Aliyeibua uozo wa vifaa tiba Tabora asimamishwa kazi

Aliyeibua uozo wa vifaa tiba Tabora asimamishwa kazi

Niliwahi kuzungumza na mwanamaabara mmoja akasema hizi rapid test zote malaria/ukimwi huwa hazitupwi mara tu zinapoexpaya.

Wanafanya kitu tukiite kukipima kipimo chenyewe. Huwa wanachukua wanatest kwa damu iliyo postive na hicho kitu halafu wanachukua kingine[cha batch hiyohiyo] wanatest kwa iliyo negative. Vikipatia kusoma basi hata kama ni mwaka umepita tangu viexpaye inaonesha bado vipo vizuri.

Na ifahamike wazi kwamba vipimo vinachofanya ni kucomfirm suspicion za dokta au kuzikataa. Na rapid test mda mwingine ni preliminary test nyingine zinafuata. Sio utaratibu lakini pia sio jambo la kutisha saaana kwa afya.

By the way vipimo vyote hata vilivyofata utaratibu kamili bado vinaweza kutoa majibu sio mfano, mbuzi na papai kuwa na korona. Wabongo hamjifunzi tu?
Jana tumejaribu kuelezea tumetukanwa nilikuwa sijui kama griti thinkaz ni waovyo hivi mtu hajui na hataki kukubali hajui
Sheenz kabisa
 
Yule dada, alijua wako wawili tu, kumbe mwenzake anamrekodi,, kwa jinsi anavyomjibu inaonyesha huyo dada alishagamkataa huyo jamaa,,
Ndo jamaa akaja n hiyo mbinu ua kumharibia kazi
Kwa nini tusiwaze uwepo wa mtu wa tatu aliyerekodi?
Yawezekana kabisa waliokuwa wanabishana na hawahusiki na kurekodi au kutuma mtandaoni.
 
Niliwahi kuzungumza na mwanamaabara mmoja akasema hizi rapid test zote malaria/ukimwi huwa hazitupwi mara tu zinapoexpaya.

Wanafanya kitu tukiite kukipima kipimo chenyewe. Huwa wanachukua wanatest kwa damu iliyo postive na hicho kitu halafu wanachukua kingine[cha batch hiyohiyo] wanatest kwa iliyo negative. Vikipatia kusoma basi hata kama ni mwaka umepita tangu viexpaye inaonesha bado vipo vizuri.

Na ifahamike wazi kwamba vipimo vinachofanya ni kucomfirm suspicion za dokta au kuzikataa. Na rapid test mda mwingine ni preliminary test nyingine zinafuata. Sio utaratibu lakini pia sio jambo la kutisha saaana kwa afya.

By the way vipimo vyote hata vilivyofata utaratibu kamili bado vinaweza kutoa majibu sio mfano, mbuzi na papai kuwa na korona. Wabongo hamjifunzi tu?
Kutokujua vifaa vya kupimia vinavyofanya kazi nalo ni tatizo.
 
Madudu ni mengi sio Hospitalini tu ni sehemu nyingi lakini hii halifanyi kuwa sawa amekosa lakini hapa kujiuliza ni sababu zipi mmoja ku record ni nini hasa lengo? Maana hii ni wazi sio kitu kipya ila kwanini siku hiyo? Motives ni nini?

Maana hapa hawa labda makosa yao madogo tu lakini watu wengi wanawajibika hapa, hivi kweli msimamizi mkuu hajui dawa fulani zimeisha muda? sio kwamba kuna namna ya kuzi replace au hakuna mifumo hii ma Hospital?

Mimi sijui lakini kitu kimoja najuwa lazima kuwe na record na inventory check issue ni kubwa kuliko huyo dada. Kama ni mifumo basi shida hii iko Hospital zote. Mimi mke nilikuwa namuona kama ana gubu fulani tukienda Hosp kabla hajakubali dawa lazima apewe atizame expire date nilikuwa namuona kama gubu fulani hivi huwa namwambia mke wangu unadhani mtu ataweka kitu kime expire lakini sasa namuelewa.
 
Sheria msumeno. Amekiuka taratibu.

Alikuwa anatafuta umaarufu sasa anakwenda kupoteza kazi, mpuuzi kweli yule kijana.
Acha uzwauzwa, yule kijana ni mzalendo na shujaa kufichua uovu unaotendeka kwenye sekta ua afya. Mbona uko hivyo? Unafurahia wagonjwa kupimwa vipimo vyeki? tena mjamzito hapo kuna watu wawili tunataka kuwadhuru au kuwaangamiza. Mkoje lakini? Au ndio roho za uchawi imekujaa.
 
Ummy Mwalimu anatakiwa ajitafakari kuchezea uhai wa watu, kuing’ang’ania hiyo wizara ni sawa na yeye kufoji vyeti vya intensive care na kupewa kazi hospitali.

No one as personal issues na yeye, hiyo wizara ina matatizo mengi at service level and troubleshooting is technical.

Tatizo hapo sio wale nurses waliokuwa wanabishana bali ni watu wengi, including mwenye majukumu ya inventory control kwanini products ambazo have passed their due date bado zipo wakati zinaweza waletea madhara wagonjwa.

Watanzania tuna roho mbaya sana mtu kazi unayoililia huna technical skills za kuifanya unang’ang’ania tu kisa raisi wa nchi mnaelewana at personal level.

Dorothy Gwajima alikuwa mtu sahihi kwenye hiyo wizara, watu wanafanya mzaha na maisha ya watu. Yule nurse wa kiume anatakiwa kupangiwa kazi sehemu nyingine kwa ku expose uozo sio kuadhibiwa.
 
Hivi mtu akifichua maovu unamsimamisha kazi? Kumbe mtumishi wa umma hutakiwi kufichua maovu? Mimi nilijua atapewa zaidi kwa kufichua uozo huo, aisee mbona sasa mtumishi hatasema uovu wowote akiona, hata rushwa ikitokea mtumishi atakataa kabisa kufichua sababu atasimamishwa au kufukuzwa kazi, i hope huo sio msimamo wa Mh. Rais wetu, huyo James kaibua madudu nilijua atapewa hata promotion labda, Mmmhh Mungu tusamehe.
 
Acha uzwauzwa, yule kijana ni mzalendo na shujaa kufichua uovu unaotendeka kwenye sekta ua afya. Mbona uko hivyo? Unafurahia wagonjwa kupimwa vipimo vyeki? tena mjamzito hapo kuna watu wawili tunataka kuwadhuru au kuwaangamiza. Mkoje lakini? Au ndio roho za uchawi imekujaa.
Angeweza kuibua huo uovu bila kumrekodi mwenzake na kusambaza video.

Kwani yule nesi ndiye anayenunua hivyo vipimo? Au ndio mkuu wa hiyo zahanati??

Yule jamaa ni mpuuzi tu. Kwasasa anakesi ya kuketa taharuki kwa jamii kuwa hospitali za Serikali zina vifaa vilivyo expire.
 
Angeweza kuibua huo uovu bila kumrekodi mwenzake na kusambaza video.

Kwani yule nesi ndiye anayenunua hivyo vipimo? Au ndio mkuu wa hiyo zahanati??

Yule jamaa ni mpuuzi tu. Kwasasa anakesi ya kuketa taharuki kwa jamii kuwa hospitali za serikali zina vifaa vilivyo expire.
Yule nesi kauli zake ni mbaya sana zinachefua. Ndugu yule mdada anaakisi sura halisi ya wanawake wa kitanzania maofisini. Mimi huwa nikimwona mhudumu ni mwanamke sazingine naahirisha huduma yenyewe kama siyo lazima.

Wana nyodo, dharau, ni makatili hayana huruma wanakuharibia siku dakika ni nyingi. Mtumishi gani unamwambia mwenzako au unataka kuwa mfanyakazi bora, mara pita hivi, ligha za baamedi kabisa zile. Km ameolewa anayeishi naye yuko jehanamu tayari. Hapana yule hastahili kuwa nesi tena manesi wana viapo usisahau. Watu wenye viapo vya kweli nimeamini ni majasusi na wanajeshi siyo rahisi kusaliti viapo vyao.
 
sa huyo alierekodi kafichua maovu anasimamishwa vipi, hii ndio sababu watu wanaogopa kufichua maovu na yote hii ni sababu serikali haipendi kukosolewa mapungufu yake.
Hawajafukuzwa kazi bali wameondolewa ofisini ili uchunguzi huru ufanyike.
Umejiuliza haya?;
1. Kwanini hawajaongea wenyewe bila kuhusisha kamera?
2. Kwanini mdada alikuwa na jazba?

Haya yaweza kuwa majibu;
1. Huenda wana bifu la muda mrefu James ameamua kumchoma huyo dada

2. Huenda huyo dada haelewani na watu

3. Huenda walikuwa na mahusiano jamaa kapigwa chini naye anampigisha chini.

Note; Kutumia vifaa vilivyopitwa na muda si kosa la wauguzi bali ni UONGOZI

BAADA YA UCHUNGUZI YATAIBULIWA MENGI NDIPO WA KUFUKUZWA ATAJULIKANA
 
Angeweza kuibua huo uovu bila kumrekodi mwenzake na kusambaza video.

Kwani yule nesi ndiye anayenunua hivyo vipimo? Au ndio mkuu wa hiyo zahanati??

Yule jamaa ni mpuuzi tu. Kwasasa anakesi ya kuketa taharuki kwa jamii kuwa hospitali za serikali zina vifaa vilivyo expire.
Haha wabongo maboga sana.

Huyu jamaa ndiye zwazwa na huenda kesi ikamuelemea yeye.

Kama alikuwa na nia njema angeongea na uongozi na uongozi ukikaidi alikuwa na nafasi kwa siri kuwajulisha ngazi ya juu.
Aliuofanya ni utoto itakula kwake..
Kosa la huyo dada ni dogo...ni matumizi mabaya ya mdomo tu...vifaa havimhusu yeye
 
Huyu jamaa ipo siku atamrekodi mgonjwa nyeti na hiyo simu yake,maana anaonekana anapenda sn kurekodi
Hana maadili na hajui taratibu.
Hili lilipaswa kufanywa na mgonjwa na sio yeye.
Yeye ana access ya kuongea na mkubwa kuhusu vifaa kupitwa na wakati na wakayamaliza ndani kwa ndani
 
Back
Top Bottom