Aliyeibua uozo wa vifaa tiba Tabora asimamishwa kazi

Aliyeibua uozo wa vifaa tiba Tabora asimamishwa kazi

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Bwana James Getogo wa Ishihimulwa Tabora amesimaishwa kazi pamoja na dada Rose Shirima kupisha uchunguzi. Wawili hao walionekana kwenye video wakijibishana juu ya kutumia vifaa tiba vya malaria vilivyopita muda.

=====

Watumishi wawili wa Afya wa Zahanati ya Ishihimulwa Rose Shirima na James Getogo waliohusika kwenye video ya mabishano iliyosambaa wamesimamishwa kazi kwa muda ili kupisha uchunguzi.

Watumishi hao wamesimamishwa kazi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Uyui, Tabora Dr. Kija Maige ambaye amesisitiza kuwa wawili hawa wanapisha uchunguzi kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003.

“Uchunguzi huo utashirikisha Mabaraza yao ya kitaalamu ambayo ni Baraza la Wauguzi Tanzania na Baraza la Wataalamu wa Maabara Tanzania na hatua zaid zitafuata baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.
 
Kwakuwa tayari Serikali imeaibika....
Rose na James watasimamishwa kazi kama ilivyoahinishwa na kaimu mkurugenzi wa wilaya, then baada ya uchunguzi wote tunajua nini kitafuata kwa majibu ya (hapakuwa na dawa zilizo expire) na mwisho tutaambiwa kwamba tume imebaini (watumishi Rose na James walikuwa kwenye tofauti zao binafsi na wakazileta kazini) hivyo tume itawapa onyo kali ili iwe fundisho kwa wengine na kisha watahamishwa vituo vya kazi.

Kwa mtazamo wangu, Mganga mkuu na Mfamasia mkuu wa wilaya ndio walipaswa awajibike kwanza kwenye hili saga kwa kutoondoa dawa zilizo expire na kutokuwajibika.
 
Kwenye sekta ya afya kuna madudu mengi sana hasa kwenye awamu hii.
Yaani unahitaji huduma, muhudumu anakujibu atakavyo.

Hapo huyo dada angemjibu tu kistaarabu kuliko kumshushua ili hali ni kweli inaonesha mrdt zimekwisha muda wake.
 
Mfichua uovu anasimamishwa kwa minajili gani?

Is this a cognitive dissonance?
Zipo hatua za kufuata katika kuibua maovu....Nadhani wapo viongozi katika hospitali zao na hata wilayani ilitakiwa afikishe malalamiko huko lakini sio kurekodi na kutuma mtandaoni....Huo sio utaratibu.

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Zipo hatua za kufuata katika kuibua maovu....Nadhani wapo viongoz katika hospitali zao na ata wilayani .Ilitakiwa afikishe malalamiko huko lakin sio kurekodi na kutuma mtandaoni....Huo sio utaratibu.

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Anafanya mambo bila kufuata utaratibu kwa makusudi kabisa halafu anategemea huruma ya wananchi ambao hata hizo dawa hawajaziona zaidi ya kutuhumu kwa hisia tu.
 
Niliwahi kuzungumza na mwanamaabara mmoja akasema hizi rapid test zote malaria/ukimwi huwa hazitupwi mara tu zinapoexpaya.

Wanafanya kitu tukiite kukipima kipimo chenyewe. Huwa wanachukua wanatest kwa damu iliyo postive na hicho kitu halafu wanachukua kingine[cha batch hiyohiyo] wanatest kwa iliyo negative. Vikipatia kusoma basi hata kama ni mwaka umepita tangu viexpaye inaonesha bado vipo vizuri.

Na ifahamike wazi kwamba vipimo vinachofanya ni kucomfirm suspicion za dokta au kuzikataa. Na rapid test muda mwingine ni preliminary test nyingine zinafuata. Sio utaratibu lakini pia sio jambo la kutisha saaana kwa afya.

By the way vipimo vyote hata vilivyofata utaratibu kamili bado vinaweza kutoa majibu sio mfano, mbuzi na papai kuwa na korona. Wabongo hamjifunzi tu?
 
Kwani anaehusika kuagiza vifaa tiba na kuchunguza muda wake wa matumizi ni nani?

Kwa namna nilivyotazama ile video, hata huyo dada Rose simuoni kama ni muhusika, zaidi kwenye ile video anaonekana ana majukumu mengine kabisa, sasa sioni ni kwa vipi anaweza kuadhibiwa kwa kosa asilohusika nalo la kuagiza vifaa tiba vilivyopitwa na wakati.

Huyo mtumishi ni kweli amefichua, lakini amefichua kosa ambalo sio la dada Rose, labda Rose aadhibiwe kwa matumizi mabaya ya lugha aliyomtolea mwenzake, naamini pia hili litatokea endapo kosa hilo litakuwa miongoni mwa yale makosa aliyohusishwa nayo.
 
sa huyo alierekodi kafichua maovu anasimamishwa vipi, hii ndio sababu watu wanaogopa kufichua maovu na yote hii ni sababu serikali haipendi kukosolewa mapungufu yake.
Amefichua au alikuwa na visa, anaanzaje kumrekodi mtu bila sababu na pia maadili ya mtumishi hayaruhusu taarifa kuwekwa mitandaoni.

Angemrekodi akapeleka kwa uongozi
 
Kwenye sekta ya afya kuna madudu mengi sana hasa kwenye awamu hii.
Yaani unahitaji huduma, muhudumu anakujibu atakavyo.

Hapo huyo dada angemjibu tu kistaarabu kuliko kumshushua ili hali ni kweli inaonesha mrdt zimekwisha muda wake.
Yule dada, alijua wako wawili tu, kumbe mwenzake anamrekodi,, kwa jinsi anavyomjibu inaonyesha huyo dada alishagamkataa huyo jamaa.

Ndo jamaa akaja na hiyo mbinu ya kumharibia kazi
 
Acha tusubiri majibu ya mchongo baada ya uchunguzi
Mkuu, unatarajia patakua na majibu zaidi ya (tume haihabaini dawa iliyo expire na hakuna dawa iliyo expire kwenye pharmacy ya zahanati hiyo....🤣
 
Back
Top Bottom