Mtakatifu Mtakatifu Mungu wa Majeshi analo kusudi kuruhusu kila jambo linalotokea duniani.
Yatupasa kukumbuka kuyatenda,kuyanena na kuyawaza yalio mapenzi yake..Yenye utukufu kwake,yenye heshima kwake ,yenye sifa kwake pekee.
Kila Nafsi itaonja mauti na duniani wote tu wapitaji na Mwenyezi Mungu anayo makusudi makuu ya kutufanya tuishi kwa kiwango tutakacho ishi.Ndugu zangu Tusiache kutubu {Toba} kila wakati kwa maana hatujui siku wala saa tutakayokutana na umauti.Haijarishi tunajulikana kiasi gani,haijarishi tuna vyeo vya namna gani,haijarishi tuna mapesa kiasi gani,haijarishi tuna elimu ya mapana gani,Haijarishi tu maarufu kwa kiwango gani..
Utu,wema,unyenyekevu,Ustahimilivu,Sadaka,Dhaka,Kusamehe,Upendo viwe nguzo ktk maisha yetu ya kila sekunde,dakika,saa,siku,wiki,mwezi,mwaka,miaka...