Wewe ni jiongo sana!
Kila mahala unapwaya. Ongeza knowledge bro. Unatia aibu.
Ni lini Moses Kulola na Emmanuel Lazaro walikuwa na mgogoro wa kugombea uaskofu?.
Ni kweli ugomvi haukuhusu uaskofu
Tatizo ni kanisa la TAG kutokujua matumizi ya karama na huduma
Moses Kulola alikuwa mwinjilisti maisha yake yote hajawahi omba kuwa awe mchungaji au Askofu na wala hakutamani hivyo vyeo aliridhika TU na kuwa mwinjilisti tena bure hata bila kulipwa hata mia akialikwa alilala maporini alisafiri Kwa miguu mikoa na mawilaya kibao
Akialikwa hakula hata chakula alifunga siku zote za mkutano akipewa kahela sawa asipopewa sawa Hakudai Kanisa lilikua kwa kiwango cha kutisha kipindi chake maelfu waliokoka si kwa sababu wana shida za maisha waliokoka watu wenye vyeo na maisha wasiohitajo maombi yeyote au huduma ya maombezi . Mfano Hadi Professor ISSA Shivji aliokoka kwenye huduma ya Moses Kulola
Tofauti na sasa waokokaji wengi wanachi shida au changamoto za maisha
kipindi cha Kulola wanaookoka walikuwa wengi kuliko wanaohitaji huduma za maombi au maombezi kama ilivyo sasa wahitaji huduma za maombi na maombezi wengi waokokaji wachache
Aliifanya TAG kuwa kanisa kubwa la kipentecoste pekee lililoogopwa Hadi na serikali
Ukaundwa mkakati wa kuliua na kulivunja vunja vipande .Moses Kulola akapewa uchungaji na umakamu Askofu vyeo visivyoendana na huduma na karama zake .Wakaanza kumbana afanye zaidi kazi za uchungaji na umakamu Askofu sio uinjilisti akawa mkaidi kuwa hataki wachungaji wengine wakamuunga mkono vita ikaanza kuwa wachumgaji sasa kanisa litakuwa linalipa mishahara wachumgaji hivyo kunakuja uhamisho
Wachungaji wakorofi wa maeneo kama kinondoni mchungaji Mhina na Temeke mchungaji Masalu nk wakawa wa kwanza kupewa barua za kuhama!!! Vita ikaanza hapo Temeke kupitia choir wakagoma mchungaji kuondoka na ilitokea baada ya kuona kuwa Mchungaji Mhina wa kinondoni alipohamishwa nafasi yake imejazwa na mchaga Ndugu yake kabisa na Askofu Emmanuel Lazaro .Kanisa la Temeke wengi walikuwa wasukuma Taarifa zikasambaa kuwa Askofu katoa kabila ingine kinondoni kaleta mchaga mwenzie.Makanisa yenye wasukuma wengi yakagoma wachumgaji kuondoka ndipo ikaanza vita ya Sukuma gang vis chaga gang ndani ya TAG Wanyakyusa wakaunga Na Waha pia wakaunga mkono Kulola
Walipomfukuza Akaondoka na wachumgaji kibao wa kisukuma kinyakyusa na waha.Baadaye yakazaliwa madhehebu kibao ya watu ambao wote walikuwa TAG Kuna wale waliosema hatuko upande wa Kulola wala Emmanuel Lazaro wakafungua makanisa yao kibao.nguvu ya TAG ikasambaratika mission ikawa acommlishe
Hadi Leo TAG haijapata mwinjilisti mwenye nguvu ambaye alikuwa Billy Graham wa Tanzania kama Moses Kulola
Wangenwacha abaki tu kama Mwinjilisti kanisa la TAG Leo lingekuwa kubwa kuliko KKKT kwani wachumgaji na waumini wengi sana wa KKKT na Anglican walihamia TAG