Aliyebuni hizi engine za forester XT aishi milele huko aliko

Aliyebuni hizi engine za forester XT aishi milele huko aliko

Usisumbuke ipo Ford ranger ya 2020 2.2 Diesel ipo hapa Arusha mwambie aje na gari yake anayoiamini haya madudu ni mepesi sana..nilipokua naileta kutoka SA huko Mbeya tulikua na jamaa wana V 8 walikua wana Bendera ya Ubalozi wa DRC tulipofika Iringa nilipokua naweka mafuta walisema wataagiza Ranger kwa safari ndefu na Contact walichukua walikua hawajui kuwa Ford Ranger yupo hivi Road harafu balance ya kutosha..Jan hii ntaleta Mazda CX-5 za Petrol na Diesel ntaona moto wake Subaru ipo SH 9 kweli ni gari ila Ford ni moto mwingine..
Hio Ford ranger unaisukuma kwa ngapi
 
Kwenye safari niliyofanya kutoka DAR-DODOMA-SHINYANGA-MASWA-LAMADI HADI KISORYA nilifanya test ya kumwaga moto nione hii ndinga ikoje, aisee Subaru ni gari banaa asukuambie MTU.

Aliyebuni hizi boxer engine anastahili sifa maana kama hii nguvu iliyopo kwenye hizi engine ni balaa Sana maana Ngoma ilikuwa inapenda mlima kama inashuka vileee!!!

Kwenye overtaking inakupa kujiamini mno na niliweza kuovertake magari manne bila shida( mfumo wake wa sport na sport sharp# ni kama unaendesha fighter jets)
Kama mateso kuna madereva nimewatesa Sana njiani hasa wale wanaopenda ligi.

Compact crossover Ambazo ukizifuata unapotea ni Mazda CX5

....
mazda CX 5 zina balaa Sana hii gari ikikupita achana nayo usijaribu kuifuata maana Moto wake sijaona WA kuifananisha, Kwa segment ya crossover sijaona bado WA kuikalisha hii Mazda CX5

Ukiachana na land cruiser LC 200 na LC 300 kuna Prado TXL na Baba lao FORD RANGER hizi gari usijaribu kubishana nazo

madereva ambao wanapenda kutunisha misuli msijaribu kwa FORD RANGER hii ni habari nyingine,hii gari nahisi inaongoza Huko barabarani Kwa kumwaga moto maana kama V8 ilikuwa inakalishwa wewe ni Nani unataka kufata huu Moto?

Hadi namaliza safari yangu sijaona gari inakimbia kama ford ranger......

Kila kheri madereva!!!!!
Ulitumia mafuta kiasi Gani?
 
Ulitumia mafuta kiasi Gani?
Mkuu kwenye mafuta itabidi ujipange kidogo maana kutoka DAR Hadi KISORYA nilitumia mafuta ya 400,000/= kwasababu gari ilibeba vitu vingi Sana...wakati wa kurudi nimetumia mafuta ya 374,000/=
 
Hiyo mashine sura yake kwa mbele imekaa box,, iko unyama sana, hapa arusha kuna mbili huwa naziona moja ni gray colour na nyingine ni nyeupe
Ile ni ingine toleo la 2023 na 2024 hii ni version ya Wildtruck sema Ford Ranger HR sio XLT au Ranger kama hiyo unayoisema wewe ile inafika kuanzia 150m ina upana sawa na Ford ranger Raptor ni gari nyepesi sana na ulaji wa mafuta ikiwa kuanzia 80km/h kuendelea ni 1L kwa 14.4km kuendelea inakuonyesha kwenye dashboard kwa kila speed yake na kiwango cha mafuta inachotafuna...
 
Naijua vizuri boxer engine. Haiitwwi hivyo kwasababu iko kama box. Inaitwa hivyo kwasababu gari piston nne zi.epangwa mbili kulia mbili kushoto. The way zinazungusha engine ni kama mabondia wanarushiana ngumi hence the name boxer engine.
Duuh unakabia juu sana mkuu...😂😂😂😂
 
Acha ushamba wewe nooo Hulu free way za South Africa uone ndinga hayo MA Toyota na LA Subaru yako nakupa Golf GT upambane nayo.
 
Acha ushamba wewe nooo Hulu free way za South Africa uone ndinga hayo MA Toyota na LA Subaru yako nakupa Golf GT upambane nayo.
Subaru WRX STI ukiwaambia waitafute Gaborone mpaka mpakani mwa Zambia na Botswana maana ile bara bara haina shida huyo wa Subaru atafika mapema na akiambiwa aendelee na safari utamkuta Tunduma kapaki gari siku moja kabla ya Golf GTI kufika..
 
Ile ni ingine toleo la 2023 na 2024 hii ni version ya Wildtruck sema Ford Ranger HR sio XLT au Ranger kama hiyo unayoisema wewe ile inafika kuanzia 150m ina upana sawa na Ford ranger Raptor ni gari nyepesi sana na ulaji wa mafuta ikiwa kuanzia 80km/h kuendelea ni 1L kwa 14.4km kuendelea inakuonyesha kwenye dashboard kwa kila speed yake na kiwango cha mafuta inachotafuna...
Ila 2024 vyuma vya kibabe sana vimeingia nchi
 
Mkuu Mimi nimeongelea compact crossover hiyo gari unayoisema ni supercar
hiyu nse si kaja tu wangu wangu kamaliza form two kapata div 2 a nasubir arud shule. zimeongelewa compact suv analeta google . ok vip kuhusu tiguan? na jeep cherokee na volvo naziona ona wadau wanazo?
 
Sasa mzee si inategemea unazungumzia BMW na Range Rover gani!

Kwa mfano, ukiweka X5M competition inakupa power ya bhp 616 na torque ya lbs/ft 553. Range Rover SV Autobiography inakupa ya bhp 542 na torque ya lbs/ft 502.

Halafu madereva wa STK wanasema LC 300 haifai kwa zile draft za haraka haraka walizozizoea barabarani kwa sababu ni nyepesi kuliko LC 200.
Nashangaa au kazichagua range rover na x5 za 3.0 L?
 
Tukiwa sehemu tambarare, gari yako ina maximum speed 280km/hr, na yangu ina maximum speed 260km/hr, na wote sehemu hiyo hatuwezi kuzidi spedi ya 180km/hr ambayo iko within range ya gari zetu. Nipe sababu ya kisayansi kwa nini useme gari mojawapo ya hizo mbli ni moto chini kuliko nyingine, kama hilo sio suala la dereva anaeiendesha. Nimeshawawashia moto watu na Benz zao mimi nikiwa na IST. Sikuona IST ni moto chini zaidi ya Benz, bali nilijua mimi ni dereva moto chini kuliko dereva wa Benz. Ndio maana hata mabasi Yutong kwa Yutong yanazidiana, kutegemea dereva!
Kwa hiyo kwa sababu madereva wanazidiana tuache ku specify magari?Je huyo dereva mahiri akipewa ashok leyland yenye hp 248 katika free driving atazichachafya yutong ya hp 360?wewe kuwapita wenye BMW na IST inawezekana maana unaweza ukawa na uwezo wa kufika 180 na mwenzako gari ikawa na 320 km/h lkn ukute hajawahi kufika hata 160km/h huyu tumwite ni mshindani?
 
Life bwana nimepambanaa wewe nimeishia kununua Pikipiki Sino ray 250cc used kwa mtu
Una roho mbaya ndo maana huna gari unaishia kuendesha mikweche ya bodaboda yenye taa moja (taa chongo).

Jifunze kutoka kwa mume wangu Extrovert anayemiliki yards

Maskini mkubwa wewe
 
hiyu nse si kaja tu wangu wangu kamaliza form two kapata div 2 a nasubir arud shule. zimeongelewa compact suv analeta google . ok vip kuhusu tiguan? na jeep cherokee na volvo naziona ona wadau wanazo?
Hizo gari za wazungu ni sayari nyingine Kwa mfano Volkswagen Tiguan naijua kidogo hiyo gari gearbox yake ni DSG (direct shift gear box) inachanganya mapema kama unafumba macho ni balaa Sana.
Volvo nayo ni zaidi hizi gari zetu za kijapan kama Subaru na mada CX 5
 
Kwa hiyo kwa sababu madereva wanazidiana tuache ku specify magari?Je huyo dereva mahiri akipewa ashok leyland yenye hp 248 katika free driving atazichachafya yutong ya hp 360?wewe kuwapita wenye BMW na IST inawezekana maana unaweza ukawa na uwezo wa kufika 180 na mwenzako gari ikawa na 320 km/h lkn ukute hajawahi kufika hata 160km/h huyu tumwite ni mshindani?
Umeuliza swali ukajijibu!
 
Gari hua Ni uwezo tu wa dereva kua kichaa.Nishakimbizana na Ford ranger T6 nikiwa na gx110,mpk mwenye hio Ford akaja kunisalimia kwny msosi Singida hio.Akaniambia mdau hii kitu si mchezo
Gx110 👏🏻👏🏻
 
Back
Top Bottom