witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,704
- 47,260
Wanachomoa side mirrors? Kwanini?Kifupi pikipiki zetu za mchina hapa bongo ni kuwa nazo makini halafu madereva wetu ndio hivyo hata sheria hawajui. We mtu anaipepea pikipiki halafu mbaya zaidi hizo boda hazina hata ABS, tairi ikiloki wakati wa breki ya ghafla unaenda nayo chini kishujaa huku kichwa hakina helmet.
Haya ndio naona makosa mengi yanayofanywa na bodaboda wengi;
1. Kupita red light, hili ni tatizo sugu kabisa na lishaota tende
2. Kuovateki upande wa kushoto
3. Kutokufahamu nani mwenye kipaumbele cha kupita kwenye mzunguko
4. Kutovaa helmet na kuchomoa side mirrors
5. Usiku kutembelea high beam
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app