Pre GE2025 Aliyefukuzwa CCM baada ya kupinga Rais Samia kupitishwa mgombea pekee urais agoma kuondoka CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mental case hiyo

Ukishafukuzwa hakuna kugoma
 
Amesimama kwenye ukweli apewe ulinzi kabla ajatekwa na kupotezwa.
 
Sio kila mtu ni muoga kama wewe
Haki inapiganiwa vitu vingi unavyoviona leo watu walivipigania kwa jasho na damu
Acha ushujaa wa nyuma ya keyboard kijana, kama unajiona unaujasiri wa kupigania hayo unayo yataka ebu jaribu kuingia barabarani uone kitakacho kupata kwenye utawala wa hiki chama chenu...🤣
 
jibu hoja za malisa
Gentleman,
kwahiyo kimbwelambwela kwa mgombea urais wa cck kujibiwe na chama chenye kazi ya kuwatumikia wananchi?

huo si utakua ushirikina sasa,
yaani watu waache kuwajibikia wananchi wa deal na mzee magoma kweli?🐒
 
Msimtishe mmezoea kutishia watu ,ndivyo mlivyo eee hamtaki wasema kweli ndani ya chama,sasa hiyo democrasia mnayo taka wengine wawe nayo ni ipi?
Mambo ya bring back fulani.. Anyways, hili lichama ni la kidictator. Akiona hawezi aondoke
 
Acha ushujaa wa nyuma ya keyboard kijana, kama unajiona unaujasiri wa kupigania hayo unayo yataka ebu jaribu kuingia barabarani uone kitakacho kupata kwenye utawala wa hiki chama chenu...🤣
unafikiri nyerere angekuwa na fikra kama zako tungepata uhuru acha ujinga
Nyie ndo wale wanaume mnaopigwa makofi mbele ya familia yako unakubali kwa sababu aliyekupiga amekuzidi mamlaka na madaraka
 

View: https://youtu.be/oBNyN8ncqiI?si=ZIyk5CUcoD3-qrAb
➡Anasema, hajui na wala hatambui kama amefukuzwa uanachama wa CCM...

➡Hakupinga kuteuliwa kwa Samia kuwa mgombea u - Rais bali anapinga mchakato wa uteuzi wake kwa kuwa haukufuata utaratibu wa kikatiba na hivyo katiba imevunjwa..

➡Amewahimiza wana CCM wote wanaotaka kugombea u - Rais kwenda kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea u - Rais kufanya hivyo maana kilichofanyika Dodoma tarehe 19/1/2025 ni ubatili mtupu kikatiba...

➡Mwisho, amemaliza kwa kuahidi kumpeleka mahakamani katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro kwa kumuita "mhaini" eti tu kwa kupinga mchakato batili wa kumteua Bi Samia kuwa mgombea u - Rais pekee bila kufuata utaratibu wa kujaza fomu na kusimama mbele ya mkutano mkuu kuomba kuteuliwa ili akathibitishe huo uhaini wake pamoja na kumsafisha..

➡Ameendelea kushikilia msimamo wake kutaka mchakato wa uteuzi wa mgombea u - Rais CCM urudiwe kwa sbb ule ulikuwa batili kikatiba. Hakuna utamaduni wa kumteua mgombea u Rais ndani ya CCM kwa azimio tu. Hakuna utaratibu wala utamaduni huo..
 
Na akasema Jakaya Kikwete aliupotosha Mkutano Mkuu kuvunja Katiba.

Na akasema Mwana CCM anafukuzwa kwa mchakato uliopo kikatiba, wamevunja mara ya pili kwa kumtangaza sio mwana CCM tena.

Akasema Mkapa, Kikwete na Magufuli walijaza fomu siku wanaingia, na siku wanaomba kuongezewa muda.

Kiti cha Urais, Mzee Malissa anasema, kiko wazi kwa mwana CCM mwenye nia ya kukiomba chamani.

Mwisho kabisa akatuma ujumbe ambao kasema anataka ufike juu kabisa kwenye uongozi wa chama, kwamba hawatakubali tena kuburuzwa na hawataogopa tena kamwe viongozi wanaovunja Katiba.

=============

Right or wrong, the man's got some brass balls. A true patriot. Ana kende za chuma na za kizalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…