Niko hapa kuthibitisha bus lipo, linafanya safari fresh tu, juzi limeondoka Magufuli bus terminal leo wanaingia Johannesburg, nauli ni 350,000/=
Ofisi zao upande wa Tanzania zipo Shekilango Sinza, wana ofisi Lusaka na Johannesburg.
Tunakumbushana tu wale jamaa Primitive wanataka kuendesha oparesheni Dudula jijini Johannesburg na kitongoji kinacholengwa ni Hillbrow.
Inasemekana Dawa za kulevya zinamaliza nguvu kazi yao sasa wanataka kuendesha oparesheni kwenye mizizi ya wauza Dawa za kulevya hasa kutoka Tanzania na West Africa.
Kabla ya kuanza oparesheni Dudula wameshaanza kuchoma moto mijengo wanayoishi wageni kama chaka.
Ukitumia jicho la tatu kufuatilia hali halisi hii oparesheni ina baraka zote za serikali yao.
Kama huna jambo la maana la Kukupeleka South Africa kaa kitako kwa kutulia tafuta chaka lingine, wale jamaa huwa hawatanii na wala huwa hawatishii kuweka mkwara, wakisema kitu wanafanya kweli.