Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Soma Mwenyewe halafu Tafakari

View attachment 3029878
Baada ya kuwa ameondoka?
Msaliti angeozozana na Lisu kwenye mikutano yake (basi kama ndio tuambieni mapema Lisu yupo upande gani)
Mwisho wa siku hizi zinabakia kuwa kauli za kilaghai na kupotosha wananchi.
Kuna pahala hamtaki kuwa wakweli ila muda utaongea.
Mwenye jicho kubwa anaona mgawanyiko uliojitokeza kutoka viongozi wajuu kabisa wa chama kwenye mikutano yao ya hadhara, kuna la kujifunza hapa
 
Soma Mwenyewe halafu Tafakari

View attachment 3029878
Chadema wakati mwingine ni vichwa ngumu aisee.kwa hiyo P msigwa alikuwa anakisaliti chama akiwa ndani ya chadema ? Common guys !! Mwenyekiti amekata zaidi ya Miaka 20 ,Leo mnafundisha watu democrasia? Serious ? Na Kabwe naye alikuwa msaliti eti? Na Dr slaa naye alikuwa msaliti? Daaaah
 
Soma Mwenyewe halafu Tafakari

View attachment 3029878

Maneno ya hovyo kabisa, leo eti Msigwa alikuwa msaliti, vijana wa CHADEMA wengi wamekuwa misukule ya Mbowe..!!

Msigwa ndio alikuwa anatetea demokrasia ya kweli ndani ya Chadema, alikataa rushwa na udikteta wa Mbowe, yaani Mbowe ndio awe kama Mungu mtu huko Chadema, hata ile kuruhusu mgombea mwingine ndani ya CDM agombee uenyekiti tu imekuwa dhambi kubwa , yaani ukionyesha nia ya kugombea uenyekiti utaonekana msaliti mkubwa sana..!!

Vijana wa hovyo wa Chadema hawayaoni yote hayo, bali mtu akiondoka sbb ya kutetea haki na demokrasia ndani ya CDM ataitwa msaliti au pandikizi la CCM, upuuzi kabisa kwa vijana wa aina hii..!! Stupid..!! CCM ni Chama cha wote, Chama huru na Chama Tawala, Chama chenye kuongoza kwa mifano ya kweli, uongozi Imara kwa kila mwananchi na kila mwanachama mwenye sifa ana ruhusa ya kugombea..
 
Msigwa ana undugu magu,kama alishindwa kununulika kipindi cha magu iweje anunulike kipindi hiki!
 
Maneno ya hovyo kabisa, leo eti Msigwa alikuwa msaliti, vijana wa CHADEMA wengi wamekuwa misukule ya Mbowe..!!

Msigwa ndio alikuwa anatetea demokrasia ya kweli ndani ya Chadema, alikataa rushwa na udikteta wa Mbowe, yaani Mbowe ndio awe kama Mungu mtu huko Chadema, hata ile kuruhusu mgombea mwingine ndani ya CDM agombee uenyekiti tu imekuwa dhambi kubwa , yaani ukionyesha nia ya kugombea uenyekiti utaonekana msaliti mkubwa sana..!!

Vijana wa hovyo wa Chadema hawayaoni yote hayo, bali mtu akiondoka sbb ya kutetea haki na demokrasia ndani ya CDM ataitwa msaliti au pandikizi la CCM, upuuzi kabisa kwa vijana wa aina hii..!! Stupid..!! CCM ni Chama cha wote, Chama huru na Chama Tawala, Chama chenye kuongoza kwa mifano ya kweli, uongozi Imara kwa kila mwananchi na kila mwanachama mwenye sifa ana ruhusa ya kugombea..
Cdm ukiwa against mbowe tu basi lazima upewe usaliti,vijana wengi wa cdm awajielewi!
 
Watu wanafanyiwa figisu na wakihama et wasaliti

BTW;Hata Mdee alikuwa anashobokea wanaohama chama kama hivi,Leo yuko wapi?

Wajinga tu ndiyo watadumu huko
 
Mchungaji Peter Msigwa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amepokelewa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM NEC kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Daktari Samia Suluhu Hassan

Alizaliwa Juni 8 1965, ni mwanasiasa Mtanzania aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Iringa Mjini (2015-2020)

Kwa sasa Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Hivi karibuni 30 Mei 2024 Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, alimshinda Mchungaji Peter Msigwa kwenye Cheo cha Uwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa.

Katika uchaguzi wa kanda hiyo uliofanyika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makambako, ambao ulikuwa na mchuano mkali, Sugu aliibuka kidedea baada ya kupata kura 52 sawa na asilimia 51 dhidi ya Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyepata kura 51 (asilimia 49). Matokeo hayo Mchungaji Msigwa hakukubaliana nayo kwa kile alichodai haki haikutendeka na alikata rufaa.

====

Kuhusu Mchungaji Msigwa kutaka kupewa Uwaziri na Hayati Magufuli soma:

1. Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa: Hayati Magufuli alitaka kunipa uwaziri na pesa lakini nilikataa

2. Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa
View attachment 3029802
Atakuwa kanuniliwa huyo
 
Chadema wakati mwingine ni vichwa ngumu aisee.kwa hiyo P msigwa alikuwa anakisaliti chama akiwa ndani ya chadema ? Common guys !! Mwenyekiti amekata zaidi ya Miaka 20 ,Leo mnafundisha watu democrasia? Serious ? Na Kabwe naye alikuwa msaliti eti? Na Dr slaa naye alikuwa msaliti? Daaaah

..Ccm is too big and well funded kulinganisha na vyama vya upinzani.

..demokrasia yetu haiwezi kuwa na tija kama hakutakuwa na chama mbadala kinachokaribiana nguvu na Ccm.

..tunapaswa kuwawezesha wapinzani kwa kuwapigia kura kwa wingi ili Ccm isiendelee kuwakandamiza, kuwanunua, kuwahujumu, na kudumaza nchi.
 
Mch. Peter Msigwa katimkia CCM kutoka CHADEMA.
Rai yangu ni kwamba, pande zote mbili zijizuie kurushiana maneno au kulaumiana.
Yaani, Msigwa ajizuie kulaumu chama alichotoka na wafuasi wa CHADEMA wajizuie kumlaumu Msigwa.

Sumaye na Lowassa walikuwa mawaziri wakuu wastaafu lakini walihama CCM wakahamia CHADEMA na maisha yakaendelea. Kwa hiyo mimi sioni kama kuna la pekee sana linalohitaji kulaumiana kati ya hizi pande mbili.
 
Mchungaji Ogopa Mungu na teknolojia
 
Attachments

  • VID-20240630-WA0018.mp4
    1.5 MB
Back
Top Bottom