Aliyemuelewa Mkurugenzi wa TPA, Plasduce Mbossa atusaidie kufafanua hili

Aliyemuelewa Mkurugenzi wa TPA, Plasduce Mbossa atusaidie kufafanua hili

Mauzo ya Almasi Mwadui yalipata ridhaa ya wananchi. Gesi Mtwara, Dhahabu, makaa ya mawe, SGR, Bwawa la Nyerere na ............na ..........na............
Binafsi sijawahi kutoa au kupewa fursa ya kutoa ridhaa ya miradi yote mikubwa ya serikali. Leo hii sauti zinatoka wapi.....? Au dhambi ni Rais Samia kuweka vitu hadharani!
Kama waliamua kuileta hadharani ili kupata ridhaa ya wananchi basi wangefanya hivyo lakini sio unafiki walioufanya bora hiyo iliyopita kifisadi kuliko huu unafiki ulofanya na awamu ya sita kujifanya wanashirikisha wananchi kumbe changa la macho ndio mana nasema haitokuwa tofauti na miradi iliyopita na kulaumiwa na wananchi sasa so msimamo bado uko pale pale DP ni kaa la moto tutarudi hapa nakwambia
 
"DP World atafanya kazi maeneo yaleyale aliyopewa kulingana na masharti ambayo tumemuwekea. Lakini bandari zote zitaendeshwa na TPA au mwekezaji mwingine au mwendeshaji mwingine wa ndani au wa nje ambaye tutakubaliana naye."

- Mkurugenzi Mkuu TPA, Plasduce Mbossa
Mbona yupo wazi kabisa, ni nini hujaelewa?
 
"DP World atafanya kazi maeneo yaleyale aliyopewa kulingana na masharti ambayo tumemuwekea. Lakini bandari zote zitaendeshwa na TPA au mwekezaji mwingine au mwendeshaji mwingine wa ndani au wa nje ambaye tutakubaliana naye."

- Mkurugenzi Mkuu TPA, Plasduce Mbossa
Hii iko kama ile ya bendera iliyokuwa kwenye gari ya wahamiaji haramu wa Ethiopia...kwamba inafanana na bendera ya CCM ila haihusiki na CCM?
 
Hii iko kama ile ya bendera iliyokuwa kwenye gari ya wahamiaji haramu wa Ethiopia...kwamba inafanana na bendera ya CCM ila haihusiki na CCM?
Tena yule jamaa ilikuwa apewe tuzo.

Ameifanyia nchi msaada mkubwa, kwani alikuwa anawahifadhi, au anachukua pesa na anawatowa nje ya Tanzania? Bila gharama kwa serikali hata senti moja.

Kuwashika sasa ni kujitia gharama, pesa zao tunakosa na kuwalisha tunawalisha juu.

Watanzania tuna tatizo la ujinga.
 
"DP World atafanya kazi maeneo yaleyale aliyopewa kulingana na masharti ambayo tumemuwekea. Lakini bandari zote zitaendeshwa na TPA au mwekezaji mwingine au mwendeshaji mwingine wa ndani au wa nje ambaye tutakubaliana naye."

- Mkurugenzi Mkuu TPA, Plasduce Mbossa
Duu nimehisi sina akili kabisa labda ndugu yetu lucas mwashamba
 
"DP World atafanya kazi maeneo yaleyale aliyopewa kulingana na masharti ambayo tumemuwekea. Lakini bandari zote zitaendeshwa na TPA au mwekezaji mwingine au mwendeshaji mwingine wa ndani au wa nje ambaye tutakubaliana naye."

- Mkurugenzi Mkuu TPA, Plasduce Mbossa
Ndio maana mnaitwa Misukule ya Mbowe ,mmeamunishwa katika siasa za kutafuta makosa bila kuhusisha ubongo 🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Tena yule jamaa ilikuwa apewe tuzo.

Ameifanyia nchi msaada mkubwa, kwani alikuwa anawahifadhi, au anachukua pesa na anawatowa nje ya Tanzania? Bila gharama kwa serikali hata senti moja.

Kuwashika sasa ni kujitia gharama, pesa zao tunakosa na kuwalisha tunawalisha juu.

Watanzania tuna tatizo la ujinga.
Na ndio maana mtu aliyeweza kutengeneza Bunduki ya kienyeji nchini Tanzania,Badala ya kupongezwa na kupelekwa VETA kuongeza elimu na labda baadae awe mgunduzi mahiri wa kutengeneza silaha nchini.

Badala yake anakula mvua 30 jela!

Au muuza gongo na mtengeneza gongo anakamatwa badala ya kumsaidia kuiwezesha iwe na ubora wa kiwango cha Whiskey...
Hiyo ndio Tanzania bwana!
 
Mamlaka ya Bandari haijafutwa, hii haiondoi ukweli kwamba mamlaka hiyo ina uwezo wa kutumia huduma za taasisi tofauti, kwa mfano makampuni ya ulinzi, usafi, ukarabati wa vifaa kama A.C., au hata utoaji huduma wa sehemu ya bandari kama ilivyotumia huduma za DP.

Haimaanishi kampuni ya usafi, ulinzi na mengine sasa yamekuwa mamlaka ya Bandari na yanaiondoa katika udhibiti na usimamizi.

Wote wanawajibika kwa mamlaka ya bandari kama top authority
Tatizo letu weng humu JF tunahukumu kwa kila kitu tusichokifahamu vyema. Biblia inasema 'watu wangu wanaangamia kwa ukosefu wa maarifa' ujinga wetu ndio umaskini unaotutesa..
 
Anayemiliki TPA ndiyo mwendeshaji wa TPA halafu wawekezaji wote wa ndani ya nchi na nje ya nchi wa TPA wao si waendeshaji bali wabia
Alichokifanya TPA ni sawa na wewe au mimi tuwe na nyumba ya kupangisha halafu tumkaribishe mpangaji kwenye nyumba hiyo.

Ukiweza kuielewa dhana nzima ya mwenye nyumba na wapangaji wake utakuwa umelielewa vyema suala zima la TPA kuwa mmiliki anayepangisha maeneo ya biashara katika bandari yetu.
 
Mimi kupiga sina shida nako , shida yangu ni kwenda kuficha pesa kwenye mabenki ya nje ,
Tungepiga marufuku kupeleka pesa nje ya nchi , hata Kama ni muwekezaji atumie mabenki yetu local , ndio tutaona mzunguko vizuri wa pesa . Na uchumi utakua !
Ukishasema kupiga hakuna shida umeharibu.
 
Back
Top Bottom