TANZIA Aliyekuwa Mbunge wa Mufindi na Waziri wa Elimu Awamu ya Tatu, Joseph Mungai afariki dunia

TANZIA Aliyekuwa Mbunge wa Mufindi na Waziri wa Elimu Awamu ya Tatu, Joseph Mungai afariki dunia

Apumzike salama huko aliko.nakumbuka alifuta michezo mashuleni huyu.
 
Pole sana Willy...kuondokewa na baba mzazi ni shughuli pevu.

Lala Salama Mungai.
 
Kuna watu humu ni kama vile hawatakufa. Labda niwakumbuahe tu, hakuna mtu anayekufa kwa sababu alimsema mtu yoyote au hakuna mtu ambaye hatakufa eti kwa sababu hakumsema mtu fulani.

Kifo ni cha kila mwanadamu, cha msingi unaposikia mwenzako amekufa, ujue wewe ndio unafuata na ujiulize umejiandaaje siku yako ikifika sawa sawa na imani yako? Yule aliyekufa hawezi kurudi, so whether umseme vibaya au vizuri, haitakusaidia. Tuweni binadamu.

Pole kwa wakiwa wote
 
SITTA, MAULID & MUNGAI da!!!!! sijui nilie au niomboleze Mungu aturehemu,ss waja wake
 
M
View attachment 431075
Joseph Mungai enzi za uhai wake

Habari za kushtusha toka chanzo cha kuaminika Hospitali ya Muhimbili kinathibitisha aliyewahi kuwa waziri wa Elimu ndugu Joseph Mungai na Mbunge wa Mufindi amefariki dunia.!

Geofrey Mungai mtoto wa Marehemu amesema marehemu alipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuanza kutapika mfululizo na kudhaniwa kwamba alikuwa amekula kitu kibaya.

Joseph James Mungai alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1943
Mungu akulaze pema peponi. R.I.P. Mhesh Joseph Mungai. Mufindi na Kitaifa ulitutendea mengi.
 
Ninakumbuka hawa wazee kwenye moja ya mabaraza ya uwaziri awamu ya kwanza
wizara ya afya - Aaron Chiduo
" fedha- Amir Jamal
" elimu- Mama Thabita Siwale
" kilimo- Jackson Makweta
huyo makweta alikuwa waziri wa elimu pia sikumbuki ni utawala gani sijui Mwinyi
 
Back
Top Bottom