Nilishakuona muda mrefu, wewe ni fundi wa kukariri maandiko bahati mbaya hauna upeo wa kutafsìri, kama unakumbuka ulishawahi kuja na article ya constitution kwa mbwembwe hivi hivi nikakuuliza swali moja ukapotea moja kwa moja, hili tatizo bado unalo.
Umeshindwa kutafsiri kile alicholeta mleta mada, badala yake unakimbilia kuleta andiko kama vile andiko uliloleta ndio linajibu, wakati ukweli halijibu chochote, matokeo yake ni kama unataka kutuambia alicholeta mleta mada ni uongo/hakipo, wakati tatizo liko kwako, unajua copy & paste tu, hujui kuchambua kitu kwa kina.
Mimi nilimjibu mleta mada baada ya kuchambua alichoandika, wewe ukaja quote nilichoandika kwa kuweka andiko, huoni unajichanganya, usipende kukariri maandiko ukajiona msomi, wewe bado mchanga sana kupevuka kifikra.