Alivyoifanya Mobutu Congo DR ndio wanavyoifanya CCM Tanzania. Ni suala la muda tu Tanzania itakuwa kama Congo

Rwanda haina nguvu yoyote ya kuiletea fujo Congo.
Kinachoendelea ni wacongo wenyewe wa ukanda WA Kivu.
Wale ni Watutsi sio WaCongo na Watutsi ni ndugu zake na Kagame ndio maana anawapiga tafu kuisambaratisha Congo yenye mizenguo haya nyinyi Jeshi lenu mnalitoa wapi Kanda ya Ziwa?
 
🤓🤓
Sasa mbona kama unaniingiza kwenye Jambo ambalo sipo?
Mkuu nataka nikuoshee ni jinsi gani ilivyo ngumu kupambana na CCM kivyovyote maana nyuma ya CCM kuna Jeshi sio kikundi cha Wahuni wachache namaanisha ukiigusa CCM umeligusa Jeshi kiini cha Jeshi la Wananchi ila sio Jeshi la Wananchi ni Jeshi la CCM haya nyinyi Jeshi mnatoa wapi?
 
Wenye Akili kama Kikwete wanaelewa kuwa usimdharau adui hata kama ni adui mdogo.

Wewe ndio unaona ni ngumu lakini ni Jambo linalowezekana Kabisa.

Ikishatokea Ukabila Hilo Jeshi halina uwezo wa kufanya lolote.
Ukabila ni zaidi ya jeshi sijui kama unaelewa hio
 
Mwaka 2020 niliandika uzi humu jamvini kuhusu tofauti ndogo iliyokuwepo baina ya Congo ya Mobutu na Tanzania!

Niliandika uzi ule kwa sababu kuna vitu vingi sana vilivyokuwa vinatokea wakati ule havikuwa na tofauti na mambo yaliyokuwa yanatokea nchini Congo kipindi cha Mobutu. Niliweka na Documentary waliyoiandaa wazungu inayoonesha namna Congo ya Mobutu ilivyokuwa (Nashauri wanabodi muiangalie hadi mwisho bila kuchoka na mtajifunza kitu hakika).

Labda watu hawafahamu.

Congo tunayoiona leo ya vijana kuwasifia watu wenye hela na kuwaabudu badala ya kujikita kwenye kupata maarifa ya kuisaidia nchi yao kwenda mbele iliasisiwa na aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Mobutu Seseko Kuku wa Zebanga.

Baada ya kushika madaraka, Mobutu alitengeneza Congo ya machawa. Ilikuwa huwezi kupata cheo au nafasi Serikalini bila kuonesha unyenyekevu wako na kujipendekeza kwako kwake.

Chama chake alikiita chama dola na kuwatengeneza wa Congo kukisifu chama chake na yeye binafsi. Zilitungwa nyimbo za kumsifu, zilitengenezwa nguo zenye picha zake pamoja na kofia ambazo vijana, wamama na watu wa Congo walitengenezewa utaratibu wa kuzivaa ili kumsifu na kuonesha kuwa maendeleo ya Congo ni yeye na hakuna Congo bila yeye.

Badala ya wananchi wa Congo kutengenezwa kufikiri vizuri kwa fikra huru kwa ajili ya maendeleo yao kwa miaka mingi ijayo, walitengenezwa kuwaza maendeleo ni mtu na bila kumsifu huyo mtu mkono hauwezi kwenda kinywani.

Matokeo ya hayo ni kwamba badala ya kutengeneza vijana na watu wenye akili kwa faida ya nchi yao, walitengeneza mapooza kichwani ambao ndo walipewa madaraka na Mobutu, hivyo nchi ya Congo alishindwa kustawi na kuhimili maadui wa ndani na nje maana walioshika uongozi hawakushika kwa merit ila kwa kujipendekeza kwao kwa Mobutu na chama chake.

Hali hii ndo yanayotokea sasa nchini Tanzania, kwetu Mobutu wetu ni CCM.

Kuanzia mwaka 2012, CCM walianza kutengeneza mfumo wa siasa zilizoshika hatamu leo hii. Walitengeneza mfumo wa vijana wanaoonesha kuwapigania, kuwatetea na kuwasemea vizuri viongozi wao kupewa madaraka makubwa ya uongozi kwenye utumishi wa Umma. Hii ilianza kwa Nape baada ya kumtukana Lowasa na kuonesha kuwa chawa wa JK alikabidhiwa Ukuu wa Wilaya na baadae cheo ndani ya CCM.

Ilifuata kwa Makonda ambaye nae baada ya kuonesha kuwa chawa wa JK kwa kumsema vibaya Lowassa akazawadiwa ukuu wa wilaya.

Kubwa zaidi ni Magufuli ambaye kwenye kila hotuba za kuzindua miradi ya ujenzi alikuwa anamsifia JK mwishowe JK akaona ndo awe Rais wa Tz.

Kipindi cha JK, vijana waliokuwa vyuoni waliotengenezwa na siasa za namna hiyo walianza kuzawadiwa nafasi ya uongozi na utumishi Serikalini kama DAS, DED, DC na nyinginezo.

Alipokuja Magufuli ndo alilifanya suala hili zaidi ya alivyofanya Kikwete. Magufuli alikuwa akikuona leo umemuongelea vizuri kwenye chombo cha habari kesho yake unasikia Msigwa kakutangaza wewe kuwa DC/DED/DAS/RAS/KM au Mwenyekiti wa Bodi au Mjumbe wa Bodi. Watu waliacha kupewa vyeo kwa uwezo wao ila kutokana na uchawa wao kwa Rais na chama chake.

Matokeo yake hali hii imeendelea na kukua hadi kwenye maisha ya kawaida. Mitaani machawa ndo wanqpewa fursa, kwa wasanii wanaotunga nyimbo za kuwasifia viongozi ndo wanapewa tenda za kufanya kazi na Taasisi za Umma ili wapige hela.

Sasa hali hii imefika climax. Siku hizi fedha za umma (kodi za wananchi) zinazotengwa kwenye bajeti ya Serikali kutekeleza miradi mbalimbali zinahusishwa na mtu kusifiwa binafsi kuwa anafanya yeye. Utasikia Magufuli kafanya haya, hakuna kama Magufuli, mara Samia kafanya haya, hakuna kama Samia.

Sasaivi huko CCM kama huvai kofia yenye nembo ya SSH au Samia au nguo yenye picha ya Samia unaonekana kama sio mwenzao.

Kwa wasio na akili wanaweza kuona jambo hili ni la kawaida sana ila kwa wenye akili napenda kuwaambia hizi ni dalili rasmi kuwa Tanzaniartunaenda kuwa kama Congo.

Suala hili linaenda kudumaza sana akili za Watanzania, suala hili linaenda kututengenezea jamii iliyopo Congo leo nchini Tanzania ambayo inaamini kwenye kujipendekeza, kutukuza wenye hela hali iliyofanya Taifa lile leo kufa na kuwa shamba la bibi kwa watu wenye akili (Mataifa mbalimbali ambayo yanaliibia ikiwemo Rwanda na Uganda)

Leo hii Tanzania, Vijana ambao wanashika nafasi zinazopaswa kushikwa na watu smart na intelligent ni vijana ambao wanaamini bila kujipendekeza kwao kwa CCM na Viongozi wao wakuu wasingefika hapo. Vijana hawa hawataweza kuifanya nchi yetu kuhimili hila za maadui wa ndani na nje ambao nchi zao zinawatengeneza kwa kuwapa exposure na kuwatengeneza kuwa smart isivyo kawaida.

Vijana hawa hawataweza kutengeneza Tanzania Dream ambayo inapaswa kutengenezwa na watu wanaoshika nafasi za maamuzi kwa merit na sio uchawa. Watu wanaofanya research na kuandika mambo makubwa na kuyasimamia yawe kweli.

Naionea huruma Tanzania. Kama Vyombo vya dola havitaisaidia kuiondoa CCM madarakani. Sisi ni Congo tunaofuata.
We kwl ni poyoyo, we unaumwa nenda katibiwe. Umejaza server ya JF na matope
 
Mobutu ni kama Amin wanasingiziwa mambo mengi sana ila walikuwa mtu wema. Mobutu katawala miaka 32 wakati mpenda demokrasia wetu katawala miaka 22 wote kwa pamoja wameacha uchumi wa nchi zao ukiwa goigoi na dhaifu kuliko awali. Tuepuke propaganda za kumsingizia Mobutu.
Sijawahi kusoma comment ya tahira kama wewe. Unam-compare Nyerere na Mobutu!!!!!!!!! Tahira hasa; yaani cretin
 
Hicho unacho kitamani kitokee Tz hakiwezekani... Misingi ya siasa jamii na uchumi wa WaTz haufanani na nchi yoyote Africa, hivyo Tz inaendelea kubaki nchi bora ya kuigwa kwasababu ya misingi na falsafa thabiti inayojipambanua vzuri...
Misingi ndo hiyo insuobomolewa Kwa uteuzi wa machawa bila kujali uelewa na weledi, utekaji na mauaji na zaidi kuminya demokrasia. Ukiwa CCM na mnufaika wa haya mambo utaona ni kawaida na hakuna wa kuleta shida, lakini mind you Kuna moto unaochichewa chini Kwa chini, turekebishe mapema kabla hayujachelewa.

Just imagine 17/3/2021, kama Mabeyo asingekuwa mzalendo wa kweli anaye analyse mambo, tuseme angekuwa kawekwa hapo si Kwa weledi bali uchawa, nadhani Sasa tungekuwa tinaongea mengine.
 
Muda utaongea. Ni suala la muda tu!
Soon Tanzania tunaenda kuwa kama Congo kwa sababu aliyoyafanya huyo Mobutu Congo hadi ku collapse proper think tanks ndo wanachofanya CCM sasa.

Amini maneno yangu. Miaka si zaidi ya 25 ijayo Mungu atupe uhai, huu uzi utafufuliwa na kujadiliwa maana Tanzania itakuwa imefikia rasmi ilipofikia Congo leo kama hatua dhidi ya CCM hazitachukuliwa.
We bwege huna kazi ya kufanya? Unatujazia ushuzi tu. Acha uchuro huo muda utakuwa wa kifo chako usikibarie nchi yetu huo upuuzi wako. We ni zero brain afadhali ya nyumbu
 
Kuna hoja gani ya kutoa hapa? Yaani Tanzania inafananishwa na Zaire ya Mobutu halafu mimi Mtanzania wa kweli nikae kimya? Eti nitoe hoja!? Upumbavu haujadiliwi!!!!
Ukweli mchungu ni kwamba, kuna mambo mengi sana aliyofanya Rais Mobutu Sese Seko na Utawala wake ambayo pia yanafanywa na Utawala uliopo hapa Tanzania tangu zamani na hata Sasa.
Mathalani, Mobutu Sese Seko alikuwa hataki kabisa kukosolewa na Mtu yoyote yule. Yeye alikuwa anataka Asifiwe tu lakini siyo kukosolewa. Wale Watu ambao walithubutu kukosoa Utawala wake waliishia kutekwa, kupotezwa, kuwekewa sumu, kutiwa misukosuko mibaya ya kufungwa gerezani na/au kuuawa.
Raia wengi sana wa Zaire waliitoroka nchi hiyo na kukimbilia kwenda kuishi katika nchi zingine za ugenini, Zaire (DRC) kwa Sasa ni miongoni mwa nchi chache za Afrika zenye diaspora wengi sana hapa duniani, chanzo chake hasa ni hiki cha kuwepo kwa tatizo la Utawala mbaya wa Kidikteta katika nchi hiyo.

Kumkosoa Dikteta Mobutu Sese Seko ilikuwa ni kujikatia tiketi ya kifo nchini Zaire.
 
Mnavyo iombea mabaya Tz, halafu ndio kwanza Mungu anaibariki CCM inazidi kutawala nchi, hakuna maandamano hakuna kelele wapinzani wote wameufyata wamebaki kutukanana wenyewe kwa wenyewe kisa uenyekit 🤣💩
Muda utaongea. Uzuri humu JF nyuzi zinaishi.
 
Mwaka 2020 niliandika uzi humu jamvini kuhusu tofauti ndogo iliyokuwepo baina ya Congo ya Mobutu na Tanzania!

Niliandika uzi ule kwa sababu kuna vitu vingi sana vilivyokuwa vinatokea wakati ule havikuwa na tofauti na mambo yaliyokuwa yanatokea nchini Congo kipindi cha Mobutu. Niliweka na Documentary waliyoiandaa wazungu inayoonesha namna Congo ya Mobutu ilivyokuwa (Nashauri wanabodi muiangalie hadi mwisho bila kuchoka na mtajifunza kitu hakika).

Labda watu hawafahamu.

Congo tunayoiona leo ya vijana kuwasifia watu wenye hela na kuwaabudu badala ya kujikita kwenye kupata maarifa ya kuisaidia nchi yao kwenda mbele iliasisiwa na aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Mobutu Seseko Kuku wa Zebanga.

Baada ya kushika madaraka, Mobutu alitengeneza Congo ya machawa. Ilikuwa huwezi kupata cheo au nafasi Serikalini bila kuonesha unyenyekevu wako na kujipendekeza kwako kwake.

Chama chake alikiita chama dola na kuwatengeneza wa Congo kukisifu chama chake na yeye binafsi. Zilitungwa nyimbo za kumsifu, zilitengenezwa nguo zenye picha zake pamoja na kofia ambazo vijana, wamama na watu wa Congo walitengenezewa utaratibu wa kuzivaa ili kumsifu na kuonesha kuwa maendeleo ya Congo ni yeye na hakuna Congo bila yeye.

Badala ya wananchi wa Congo kutengenezwa kufikiri vizuri kwa fikra huru kwa ajili ya maendeleo yao kwa miaka mingi ijayo, walitengenezwa kuwaza maendeleo ni mtu na bila kumsifu huyo mtu mkono hauwezi kwenda kinywani.

Matokeo ya hayo ni kwamba badala ya kutengeneza vijana na watu wenye akili kwa faida ya nchi yao, walitengeneza mapooza kichwani ambao ndo walipewa madaraka na Mobutu, hivyo nchi ya Congo alishindwa kustawi na kuhimili maadui wa ndani na nje maana walioshika uongozi hawakushika kwa merit ila kwa kujipendekeza kwao kwa Mobutu na chama chake.

Hali hii ndo yanayotokea sasa nchini Tanzania, kwetu Mobutu wetu ni CCM.

Kuanzia mwaka 2012, CCM walianza kutengeneza mfumo wa siasa zilizoshika hatamu leo hii. Walitengeneza mfumo wa vijana wanaoonesha kuwapigania, kuwatetea na kuwasemea vizuri viongozi wao kupewa madaraka makubwa ya uongozi kwenye utumishi wa Umma. Hii ilianza kwa Nape baada ya kumtukana Lowasa na kuonesha kuwa chawa wa JK alikabidhiwa Ukuu wa Wilaya na baadae cheo ndani ya CCM.

Ilifuata kwa Makonda ambaye nae baada ya kuonesha kuwa chawa wa JK kwa kumsema vibaya Lowassa akazawadiwa ukuu wa wilaya.

Kubwa zaidi ni Magufuli ambaye kwenye kila hotuba za kuzindua miradi ya ujenzi alikuwa anamsifia JK mwishowe JK akaona ndo awe Rais wa Tz.

Kipindi cha JK, vijana waliokuwa vyuoni waliotengenezwa na siasa za namna hiyo walianza kuzawadiwa nafasi ya uongozi na utumishi Serikalini kama DAS, DED, DC na nyinginezo.

Alipokuja Magufuli ndo alilifanya suala hili zaidi ya alivyofanya Kikwete. Magufuli alikuwa akikuona leo umemuongelea vizuri kwenye chombo cha habari kesho yake unasikia Msigwa kakutangaza wewe kuwa DC/DED/DAS/RAS/KM au Mwenyekiti wa Bodi au Mjumbe wa Bodi. Watu waliacha kupewa vyeo kwa uwezo wao ila kutokana na uchawa wao kwa Rais na chama chake.

Matokeo yake hali hii imeendelea na kukua hadi kwenye maisha ya kawaida. Mitaani machawa ndo wanqpewa fursa, kwa wasanii wanaotunga nyimbo za kuwasifia viongozi ndo wanapewa tenda za kufanya kazi na Taasisi za Umma ili wapige hela.

Sasa hali hii imefika climax. Siku hizi fedha za umma (kodi za wananchi) zinazotengwa kwenye bajeti ya Serikali kutekeleza miradi mbalimbali zinahusishwa na mtu kusifiwa binafsi kuwa anafanya yeye. Utasikia Magufuli kafanya haya, hakuna kama Magufuli, mara Samia kafanya haya, hakuna kama Samia.

Sasaivi huko CCM kama huvai kofia yenye nembo ya SSH au Samia au nguo yenye picha ya Samia unaonekana kama sio mwenzao.

Kwa wasio na akili wanaweza kuona jambo hili ni la kawaida sana ila kwa wenye akili napenda kuwaambia hizi ni dalili rasmi kuwa Tanzaniartunaenda kuwa kama Congo.

Suala hili linaenda kudumaza sana akili za Watanzania, suala hili linaenda kututengenezea jamii iliyopo Congo leo nchini Tanzania ambayo inaamini kwenye kujipendekeza, kutukuza wenye hela hali iliyofanya Taifa lile leo kufa na kuwa shamba la bibi kwa watu wenye akili (Mataifa mbalimbali ambayo yanaliibia ikiwemo Rwanda na Uganda)

Leo hii Tanzania, Vijana ambao wanashika nafasi zinazopaswa kushikwa na watu smart na intelligent ni vijana ambao wanaamini bila kujipendekeza kwao kwa CCM na Viongozi wao wakuu wasingefika hapo. Vijana hawa hawataweza kuifanya nchi yetu kuhimili hila za maadui wa ndani na nje ambao nchi zao zinawatengeneza kwa kuwapa exposure na kuwatengeneza kuwa smart isivyo kawaida.

Vijana hawa hawataweza kutengeneza Tanzania Dream ambayo inapaswa kutengenezwa na watu wanaoshika nafasi za maamuzi kwa merit na sio uchawa. Watu wanaofanya research na kuandika mambo makubwa na kuyasimamia yawe kweli.

Naionea huruma Tanzania. Kama Vyombo vya dola havitaisaidia kuiondoa CCM madarakani. Sisi ni Congo tunaofuata.
Kabisa tatizo kubwa la nchi hii sasa sio kingine ni CCM na mfumo waliokwisha ujenga. Jamani tuondokane na genge hili mapema iwezekanavyo la sivyo...
 
Wenye Akili kama Kikwete wanaelewa kuwa usimdharau adui hata kama ni adui mdogo.

Wewe ndio unaona ni ngumu lakini ni Jambo linalowezekana Kabisa.

Ikishatokea Ukabila Hilo Jeshi halina uwezo wa kufanya lolote.
Ukabila ni zaidi ya jeshi sijui kama unaelewa hio
Mkuu nimekuelewa vizuri ila ondoa ukabila Congo kinachotokea sio ukabila wale jamaa wanachopigania kwa sasa kule haina uhusiano kabisa na ukabila, swali langu hao kanda ya Ziwa unaowasema wana Jeshi kubwa kiasi gani kulishinda Jeshi la CCM? Acheni kuota mchana
 
Mkuu nataka nikuoshee ni jinsi gani ilivyo ngumu kupambana na CCM kivyovyote maana nyuma ya CCM kuna Jeshi sio kikundi cha Wahuni wachache namaanisha ukiigusa CCM umeligusa Jeshi kiini cha Jeshi la Wananchi ila sio Jeshi la Wananchi ni Jeshi la CCM haya nyinyi Jeshi mnatoa wapi?
Kwa hiyo leo mnasema kabisavJWTZ ni jeshi la CCM?

Uzuri na wao wanasoma wanaona mlipofikia CCM.

Muda utaongea!
 
Back
Top Bottom