Hivyo kumbe ni uzembe wa kituo sio?
Hili sakata ni ndefu sana, jamaa aliyerekodi kafanya vizuri ila amefichua mapungufu ya wengi sana, na inaweza kula sehemu kubwa, kwanza Mfamasia wa Wilaya, yeye anatakiwa kuwa na orodha ya dawa/Vifaa tiba/Vitendanishi vinavyoexpire kila kituo kila mwezi, ripoti hizo anaziomba kwa Wafamasia/Watunza store wa vituo, yeye ndo awe anakumbusha kuhusu kuziondoa store dawa/Vifaa tiba/Vitendanishi vyote vilivyoexpire.
Pili, Mfamasia wa kituo/Mtunza store, huyo naye ana cha kujibu iweje Vitendanishi vimeexpire bado vipo store kwa matumizi, huyo ndo hasa mwenye makosa kabisa.
Tatu, Mganga Mfawidhi, huyo ndo msimamizi wa kituo, lazima apitie leja mali yake kila mwezi, lakin pia lazima apate ripot kutoka kwa mfamasia/Mtunza store kuhusu vitendanishi vilivyoexpire au kukaribia kuexpire ili vitembezwe viishe au avigawe kwa kituo kingine chenye mahitaji zaidi. Ikumbukwe bidhaa kuexpire kituoni kwako ni kosa.
Kosa la Mfamasia pale juu, itapelekea kumulikwa kwa CHMT yote, ambaye mkuu wake ni DMO, kama kutakuwa na uzembe kwa Mfamasia Wilaya means hata DMO hatoshi, means DMO hajaset regulatory system vizuri kwenye Halmashauri yake.
Na kama DMO hatoshi, na Mfamasia wa Wilaya akionekana ana makosa, vipi sasa kuhusu RMO?? Vipi kuhsu RHMT??