mambio
JF-Expert Member
- Mar 4, 2017
- 2,668
- 3,428
Neno la Mungu linatutaka kuheshimu namlaka iliyo kuu kwa kuwa kila mamlaka imewekwa na Mungu.Hiyo tafsiri yako kuwa Askofu ni mtumishi wa Mungu hivyo hapaswi kuwasemea na kuwatetea wanadamu ni tafsiri potofu kwa 100%.
Kama askofu hawezi kuwasemea na kuwatetea wanadamu wanaomzunguka huyo sio mtumishi wa Mungu bali ni tapeli wa kawaida sana kwa mgongo wa dini.
Wakati ule kanisa lake lilipokuwa linamsemea na kumpongeza Magufuli, halikujua kuwa Magufuli naye ni binadamu?
Utasemaje unampenda Mungu kama huwezi kumpenda jirani yako?
Kama kuna mamilioni ya watanzania wanateswa kwa dhuluma za Serikali, na wanakwenda kila jumapili kanisani kumlilia Mungu na kutoa sadaka zao, halafu wewe Askofu unapokea sadaka zao na kuzitafuna halafu hapo hapo unaogopa kufungua mdomo wako kuwasemea au kuwatetea watu hao dhidi ya serikali inayowatesa, wewe ni muovu mkubwa, na mbinguni unaweza usiingie.
Pia dini haipambanii mambo ya mwilini bali ya rohoni.