Aliyemuelewa Mkurugenzi wa TPA, Plasduce Mbossa atusaidie kufafanua hili

Ni kweli. Nafikiri wengi hawaelewi kazi ya TPA. Kwenye suala la bandari, watanzania tulikuwa watupu sana. Huu mjadala wa DP World ndio umetufungua kidogo, lakini safari ya ueleo bado ndefu. Tuendelee kuifahamu TPA si tu katika mitandao bali katika vitini vya TPA au serikali. Mwambukusi atakupotosha!

Pili, maelezo ya Mkurugenzi yanalengo ya kukazia na kutupilia mbali maelezo, eti DP World inamiliki mpaka bandari za Ziwa Tanganyika. viktoria na malawi. Mtaelewa tu!
 
Umeusoma Mkataba wa DP WORLD na Bandari ya Tanzania ?
 
Wazungu wanasema "Time will tell" wakimaanisha "Muda utaongea" hili suala la DP world hakina baraka ya watanzania haliwezi kuwa na matokeo chanya kamwe.

Mungu atupe uzima tutakuja kuambizana hapa hapa JF

Mama abdul na serikali yake wamefanya maamuzi yao bila kuwashirikisha wananchi
 
SiO Lazima wote muelewe ndugu slow learner
 
Kwahiyo Bandari zitaendeshwa na Dp World lkn ulinzi na usafi ndiyo utasimamiwa na TPA?
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Mi huwa siwaelewi kabisa serikali yangu , wananchi tupo zaidi ya M60
Lakini ni lazima tuite watu wa nje ndio watufanyie mambo yetu ya uchumi , hii sio sawa , na ndio maana tunabaki kuwa maskini wa kutupwa ili hali nchi yetu ni tajiri wa kutupwa !
Mungu atusaidie ipo siku tutaamka kutoka usingizi tuliolala !
 
Anayemiliki TPA ndiyo mwendeshaji wa TPA halafu wawekezaji wote wa ndani ya nchi na nje ya nchi wa TPA wao si waendeshaji bali wabia

Sasa Kama ni wabia , then wao wamewekeza bei gani ,na wanapata asilimia ngapi ,na sisi tunapata asilimia ngapi ,na mgao wa ajira ukoje , na vifaa vinavyotumika vina ubora gani ?
Watuambie !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…