njumu za kosovo
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 4,853
- 11,782
Huyo ndugu /wazazi wamemsusa tu kwa aibu aliyowatia wameona aone upande wa pili wa dunia ukoje kwanza kisha ndio atoke ili siku nyingine awe mwalimu mzuri kwa wenzieWakiwa chuo wanajiona wa watoto wa kishua
Ona Sasa huyo kakosa mdhamini wa kumwekea bond ya million 5 tu
Wakiwa chuo wanajiona wa watoto wa kishua
Ona Sasa huyo kakosa mdhamini wa kumwekea bond ya million 5 tu
Wakiwa vyuoni wanajiona wote wa watoto wa kitajirihii imenichekesha😄😃😅😅😅,.
Na pengine ndio sababu hasa ya kudanga vyuoni, hali ngumu za maisha
Ila wale waliomuua Mzee Kibao hawajafikishwa hata kwa courtKwa wazazi inaumiza.
Inasikitsha sana vitoto vya elfu bee badala ya kukazana na kusoma wao wanawaza mijegeje tu.Mmoja kati ya wanafunzi watatu kutoka vyuo vikuu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, waliodaiwa kumshambulia mwenzao wakimgombania msanii na mtangazaji wa vipindi vya redio, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku, ameswekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya jinai inayomkabili na wenzake hao.
Mwanafunzi huyo Mary Gervas Matogolo (22), mwanafunzi wa
Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, leo Mei 30, 2025.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, wanakabiliwa na jumla ya mashtaka manane ya kusababisha madhara kim-wili, kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali.
Mbali na Mary wanafunzi wengine waliopandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa tuhuma hizo ni Ryner Ponci Mkwawili wa
Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam na Asha Suleiman Juma, wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam (TIA) wanakabiliwa na mashitaka manane.
Hakimu Gwantwa, alitaja masharti ya dhamana, kuwa kila mshitakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, wenye barua za utambulisho, vitambulisho vya Taifa, watakaotia watakaosaini Bondi ya dhamana ya Sh5 milioni kila mdhamini.
Washtakiwa Ryner na Asha wametimiza masharti hayo na kuachiliwa huru kwa dhamana lakini Mary ameshindwa kutimiza
masharti hayo ya dhamana.
Hivyo Hakimu Mwankuga ameamuru apelekewe mahabusu gerezani mpaka Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena
Chanzo: Mwananchi
Nenda Chato ukalie vizuriIla wale waliomuua Mzee Kibao hawajafikishwa hata kwa court
Wazazi wengine hawataki mchezo kama mimi, hata kama hela ninayo naliacha huko linyooke kwanza!Wakiwa vyuoni wanajiona wote wa watoto wa kitajiri
Ona hilo limbukeni kwao masikini, wenzake wenye ushua usio wa kuigiza wamepata dhamana lenyewe linaenda kunyea ndoo
Yaani mabinti wadogo wakagombanie jitu zee kama Mwijaku waache kusoma.
SanaKwa wazazi inaumiza.
True hasa mmejinyima asome aje awaokoeKwa wazazi inaumiza.
Halafu kesho akiwa tajiri unamrudiaAngekuwa kijana wangu, Hata Mimi ningemuacha.
Anaweza akatoka na asijifunze jela si sehemu salama ya mafunzo kule ni kuzimu hakuna jema unaweza jifunza kuzimuNgoja akapate adabu kidogo huko jela yaani alichokifanya adhabu ya jela ni ndogo kabisa..
Vijuaji sana na huyo Mary nasikiaInasikitsha sana vitoto vya elfu bee badala ya kukazana na kusoma wao wanawaza mijegeje tu.
Kuwekewa dhamana huhitaji kuwa wa kishua/tajiri.Mbona umeyafanya masaibu ya mwenzako kuwa nongwa?Wakiwa vyuoni wanajiona wote wa watoto wa kitajiri
Ona hilo limbukeni kwao masikini, wenzake wenye ushua usio wa kuigiza wamepata dhamana lenyewe linaenda kunyea ndoo
Yaani mabinti wadogo wakagombanie jitu zee kama Mwijaku waache kusoma.
Kujifunza ni kujutia ujinga aliofanya na kuwa sehemu ile maana hakutakiwa kuwa jela kama angefata kilichompeleka daslm ndio maana yangu.Anaweza akatoka na asijifunze jela si sehemu salama ya mafunzo kule ni kuzimu hakuna jema unaweza jifunza kuzimu