Aliyemshauri Mbowe agombee alidhamiria kumdhalilisha na kukiua Chama

Hiii umetype ukiwa umelaza brain
 
Yupo sahihi kikatiba na hakuna alipokosea, tunachotaka ni uchaguzi huru na wa haki ili mwenye kukubalika awe mwenyekiti.

Hamuwezi kutaka demokrasia ndani ya chama halafu mnapita majukwaani kupinga mtu kuwania nafasi ndani ya chama.
 
Yupo sahihi kikatiba na hakuna alipokosea, tunachotaka ni uchaguzi huru na wa haki ili mwenye kukubalika awe mwenyekiti.

Hamuwezi kutaka demokrasia ndani ya chama halafu mnapita majukwaani kupinga mtu kuwania nafasi ndani ya chama.

Yupo Sawa upande Mmoja lakini hayupo Sawa upande mwingine. Huo upande mwingine ambao hayupo Sawa ndio umekibeba chama na utafanya chama chake kiendelee.

Ndio maana kuna watu wangepiga Kura Magufuli aendelee lakini wenye akili na macho wangekataa kwa maslahi ya chama.

Kuna Jambo ni HAKI yako lakini unaweza usilifanye kwa faida ya Familia, chama au taifa lako.
 
So long as katiba inampa haki ya kugombea tena, hakuna A wala B inaongezeka. Nyie ndio mnakuja kusema "katiba ni kakijitabu tu", stick to the rules, sio hisia. Wanachama wa CDM wanachotakiwa kufanya ni kuweka katiba ambayo ina ukomo wa uongozi na madaraka, haya mengine ni kutaka kutupia lawama zisizo na msingi wowote kikakuni.
 
amkumbuke aliyemshauri
Samahani,inaonekana upo kwa kazi maalumu! Kwani kuanzia hapa chini si mchezo! Angalia usiwe Condom!












 
Hawezi kushindwa.
Kikawaida atatumia any means kuhakikisha anashinda.
Hicho ndicho wapambe wake wanakitaka,

Anashinda Pambano lakini anapoteza Vita
Siasa ni mipango mkuu. Binafsi naamini kuna mipango. Kwa historia yao Bado siamini FAM na TAL ni maadui kwa kiwango cha kutokukaa chini na kukubaliana kuhusu hii vita.

Mpango unaweza kuwa ni:

1. Mbowe anashindwa, Lissu anashinda, Mbowe anakubali matokeo na kuahidi kutoa ushirikiano.

2. Panatokea mdahalo wa FAM v/s TAL, Lissu anajenga hoja zake vizuri, Mbowe anaitisha Press anaamua kujiengua na sababu ni Lissu kamshawishi kwa hoja.

3. Lissu anashindwa, Mbowe anashinda, Lissu anamuunga mkono Mbowe.
(Kwa maoni yangu hii somehow ni mbaya kwa CHADEMA na nzuri kwa CCM maana baada ya hapo CCM wataanza kuimba wimbo wa mbowe kung'ang'ania madaraka, kupenda pesa za ruzuku, chama cha wachaga n.k)

Kama hivi ni vita visivyo na ushirikiano baina yao, uwezekano ni TAL atachana na chama na sio nzuri kwa CHADEMA.
 
Wapambe wa mbowe kina sugu, ntobi, yeriko, boni yai wamemdanganya mbowe, Atashinda pambano ila atashinda vita
 
Yupo sahihi kikatiba na hakuna alipokosea, tunachotaka ni uchaguzi huru na wa haki ili mwenye kukubalika awe mwenyekiti.

Hamuwezi kutaka demokrasia ndani ya chama halafu mnapita majukwaani kupinga mtu kuwania nafasi ndani ya chama.
Ni sawa yuko sahihi kwa wakati usiokuwa sahihi. Lissu yuko sahihi kwa wakati sahihi.
 
Moja ya sifa kubwa na bora ya kiongozi ni kutambua majira na nyakati za kufanya maamuzi sahihi...

Bwana Freeman Mbowe ktk uchaguzi huu ndani ya CHADEMA ameonesha kuwa, huyu kumbe hakuwa kiongozi bali mpigania tumbo lake tu...

Kiongozi gani unayeshindwa kuandaa kiongozi wa kurithi kijiti cha uongozi wako? Anawezaje kupambana na Makamu Mwenyekiti wake wakati ndiyo ilikuwa fursa yake ya kujivunia kuwa ameandaa mrithi bora na akahakikisha anakalia kiti hicho...?

Ndugu Robert Heriel Mtibeli hakuna haja ya kulaumu washauri hapa...

Wa kujilaumu ni yeye meenyewe Freeman Mbowe kwa kushindwa kutumia vyema akili zake mwenyewe kufanya maamuzi sahihi...

Ameshindwa kabisa kuelewa kwamba, chaguzi za 2009, 2014 na 2019 chama na wanachama walisimama pamoja naye kumpigania aendelee kukiongoza chama hata alipopigwa vita na kuitwa kila jina baya na wapinzani wake CCM kwa kuwa hakuwepo mtu sahihI, makini na mwaminifu asiyehongeka au asiyeweza kukiuza na kukitelekeza chama kurithi mikoba yake...

Lakini safari hii, yupo mtu sahihi kabisa na mwenye sifa zote muhimu na za ziada kurithi mikoba yake kuongoza chama hiki muhimu ambaye ni Tundu Lissu na kila mtu wakiwemo CCM wenyewe wanajua kabisa, huyo jamaa hawezekaniki, hahongeki na yuko straightforward, mkweli, jasiri, na sifa zinginezo njema zote...

Kwanini yeye na chawa wake hawaoni hili?

Mimi nafikiri acha karma iamue.

Mission ya CCM na serikali yake tangu miaka hiyo ni kuifuta au kuiua CHADEMA systematically. Naona mission inakwenda kuwa accomplished chini ya Mbowe huyuhuyu...!!
 
Ni kweli Mh.Mbowe anasifa nzuri za kiongozi kuliko Mh.Lissu .ila kwa Tanzania tunahita kiongozi kama JPM. Ambaye ni Tundu lissu. Sasa ni Bora Lissu awe mwenyekiti kwa muda huu ili kurudisha Chadema ije angombee uraisi.Lissu muda huu anafaa
 
Inasikitisha kuwa Mbowe ameamua kuikataa heshima na kuikumbatia fedheha.
 
Baada ya uchaguzi ndio mtajua nguvu ya Mbowe.
 
Ni rafikiye mama Abdul, aliwahi kumpa hela azipeleke kanisani kule machame
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…