Aliyefuta somo la kilimo shuleni achunguzwe uraia wake na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

Mungai (Marehemu) japo alikuwa Mafinga ila inasemekana alitoka Kenya........ Agriculture ilikuwa somo zuri sana Kwa tuliosoma
 
Uko sahihi,hata hizo shule za kilimo zilikuwa na dhana za miaka ya 70.
 
Kilimo cha kisasa kinahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo zana bora za kilimo,tafiti,pembejeo pamoja mifumo ya umwagiliaji bado hapo mazao yanahitaji kuwepo mashine za kuchakata au kuongeza thamani ya mazao vyote hivyo ni changamoto bongo.
 
Mungai.

Miaka yetu, nyumbani na shule lazima use na kitalu cha bustani,iwe ni mboga au maua! Somo la Sayansi kilimo.

Ila kuna shule za sec watoto wanalima na kufuga

cc: weluwelu
 
Agriculture mbna ni somo kwa level ya advance, labda ungesema lirudishwe O level.
Kwahiyo kila mTanzania ana mawazo ya kupita advance?

Hili somo linatakiwa lianzie primary school hadi vyuoni.
 
Swala si kufuta somo la kilimo maana mpaka sasa zipo shule na vyuo bado zinafundisha somo hlo, swala ni je hao wasomi na wataalam wanatumiwa ilikuleta tija kwa taifa?
Kati ya Watanzania milioni 60 Wataalamu wako wangapi?. Kilimo ni tofauti na Rocket Science kwamba ukishajua hapo hapo unaweza kurusha Rocket. Kwenye kilimo lazima mtu azoee toka utotoni ili kilimo kiwe sehemu ya tabia yake.
 
Huu ulikuwa udhibitisho kwamba nchi hii kuna watu wana madaraka makubwa lakini kichwani ni hopeless
 
Mimi nimeanzisha kilimo cha kisasa nilipofika katikati naona naelekea kukwama maana ukwasi umekata. Nikaenda bank kuomba mkopo. Wamenipa mashart ambayo siwezi kutoboa. Nilidhani dhamana ya nyumba itanibeba kupata 50m nimalizie project yangu. Niliambiwa Bank Kuu imetuonya tusitoe mkopo bila mkulima kuanza kutoa mazao ya kwanza.

Mbali na kuwaonyesha shamba liliofikia 70% na lina mwaka na miezi 3 nikilihudumia bado wamegangana mpaka lianze kutoa mazao. Nikajiuliza hivi hawa huwa wanawakopesha wakina nani ikiwa bank statement yangu inaonyesha nina uwezo wa kupata hata hela ya pembeni ambayo ndiyo naitumia kuwezesha shamba kuwepo bado waligoma.

Issue hii nilimweleza afisa kilimo wa wilaya fulani. Akaniambia ukweli kuwa kuna pesa waliahidiwa kuweka kwenye alimashauri zihudumie mikopo na sisi kwa kushirikiana na wananchi tukaanzisha mradi wa kilimo skim tatu. Mpaka leo hakuna cha hela wala nini. Mradi unaanza kufa wananchi waliotumia nguvu zao wanaona serikali imewatupa.
 
Somo hili lilipaswa kuwa la lazima kwa ngazi za sekondari na msingi katika shule zote binafsi na za serikali
 
Kulazimisha watu wasome kilimo ni sera mbovu kama ile sera aliyoleta Nyerere ya kujenga vijiji vya Ujamaa, kulazimisha watu wahamie na mwishowe tukakumbwa na janga la njaa.
 
Tuna mfumo wa hovyo sn
 
Teuzi zote majina ni yaleyale ya watoto na wajuu unategemea nini? wanateuliwa kulinda maovu ya wazazi wao
 
Nilipenda hilo somo nikiwa shule ya msingi nilijua mambo mazuri na mengi kuhusu kilimo

Kwa kweli aliefuta hilo somo alitumia nini kufikiria?
 
Kulazimisha watu wasome kilimo ni sera mbovu kama ile sera aliyoleta Nyerere ya kujenga vijiji vya Ujamaa, kulazimisha watu wahamie na mwishowe tukakumbwa na janga la njaa.
Hakuna hasara yoyote taifa litapata tukilazimisha watu wasome kilimo sanasana tutajenga kizazi chenye uelewa mkubwa sana kuhusiana na mnyororo wa biashara na ajira uliopo kwenye kilimo.
 
Umesema vizuri sana ndugu yangu na hizi ndizo changamoto ambazo elimu yetu ilipaswa kuzitafutia ufumbuzi na kuzijibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…