sio vyote. Vinakuwepo vyama vingi vya upinzani vitakipa chama tawala ugumu inapotaka kuvishughulikia.
Amandla...
Kuna vyama kweli ambavyo vinaona kuwa wajibu wao ni kuwa upande wa CCM. Lakini viko ambavyo havioni shida kutofautiana na Chadema. Kutofautiana sio kupambana...kuna ukweli kwa unayoyasema.
..lakini utakubaliana na mimi, kuna vyama vya upinzani, wakati fulani vinajisahau, na kuanza kupambana na Chadema, badala ya kupambana na Ccm.
Kutofautiana ni sehemu ya siasa. Ni hili la kuona kuwa ni wajibu wa vyama vya upinzani kuunga mkono kila hoja ya Chadema ndio unaleta matatizo. Hasa ukiangalia kuwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani walitoka Chadema baada ya kutofautiana na mwenendo wa Chadema na hata sera zake. Viongozi wengi wa Chaumma walitoka Chadema kwa sababu walikuwa na tatizo na utekelezaji wa NRNE. Walipoona hamna muafaka wakajitoa. Na hilo sio dhambi. Dhambi ni kusema walilipwa na CCM kushiriki kwenye uchaguzi bila ushahidi wowote...kuna vyama vinasubiri Chadema watoke na hoja fulani, halafu vinaibuka kuanza kuipinga hoja hiyo.
Mimi sioni kosa katika hilo. Inawezekana kuwa wanaamini kuwa kuna watanzania wana integrity ya kuyasimamia bila upendeleo. Au wana hofu kuwa kipengele hicho kinaweza kutumika vibaya na CCM. Kuna tatizo gani kusema Msuluhishi anaweza kutoka kokote duniani ili mradi akubalike na vyama makini vya upinzani?..kwa mfano, sasa hivi Chadema wana hoja kwamba maridhiano yasimamiwe na Msuluhishi wa kimataifa. Sasa kumeibuka vyama kila wakiongea wanadai mgogoro uliopo umalizwe na watu wa ndani.
Chadema wanapaswa kutambua kuwa hayo maridhiano sio ya Chadema na CCM peke yake. Ni busara kusikiliza hoja za wanaotofautiana nao. Uzoefu wa ACT Wazalendo nao ni muhimu kupewa uzito...Sasa Chadema hawakuibuka tu kwamba wanataka msuluhishi aje kusimamia maridhiano. Pendekezo lao linatokana na uzoefu wa mazungumzo baina yao na Ccm bila mtu wa kati ambayo yalifeli.
Kuna vyama kweli ambavyo vinaona kuwa wajibu wao ni kuwa upande wa CCM. Lakini viko ambavyo havioni shida kutofautiana na Chadema. Kutofautiana sio kupambana.
Kutofautiana ni sehemu ya siasa. Ni hili la kuona kuwa ni wajibu wa vyama vya upinzani kuunga mkono kila hoja ya Chadema ndio unaleta matatizo. Hasa ukiangalia kuwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani walitoka Chadema baada ya kutofautiana na mwenendo wa Chadema na hata sera zake. Viongozi wengi wa Chaumma walitoka Chadema kwa sababu walikuwa na tatizo na utekelezaji wa NRNE. Walipoona hamna muafaka wakajitoa. Na hilo sio dhambi. Dhambi ni kusema walilipwa na CCM kushiriki kwenye uchaguzi bila ushahidi wowote.
Mimi sioni kosa katika hilo. Inawezekana kuwa wanaamini kuwa kuna watanzania wana integrity ya kuyasimamia bila upendeleo. Au wana hofu kuwa kipengele hicho kinaweza kutumika vibaya na CCM. Kuna tatizo gani kusema Msuluhishi anaweza kutoka kokote duniani ili mradi akubalike na vyama makini vya upinzani?
Chadema wanapaswa kutambua kuwa hayo maridhiano sio ya Chadema na CCM peke yake. Ni busara kusikiliza hoja za wanaotofautiana nao. Uzoefu wa ACT Wazalendo nao ni muhimu kupewa uzito.
Amandla....