TANZIA Aliyekuwa Askofu Mkuu wa TAG, Prof. Rainwell Mwenesongole wa Upanga CCC ametwaliwa na Bwana!

Neno la Mungu linatutaka kuheshimu namlaka iliyo kuu kwa kuwa kila mamlaka imewekwa na Mungu.
Pia dini haipambanii mambo ya mwilini bali ya rohoni.
 
Umejitahidi ingawa kuna vitu vinamiss
 
Kanisa atakabidhiwa mchungaji Dr Kipilimba.
 
Bwana ametoa ,Bwanq ametwaa!jina la bwana na libariwe!! , mwanga wa milele na umuangazie ee bwana
 
Upo vizuri chief.
Unamfahamu marehemu mchungaji mwanjala wa pale sinza?
 
Umenena vizuri sana. Isipokuwa kuna marekebisho kidogo.
Mchungaji Muhina, alkuwa Dodoma kama sikosei.
Nadhani ila sina uhakika, Kinondoni kulikuwa na Mchungaji Sosi ama Swai sijui vizuri hapo.

Tatizo, lilikuja kuwa kubwa kwenye uhamisho wa Wachungaji. Mchungaji wa Temeke, Marehemu Masalu, wakati kanisa lake na yeye mwenyewe wamekataa masuala ya uhamisho, waliamuliwa kutengwa. Katika kutengwa huko, hawakutakiwa hat kuhost mikutano ya Injili.

Mzee Moses Kulola aligoma kuwekewa mipaka ya kuhubiri kwamba Temeke mfano kwa kuwa walitengwa, asiende kule kuhubiri. Alikwenda kuhubiri kule, kwa hiyo akaonekana ameasi amuri ya watawla akatengwa. Kila aliyemkaribisha mzee kufanya huduma ya mahubiri naye alitengwa na TAG. Na kazi ikawa TAG ya Mzee Emannuel Lazaro, kwenda kuzuia Mikutano ya Injili iliyokuwa inafanywa na Moses Kulola kwa kutumia dola. TAG walicontend kwamba, wanahubiri kwa dini ya TAG wakati TAG imewatenga, haiwatambui? Vita ikaendelea hata TAG wanaanza kuzuia ibada katika majengo yenye jina la TAG yanayounga mkono Injili ya Kulola kwa kuwa amekataa kutii amri ya kutokuhubiri TEMEKE, na hivyo ameasi uongozi na kanisa halimtambui. Mzee Kulola akasema Yeey aliitwa kuhubiri Injili ili watu waovu waache dhambi wamfuate Kristo.

Ilikuwa vita hata mara nyingi alikamatwa na kupelekwa mahabusu, wakati mwingine amekaa Butmba siku 7 bila chakula, kuna wakati alipewa sumu n.k, n.k. Lakini kila walipomwachia aliingia barabarani kupeleka Injili. Ndipo miaka ya 84 hivi, chini ya Edward Sokoine, akashauriwa yeye na watuwa Injili wenzake, wasajili kanisa lingine ili wapate Jina huru ya kuhubiria badala ya kuendelea kudhikishana kwa ajili ya jina la kanisa.

Mzee kulola hakutaka kuwa askofu hata siku moja. Nashangaa sana kuona huyu mtu aitwaye johnthebaptist akikomaa kwamba eti walikuwa wanagombania uaskofu!. Wapi na wapi?

Ahsante sana YEHODAYA kwa kufafanua.
 
Uko sahihi kanisa la EAGT lilisajiliwa hata bila kuomba usajili serikali ikatoa hati ya usajili bila EAGT kuomba usajili kumaliza mgogoro sababu Kulola aliapa kufa TAG wakati TAG hawamtaki serikali ikatoa hadi Jina la kanisa jipya la EAGT kumaliza mgogoro katiba walIpeleka Baadaye baada ya kusajiliwa sababu ilikuwa si rahisi kusajili kanisa enzi hizo bila kupata approval ya Dini kubwa ikiwemo TAG serikali ikatumia busara kumpa Kulola usajili wa kanisa jipya la EAGT bila kufuata taratibu za kawaida za usajili kumaliza vita na ugomvi ndani ya TAG sababu Askofu Emmanuel Lazaro alimuona Moses Kulola mwasi asiyetii mamlaka ya Askofu mkuu TAG na Kulola alimuona Askofu mkuu Emmanuel Lazaro mpinga Injili shetani asiyetakiwa TAG

Serikali ikaona isiwe kesi wakawapa EAGT hati ya usajili bila kuomba kumaliza mgogoro na mgogoro ukaisha
 
Meneja wa benki ndio kiongozi mkubwa. Serikalini? Khaa
kwa wakati ule sawa kabisa....wewe unachukulia nyakati hizi....kipindi hicho hiyo benki ya taifa ya biashara ilikuwa ni ya serikali....ni mashirika ya UMMA yaliyoheshimika sana...na alijiunga hapo akitokea NAIROBI UNIVERSITY alikopata degree yake...imagine miaka hiyo ya sabini...degree holders wakutafuta nchini
 
Swala Sio muda mtu anatumia kufikia upadre issue ni kuwa kabla kuwa padre anakuwa jobless anaupata upadre akiwa jobless
Mbona unakuwa na kichwa kigumu. Upadre watu wanaenda seminari walitokea shule ya msingi, wewe ulipokuwa form one ulikuwa na ajira? Sasa ulitaka waajiriwe watoto wadogo kisha wastaafu ndio waende seminari
 
Kulola alikuwa spiritual kwelikweli alikuwa akishika tu maiki akisema 'yooo' mapepo yanaanza kutimka hapo bado hajaanza kuhubiri.
 
Kulola alikuwa spiritual kwelikweli alikuwa akishika tu maiki akisema 'yooo' mapepo yanaanza kutimka hapo bado hajaanza kuhubiri.
Mwenisongole mwenyewe aliokoka kwenye mkutano wa Moses Kulola Temeke tena akiwa meneja wa Benki Enzi hizo watu wa vyeo waliokoka sana mkutano yake tofauti na sasa wanaookoka wengi wenye shida na matatizo na low class kwenye jamii

Kulola alikuwa na mvuto wa ajabu
 
Umenena ukweli mtupu tukiacha unafiki kuna maaskofu na masheikh ovyo kabisa nchi hii,walitusaliti wananchi wakaungana na magufuli kututesa .sina uchungu nao hata wakifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…