Aliyeamua kuchukua hii Route ya Johannesburg to Dar Es Salaam ni Mtanzania Kweli?

Mbona kama route haijapangiliwa vizuri na ni kama haiwezekani? Imekosewa labda
Kwenda south ukiamua kupita malawi basi huwezi pita zambia na tunduma, route ya malawi unatokea kasumulu malawi msumbiji zimbabwe then south africa , labda uniambie hilo basi lita ondoka na njia moja na kurudi na njia nyingine
 
Kama wamekosea ni wao, coz nimeandika kutokana na taarifa yao kwa umma, nimewasiliana nao hadi leo hawajanijibu so twende as walivyosema kama wrong/correct basi tutapata majibu siku ya kwanza ya safari, si mbali.
 
Hao nao miyeyusho walisema 30 may linaenda Johannesburg lakin mpaka leo 1 June haijulikan wataenda lini.
Kwa mtu ambaye hataki mbambambaa za Wabongo, Lusaka kuna mabasi ya Wasouth Africa wenyewe yanaitwa Translux na Greyhound, yanakwenda rout za Miji yote mikubwa ya South Africa kutokea Lusaka Zambia.

Kama hutaki longolongo nashauri mtu upande hayo mabasi, madreva wazungu hadi wahudumu wa kike kwenye mabasi ni wazungu, hakuna longolongo, route ni kutoka Lusaka to Pretoria na Jo'burg kupitia Zimbabwe au Gaborone Botswana

Lusaka to Natal Durban.

Lusaka to Cape town unapitia Namibia.
 
Hata mimi mwenyewe nimeshangaa, route ya Dar-Tunduma-Zambia-Malawi-Msumbiji-Zimbabwe-Joasberg?????
Hiyo route ni controversial. Haiwezekani Kwa kutumia basi Moja.
Hiyo Route inawezekana lkn ni unnecessary. Tunduma unaitafuta Lusaka then Chipata unaingia Malawi Lilongwe unaenda Dedza au Mwanza Kuingia Mozambique. Inawezekana kabisa lkn hii Route ni ngumu sana yaani sana
 
Hiyo ni miaka nenda miaka Rudi ukifika hapo hasa baada ya kuvuka border ya Zimbabwe utakaguliwa hadi aibu binafsi walinikagua rusha rusha vitu dah nilitaka kugeukia palepale ila nikasema no sweat ngoja niendelee
SA ilinipa experience ya kuthamini sana nchi yangu
 
Aisee noma sana
 
Hao nao miyeyusho walisema 30 may linaenda Johannesburg lakin mpaka leo 1 June haijulikan wataenda lini.
Kama walikujibu wenyewe it's okay ila kama ni watu back it wasn't miyeyusho, chuma inaingia leo usiku bondeni.
 
Niliwacheck kwenye ile namba yao wakasema watanijulisha.
Inasemekana wanamalizia kujenga ofisi.
Yaan hawa ni miyeyusho kuliko miyeyusho yenyewe mana niliwasiliana na jamaa mmoja wa huko akanaiambia anakuja bongo 15 May yaani hadi sasa hajaja yeye daily ni kunitumia tu mipicha ya mbasi wao eti nimsaidie kushare malaaabuik
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…